Kitu cha kwanza ambacho wanawake wenye mimba hujuzwa wanapotunga mimba ni vyakula hatari kwa mama mjamzito. Sio rahisi kuwacha vyakula ulivyokuwa umezoea hapo awali kama kula sushi ama kunywa vikombe viwili vya kahawa kila siku. Hata hivyo, sio jambo la kutia wasiwasi kwani kuna vyakula vingi ambavyo mama mjamzito anaweza kukula. Tuna orodhesha baadhi ya vyakula ambavyo mama mjamzito hapaswi kula.
Vyakula Hatari Kwa Mama Mjamzito
- Samaki mbichi

Wanawake waliozoea kula chakula kilicho na samaki mbichi kama sushi ama samaki ambaye hajapikwa vizuri. Vyakula hivi vinamweka mama katika hatari ya kupata maambukizi ya viini na mengineyo kama Listeria, Vibrio, na Salmonella. Maambukizi haya yanamfanya mama akose maji tosha mwilini na kumfanya akose nishati mwilini. Katika visa hatari, huenda mtoto akapata viini hivi na kusababisha kifo chake. Bakteria hizi zinapatikana kwenye samaki mbichi, na maji na mimea iliyo ambukizwa. Ni muhimu kwa mama kujitenga na vyakula hivi anapokuwa na mimba.
2. Samaki wenye viwango vya juu vya zebaki
Zebaki ni hatari, na viwango vya juu husababisha matatizo kwenye mfumo wa neva, kinga na figo. Inapopita amniotic fluid na kumfikia mtoto, inasababisha matatizo ya ukuaji. Samaki wenye viwango vya juu vya zebaki ni kama vile tuna, shark, marlin na swordfish. Samaki bora katika mimba ni kama salmon, tilapia, haddock, trout na cod.
3. Nyama mbichi
Kula nyama mbichi ama ambayo haijaiva vizuri inahatarisha afya ya mama mjamzito. Inamweka katika hatari ya kupata maambukizi ya viini kama Salmonella na E. coli. Na kumweka mtoto katika hatari ya kupoteza maisha yake, kupoteza uwezo wa kuona, kukosa maarifa na kuwa epileptic. Mama mjamzito anapaswa kula nyama iliyopikwa vizuri na ikiwezekana kula chakula alichokitayarisha mwenyewe ama anachofahamu kilivyo tayarishwa.
4. Mayai mbichi

Mayai mbichi huwa na viini vya Salmonella. Inayosababisha ishara kama maumivu ya tumbo, kuharisha, kutapika na joto jingi. Inapomfikia mtoto, huenda ikasababisha kujifungua mtoto aliyefariki ama kujifungua kabla ya wakati. Mama mwenye mimba anastahili kuhakikisha kuwa chakula chake kina mayai yaliyoiva na kujitenga na vyakula vilivyo na mayai mbichi kama mayonnaise.
5. Pombe
Kunywa vileo katika mimba kunaongeza hatari ya kupoteza mimba ama kujifungua mtoto aliyeaga dunia. Mtoto aliyezaliwa na mama aliyekuwa anatumia pombe katika mimba huenda akawa na matatizo ya kimaumbile, matatizo ya moyo na kutatizika kiakili.
Mbali na vyakula hatari kwa mama mjamzito tulivyoangazia, mama mwenye mimba anapaswa kuepuka utumiaji wa kaffeini nyingi, vitamutamu vya kuchakatwa, na kuhakikisha kuwa anakula mboga na matunda yaliyosafishwa vizuri.
Soma Pia: Chakula Bora Katika Mimba: Vyakula Muhimu Kwa Mama Anapokuwa Mjamzito