Lishe Ni Nini Na Inapaswa Kuwa Na Vyakula Vipi Bora Kwa Afya?

Lishe Ni Nini Na Inapaswa Kuwa Na Vyakula Vipi Bora Kwa Afya?

Ufuta wenye afya unapatikana kwenye nazi, njugu, maziwa, cheese, nyama na husaidia katika kutengeneza seli na kusaidia membrane kuepuka kuharibika kwake.

Lishe ni nini? Ili kuelewa lishe, unapaswa kuelewa uhusiano kati ya lishe bora, afya na magonjwa. Unapaswa pia kuelewa jinsi virutubisho vinavyo athiri mwili.

Lishe huupa mwili virutubisho. Protini, wanga, ufuta, vitamini, fiber, madini na maji. Mwili wako unapokosa usawazishaji wa virutubisho, afya yako huenda ikawa na matatizo. Hii ndiyo sababu moja ya kuichukulia lishe yako kwa umakini. Tazama orodha ya vyakula bora kwa afya.

Kwa nini lishe ni muhimu?

Kama tulivyo angazia, lishe ndivyo jinsi chakula kinavyo athiri afya ya mwili wako. Chakula ni muhimu; huupa mwili wako virutubisho muhimu katika utendaji kazi wake.

 • Wanga

vyakula bora kwa afya

Jukumu la vyakula katika kundi hili ni kuupa mwili nishati ya kuweza kutimiza majukumu yake. Vyakula kama vile mahindi, maharagwe, ndizi mbichi, wali, viazi na vinginevyo.

Nishati huuwezesha mwili kufanya majukumu ya kila siku kama vile kutembea na kuongea, kukimbia na kuinua vitu vizito. Unahitaji nishati ili kukua.

 • Protini

vyakula bora kwa afya

Kundi hili lina vyakula kama vile nyama ya ng'ombe, nguruwe, kuku, samaki na nyama za wanyama wengine. Kundi hili huupa mwili amino acids ambazo zinahitajika katika ukuaji na maendeleo ya mwili. Na pia kutengeneza tishu za mwili na kuusaidia kupigana dhidi ya maambukizi ya inflammation.

 • Ufuta

Ufuta wenye afya unapatikana kwenye nazi, njugu, maziwa, cheese, nyama na husaidia katika kutengeneza seli na kusaidia membrane kuepuka kuharibika kwake.

Ufuta ni muhimu kwa:

 • Kusaidia viungo kutoa homoni
 • Kusaidia mwili kutumia vitamini
 • Kupunguza inflammation
 • Kuboresha afya ya ubongo

Ufuta mwingi unaweza sababisha kuongeza uzito mwingi, viwango vingi vya kolesteroli, maradhi ya figo na matatizo mengine ya kimwili. Aina ya ufuta unao kula ndiyo muhimu.

Vitamini

vegetables

Husaidia na utoaji wa nishati, kuponya vidonda, kutengeneza mifupa, kinga ya mwingi na afya ya ngozi.

Madini

Husaidia na afya ya moyo.

Kukula lishe sawa yenye matunda, mboga, bidhaa za maziwa, protini na nafaka husaidia kuhakikisha kuwa mwili una virutubisho tosha vya kutumia.

 • Vitamini A husaidia macho kuona
 • Kalisi na magnesium kusaidia misuli na kupunguza shinikizo la juu la damu
 • Vitamini C husaidia kuponya vidonda na kuboresha uwezo wa mwili wa kupigana dhidi ya viini
 • Iron husafirisha hewa mwilini

Hakikisha kuwa wakati wote, sahani yako ina vyakula bora kwa afya ili kuuwezesha mwili wako kutenda kazi inavyo hitajika.

Soma pia:Vyakula Bora Kwa Afya Ya Mwanamme Ili Kuboresha Afya Ya Kiume

Written by

Risper Nyakio