Katika ujauzito, chakula cha mama hupita kwa mtoto pia. Vyakula ambavyo huenda vikakosa kuwa na athari hasi kwa mama huenda vikamwathiri mtoto. Orodha hii ya vyakula hatari kwa mjamzito inamwelemisha mama kuhusu madhara ya kuchukua vyakula fulani kwa afya yake na ya mtoto.
Vyakula Hatari Kwa Mjamzito
1.Chakula cha baharini chenye zebaki ya juu

Chakula cha baharini ni chanzo bora cha protini na omega-3 ambazo huhimiza ukuaji wa ubongo na macho ya mtoto. Hata hivyo, vyakula vya baharini vyenye viwango vya juu vya zebaki huwa hatari kwa mfumo wa neva wa mtoto unaokua. Kama shark, swordfish, marlin, king mackerel na tilefish.
2. Chakula ambacho hakijapikika
Katika mimba, mjamzito huwa katika hatari kubwa ya kupata sumu kupitia chakula. Ili kujitenga dhidi ya magonjwa haya, ni muhimu kuhakikisha kuwa nyama imepikika vyakula, kuepuka chakula kilichoweka kwenye jokofu kwa muda mrefu. Kupika mayai mpaka yaive vizuri.
3. Safisha matunda na mboga vizuri
Ili kutoa bakteria mbaya, safisha matunda na mboga vyema. Epuka kula sprouts mbichi na papai mbichi kwani zina bakteria zinazosababisha maradhi.
4. Kaffeini nyingi

Kaffeini hupita kwenye placenta na kumfikia mtoto. Ili kuwa salama, mjamzito anashauriwa kupunguza kiwango cha kaffeini na bidhaa za kaffeini anazochukua. Kisha kuwachana na unywaji wake kwa pamoja.
5. Mayai mbichi
Mayai mbichi pamoja na bidhaa zenye mayai mbichi. Kama vile mayonnaise na custards kwani zinamweka mama mjamzito katika hatari ya kupata salmonella.
6. Epuka pombe
Hakuna kiwango cha pombe kilicho salama katika mimba. Njia salama ni kuepuka unywaji wowote wa pombe. Wajawazito wanaochukua pombe huwa katika hatari ya kupoteza mimba ama kujifungua watoto wenye matatizo ya kimaumbile.
7. Chai ya mitishamba
Hata ingawa hakuna utafiti dhabiti unaoonyesha athari za chai ya mitishamba kwenye mtoto anayekua. Chai za mitishamba zinapaswa kuchukuliwa daktari anapompa mama kibali.
Chochote mama anachotia mdomoni katika mimba kinamfikia mtoto. Ni muhimu kuwa makini na lishe na kuhakikisha kuwa ni ya afya na salama kwa mama na mtoto.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Vidokezo 7 Vya Kuwa na Mimba Salama na Yenye Afya