Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Vyakula 7 Bora Kupigana Dhidi Ya Vidonda Vya Tumbo

2 min read
Vyakula 7 Bora Kupigana Dhidi Ya Vidonda Vya TumboVyakula 7 Bora Kupigana Dhidi Ya Vidonda Vya Tumbo

Orodha ya vyakula bora dhidi ya vidonda vya tumbo ina vyakula kama vile samaki, plantains, viazi vitamu na maziwa ya bururu.

Vidonda vya tumbo ama ulcers hutokea kwenye trakti ya kuchakata chakula ikiwemo tumbo na koo ya chini. Hufanyika asidi ya tumbo inapoharibu kuta za trakti ya kuchakata chakula. Kuhusisha vyakula bora dhidi ya vidonda vya tumbo kwenye lishe ni muhimu. Kula chakula kinachofaa husaidia kupunguza uchungu kwa wagonjwa wa vidonda vya tumbo.

Kwa watu wanaotatizika na ulcers, hakikisha kuongeza vyakula hivi kwenye lishe yako.

Vyakula Bora Dhidi ya Vidonda Vya Tumbo

  1. Plantain

vyakula bora dhidi ya vidonda vya tumbo

Plantains huwa sawa na ndizi. Husaidia kutuliza kuta za trakti ya kuchakata chakula na kupunguza uchungu. Pia zina antibakteria hasa zinapokuwa mbichi. Epuka kuzikaanga kwenye ufuta mwingi. Ufuta mwingi huchangia katika uchungu mwingi tumboni.

2. Maziwa ya bururu

vyakula bora dhidi ya vidonda vya tumbo

Watu wanaotatizika na asidi nyingi tumboni ama vidonda vya tumbo wanapaswa kuhakikisha kuwa wanakunywa maziwa ya bururu mara kwa mara. Yanasaidia kuponya vidonda vya tumbo kwa kasi.

3. Asali

vyakula bora dhidi ya vidonda vya tumbo

Asali ina saidia kupigana dhidi ya bakteria. Kula asali husaidia kutuliza tumbo inayouma. Kijiko kimoja cha asali kila jioni kabla ya kulala ama kuongeza asali kwenye lishe kama oats na vinywaji badala ya sukari. Tumia asali badala ya sukari kwenye vinywaji kama chai na kahawa.

4. Matunda na mboga

vyakula bora dhidi ya vidonda vya tumbo

Kwa wanaotatizika na suala hili, wanapaswa kuhakikisha kuwa kila lishe ina mboga na matunda. Karoti, sukumawiki, broccoli, kabichi, grapes na matunda ya kiwi. Matunda yana beta-carotene na vitamini c zinazolinda ukuta wa tumbo. Berries kama vile strawberries huwa na viwango vya antioxidants vinavyopunguza hatari ya vidonda vya tumbo na kupunguza maumivu yanayoambatana na vidonda vile.

5. Viazi vitamu

vyakula bora dhidi ya vidonda vya tumbo

Viazi vitamu vina vitamini A, inasaidia kupunguza vidonda vya tumbo. Kula viazi vitamu mara kwa mara kunasaidia kulinda dhidi ya kupata vidonda vya tumbo.

6. Samaki

vyakula bora dhidi ya vidonda vya tumbo

Samaki wanaokuwa na viwango vya juu vya omega-3 fatty acids husaidia katika kupunguza hatari zinazoandamana na vidonda vya tumbo. Mifano ya aina hizi za samaki ni kama vile mackerel, salmon na sardines.

7. Pilipili nyekundu

vyakula bora dhidi ya vidonda vya tumbo

Ina fahamika kwa kuwa na vitamini C nyingi. Vitamini C husaidia kulinda dhidi ya vidonda vya tumbo na kuviponya.

Mbali na vyakula tulivyoangazia, hakikisha kuongeza broccoli, kiwi, grapes, blueberries, pears na oats.

Wakati wote, hakikisha kuwasiliana na daktari wako akushauri kuhusu ratiba bora ya vyakula unapokuwa na vidonda vya tumbo.

Chanzo: WebMD

Soma Pia: Je, Kuna Uhusiano Kati Ya Kula Lishe Ya Mboga Pekee Na Kupoteza Uzito?

Got a parenting concern? Read articles or ask away and get instant answers on our app. Download theAsianparent Community on iOS or Android now!

img
Written by

Risper Nyakio

  • Home
  • /
  • Health
  • /
  • Vyakula 7 Bora Kupigana Dhidi Ya Vidonda Vya Tumbo
Share:
  • Je, Kiamsha Kinywa Kina Manufaa Mwilini?

    Je, Kiamsha Kinywa Kina Manufaa Mwilini?

  • Vyanzo 5 vya Kuhisi Uvimbe na Maumivu ya Tumbo

    Vyanzo 5 vya Kuhisi Uvimbe na Maumivu ya Tumbo

  • Dalili za Ugumba Kwa Wanaume na Jinsi ya Kujikinga Dhidi ya Hali Hii

    Dalili za Ugumba Kwa Wanaume na Jinsi ya Kujikinga Dhidi ya Hali Hii

  • Je, Kiamsha Kinywa Kina Manufaa Mwilini?

    Je, Kiamsha Kinywa Kina Manufaa Mwilini?

  • Vyanzo 5 vya Kuhisi Uvimbe na Maumivu ya Tumbo

    Vyanzo 5 vya Kuhisi Uvimbe na Maumivu ya Tumbo

  • Dalili za Ugumba Kwa Wanaume na Jinsi ya Kujikinga Dhidi ya Hali Hii

    Dalili za Ugumba Kwa Wanaume na Jinsi ya Kujikinga Dhidi ya Hali Hii

Get advice on your pregnancy and growing baby. Sign up for our newsletter
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • More
    • TAP Community
    • Advertise With Us
    • Contact Us
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2023 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
About Us|Team|Privacy Policy|Terms of Use |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it