Aina 6 Ya Vyakula Vinavyo Tatiza Ukuaji Wa Mtoto Wako

Aina 6 Ya Vyakula Vinavyo Tatiza Ukuaji Wa Mtoto Wako

Vyakula hivi huenda vika zuia mtoto wako kurefuka inavyo faa.

Kumbuka ulipokuwa mtoto mchanga na mama alikuwa anakwambia kuwa kahawa itatatiza ukuaji wako? Ukweli ni kuwa hakuwa anakosea. Walakini, kuna aina ya vyakula vinavyo tatiza ukuaji wa mtoto wako vikiliwa sana. Hapa kuna orodha ya vyakula unavyo paswa kufikiria kwa makini kabla ya kula iwapo unataka urefu wa mtoto wako ufike kiwango kinacho faa.

Aina Ya Vyakula Vinavyo Tatiza Ukuaji Wa Mtoto Wako

Junk food stunt growth

1. Vitamu tamu (junk)

Kuna sababu nyingi sana za kukata vitamu tamu kutoka kwa lishe ya mtoto wako, na hapa kuna moja. Vitamu tamu kama jina linavyo ashiria havina umuhimu wa virutubisho na haviongezi chochote ila kufanya tumbo ya mtoto wako kujaa (na kuongeza hatari ya kisukari na uzito mwingi). Hakikisha kuwa mtoto wako anakula kiwango kidogo chako vitamu tamu tu.

soda is bad for your child's development

2. Soda

Vinywaji vilivyo na carbon huwa na phosphorous ambayo ni madini muhimu kwa ukuaji, ila vikinywiwa sana huenda vika athiri viwango vya kalisi. Utafiti umeripoti kuwa watoto ambao hunywa phosphorous huwa na mifupa isiyo na nguvu. Watoto wanapo zidi kunywa vinywaji visivyo na afya kama soda na vitamu tamu, ndivyo wanavyo punguza nafasi ya kutumia virutubisho mwilini vinavyo hitajika kwa ukuaji wenye afya. Punguza idadi ya soda wanazo kunywa ikiwa hutaki zi athiri ukuaji asili wa mtoto wako.

too much carbohydrate is not good for development

3. Wali

Wakati ambapo wali sio mbaya kwa mtoto wako -  wanga nyingi na protini chache zinaweza punguza ukuaji wake. Ikiwa sahani ya mtoto wako ina wanga nyingi kuliko protini, hii ni sababu ambayo inaweza athiri ukuaji wake. Kumbuka, viwango vidogo wakati wote. Watoto wanao kula lishe bora yenye viwango tosha vya wanga na protini wana nafasi zaidi za kufikisha urefu unao wafaa.

4. Vileo

Wakati ambapo tuna uhakika hauwapi watoto wako pombe ama vileo, ni vyema bado kufahamu, hasa kwa watoto wenye umri mkubwa. Masomo yana ashiria kuwa unywaji wa vileo unaweza tatiza ukuaji lakini cha kuhuzunisha ni kuwa watoto wengi bado wanakua na kunywa pombe. Hakikisha kuwa watoto wako wana fahamu hatari za vileo, na uwe mfano wa kuigwa wa tabia nzuri ya kunywa.

5. Soya
Hata kama haija dhibitishwa kisayansi kuwa soy huathiri ukuaji, soy isiyo chachu kama maziwa ya soy, maziwa ya bururu na tofu huwa na asidi ya phytic, ambayo hupunguza uwezo wa mwili kutumia kalisi. Kalisi ni muhimu kwa ukuaji wa mifupa, kwa hivyo kunywa viwango vingi vya soy isiyo chachu kuna weza athiri ukuaji wa mtoto wako.

sugar

6. Sukari

Watoto ambao hula sukari nyingi mara nyingi huwa wafupi ikilinganishwa na watoto ambao hula lishe zenye sukari ndogo. Kama wanga, sukari huongeza insulin kwenye mwili na kuthibiti mwili kukua vyema ipasavyo. Hata kama hupaswi kumpiga mtoto marufuku ya kula vitamu tamu vyenye sukari chache, hakikisha kuwa hawazoei.

Kumbuka: Hatu shauri kukaa mbali na vyakula hivi kabisa, kwani baadhi ya vyakula hivi ni muhimu kwa ukuaji wa mtoto wako. Kuwa makini kwa viwango na mara anazo kula ili akue kwa afya inavyofaa.

 

Soma pia: Majina Ya Watoto Wavulana Na Wasichana Yenye Maana Ya Dua Njema

Makala haya yalichapishwa tena na idhini ya theAsianparent kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio