Vyanzo vya ugonjwa wa asubuhi havijadhibitika bado. Huku wanasayansi wakizidi kufanya utafiti zaidi katika nyanja hii, wanawake wajawazito wanaweza kula chakula fulani kufanya mimba iwe kipindi rahisi zaidi. Tazama orodha hii ya vyakula bora vya kichefuchefu vinavyowasaidia wajawazito kukabiliana na hali hii.
Vyakula bora vya kichefuchefu na ugonjwa wa asubuhi
- Tangawizi

Tangawizi ni mmea wa mzizi wenye manufaa mengi. Baadhi ya manufaa haya ni kupunguza uchungu wa tumbo na kupunguza kichefuchefu. Ongeza tangawizi kwenye chai, maji na vyakula vingine unavyo tayarisha.
2. Ndimu

Ndimu zinasaidia kukabiliana na ugonjwa wa asubuhi. Ongeza ndimu kwenye maji, kuyapa ladha na kukuwezesha kunywa maji zaidi. Nusia ndimu ama vitu vyenye harufu sawa kupunguza hisia ya kichefuchefu.
3. Crackers zenye chumvi
Weka pakiti ya crackers karibu na kitanda chako. Zitakuwa chakula chako cha asubuhi mara tu unapoamka kwa miezi michache ijayo. Kula asubuhi kunapunguza kichefuchefu, lakini baadhi ya vyakula vina uwezo wa kuongeza hali hii. Ila, crackers zenye chumvi zinasaidia kukabiliana na hali hii.
4. Vyakula vya protini

Utafiti umedhihirisha kuwa vyakula vyenye protini nyingi kama mayai, samaki na nyama husaidia kupunguza kichefuchefu. Ikiwa unatatizika kula mojawapo ya vyakula hivi, chukua maharagwe na njugu.
5. Chakula baridi

Ili kupunguza kuhisi kichefuchefu, epuka kula vyakula moto. Badala yake, kula chakula baridi kama maziwa ya bururu, mchirizi wa baridi ama aiskrimu na matunda baridi.
6. Ndizi
Ndizi kila asubuhi unapoamka ama unapohisi kutapika inasaidia kutuliza hisia hiyo.
7. Tikiti maji

Tunda hili lina maji mengi yanayosaidia kuweka viwango vya maji mwilini juu. Kuwa na maji tosha mwilini kunaepusha kichefuchefu. Kula tunda ama kunywa sharubati ya tikiti maji.
Kunywa maji tosha na matunda, hasa matunda yenye viwango vingi vya maji kunasaidia kuweka kichefuchefu chini. Mazoezi pia yamedhihirishwa kusaidia kukabiliana na hali hii. Mazoezi yanapaswa kuwa mepesi na yasiyohusisha kuinua uzito mwingi. Yanaweza kuwa kama kutembea kwa dakika chache, kufanya kazi nyepesi kwenye nyumba ama kuogelea siku moja ama mbili kwa siku.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Mabadiliko Ya Maziwa Ya Mama Yanavyotendeka Katika Kila Muhula Wa Ujauzito