Lishe bora na yenye afya ni muhimu sana mama anapo nyonyesha. Anapaswa kuhakikisha kuwa anakula vyakula bora kwa mama anapo nyonyesha ili kuhakikisha kuwa utoaji wake wa maziwa ya mtoto hakuta athiriwa. Anapaswa kuhakikisha kuwa ako makini na viwango vya vyakula anavyo vikula.
Orodha ya vyakula bora mama anapo nyonyesha
- Samaki

Samaki ni chanzo kizuri cha protini, kwa mfano tuna ama tilapia zina wingi wa omega-3 ambayo mwili wako una hitaji. Vyakula vya baharini vina wingi wa mercury na kemikali zingine, punguza mara unazo zikula kwa wiki. Hakikisha pia unachagua aina zilizo na viwango duni vya mercury kama vile trout, tilapia na salmon. Epuka aina ya samaki kama vile papa ama swordfish kwani zina idadi kubwa ya mercury.
2. Pilipili kwenye chakula
Je, unapenda chakula kilicho na pilipili? Watoto wengi hawana tatizo na pilipili kwenye chakula, ila ikiwa mtoto wako ana sumbuliwa na gesi ama kuharisha, punguza kiwango cha pilipili unacho kula ama kuweka kwenye chakula chako.
3. Viungo
Viungo vyenye ladha nyingi kama peppermint, sage na parsley. Lakini kuna baadhi ya viungo ambavyo huenda vika athiri kiwango cha maziwa ambacho mwili wako una tengeneza. Kwa mfano, kula parsley nyingi huenda kuka athiri utoaji wako wa maziwa. Kuna baadhi ya wanawake wanao nyonyesha wanao athiriwa wanapo tumia dawa ya meno iliyo na peppermint.
4. Maziwa

Ni nadra mtoto kuathiriwa na maziwa, lakini ni vyema kuwa makini. Tazama ikiwa anapata matatizo yoyote baada ya kunyonya kama vile kutatizika kupumua ama ishara zingine.
5. Mayai, njugu
Kuna baadhi ya wazazi wanao penda kuwa linda watoto kutokana na mizio ya aina yoyote ile kwa kuto kula vyakula fulani. Kama vile mayai na njugu. Lakini hakuna utafiti dhabiti kuwa kuto tumia vyakula hivi kutatimiza lengo lako. Wasiliana na daktari wako ili akushauri zaidi!
6. Vinywaji vyenye sukari
Kumnyonyesha mtoto kutakufanya uhisi una kiu kingi. Unapo hisi kiu, hakikisha kuwa unakunywa glasi ya maji kila mara unapo nyonyesha. Hata unapo hisi kiu sana, epuka kunywa vinywaji vyenye sukari kama vile soda, kwani havina umuhimu wowote mwilini mwako, ili kukutwika kalori nyingi.
7. Vyakula vyenye gesi
Kama vile maharagwe, broccoli, na kabichi. Ikiwa mtoto wako ana gesi ama colic, hakikisha kuwa una jitenga na vyakula hivi kwa wiki chache kuona kama ishara hizo zitapungua. Hakikisha kuwa lishe yako ina vyakula bora mama anapo nyonyesha ili mama na mtoto wawe na afya.
8. Vileo

Epuka kutumia vileo kabisa katika kipindi hiki. Na unapo amua kunywa, usimnyonyesha mtoto hadi pale ambapo vileo hivyo vitaisha kwenye maziwa.
Soma Pia:Matunda 8 Ya Kula Unapo Nyonyesha Kuboresha Utoaji Wa Maziwa Ya Mama