Utafiti zaidi ungali unafanyika kuhusu uhusiano kati ya lishe wakati wa hedhi na kupunguza uchungu. Hata hivyo masomo katika mada hii yanadhihirisha kuwa lishe bora na yenye afya huwa na manufaa kwa mwanamke wakati wa hedhi. Tunaangazia vyakula bora wakati wa hedhi vinavyosaidia kupunguza uchungu.
Ishara za muda kabla ya kipindi cha hedhi huwa kama vile; kufura tumbo, kuharisha, maumivu ya kichwa, maumivu ya tumbo, uchungu kwenye mgongo, uchovu na chuchu kuwa laini.
Vyakula bora wakati wa hedhi
- Matunda

Matunda yenye viwango vingi vya maji kama vile cucumber ama tikiti maji husaidia kuwa na maji tosha mwilini. Kula matunda kunasaidia kukabiliana na hamu ya kula sukari inayotokana na chakula kilichochakatwa. Matunda kama machungwa, strawberries, parachichi na nanasi.
2. Mboga za kijani

Mboga za kijani huwa vyanzo bora vya chuma, muhimu katika kutengeneza seli nyekundu za damu. Kwani mwili unapoteza damu nyingi katika hedhi. Baadhi ya mboga bora ni kama vile mchicha, sukuma wiki, broccoli na kunde.
3. Maji

Kunywa maji katika hedhi huwa muhimu ili kuhakikisha kuwa una maji tosha mwilini na kuwa hutapata maumivu ya kichwa. Kunywa maji tosha katika kipindi hiki kunalinda dhidi ya kufura tumbo. Zingatia unywaji wa maji tosha katika siku unazokuwa na hedhi.
4. Mayai

Mayai huwa na virutubisho vya chuma, vitamini B na protini zinazosaidia na PMS.
5. Samaki

Samaki huwa na virutubisho vya chuma, omega-3 na protini. Chuma husaidia kudumisha kiwango cha virutubisho vya chuma vinavyopotezwa mwilini katika kipindi hiki. Omega-3 husaidia kupunguza ukali wa uchungu. Pia kupunguza kusombwa na mawazo katika hedhi ambako ni maarufu.
6. Oats
Image credit: flickr
Oats huwa na vitamini A na B, chuma na kalisi. Kula oats wakati wa hedhi husaidia kulinda dhidi ya matatizo ya tumbo na kupunguza PMS.
7. Chokleti nyeusi

Chokleti nyeusi huwa na virutubisho vya chuma na magnesiamu. Magnesiamu inapunguza ishara za PMS.
8. Maziwa ya bururu

Kunywa maziwa ya bururu husaidia kulinda dhidi ya kupata maambukizi katika na baada ya kipindi cha hedhi.
Vyakula vya kujitenga navyo
- Pombe
Punguza unywaji wa pombe unapokuwa na kipindi cha hedhi. Kupoteza damu katika hedhi hupunguza shinikizo la damu na kufanya uchoke kwa kasi.
2. Vyakula vya kuchakatwa
Vyakula vilivyo chakatwa huwa na sukari na chumvi nyingi pamoja na kemikali za kuhifadhi. Zinazofanya ufure na mwili kubaki na maji mengi katika kipindi cha hedhi.
3. Vyakula vyenye pilipili nyingi
Kula pilipili nyingi katika hedhi hufanya uhisi uchovu mwingi, kufura tumbo na kujaa gesi tumboni.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Hedhi Isiyo ya Kawaida: Utambuzi, Ishara na Jinsi ya Kulinda Dhidi ya Vipindi vya Hedhi Visivyo vya Kawaida