Jokofu lako linapaswa kuweka chakula kikiwa freshi kwa muda mrefu, lakini aina fulani ya vyakula usivyofaa kuhifadhi kwenye jokofu. Kuna vyakula ambavyo kamwe havipaswi kuwekwa kwenye jokofu, kwani kufanya hivi kunaweza athiri ladha na ubora wake.

Hapa kuna orodha ya vyakula usivyofaa kuhifadhi kwenye jokofu lako ama friji ili kutengeneza nafasi ya kuweka chakula kilicho freshi zaidi.
1. Viazi

Kuhifadhi viazi kwenye jokofu kunaweza haribu ladha yake na kuvifanya vioze mbio. Badala yake, viweke kwenye karatasi na kisha uhifadhi mahali palipo baridi ama kwenye pantry iliyo kauka.
2. Vitunguu

Sawa na viazi, vitunguu huanza kuharibika vinapo achwa kwenye jokofu kwa kipindi kirefu. Ni vyema kuviweka mahali palipo kauka na penye hewa tosha. Kumbuka kuviweka mbali na viazi kwani vina sababisha viazi kuharibika kwa kasi zaidi.
3. Nyanya

Temprecha baridi kwenye jokofu huharibu nyanya na kuzifanya ziwe rahisi kubondeka. Ziweke kwenye bakuli juu ya meza yako ya jikoni.
4. Asali

Asali kamwe haiharibiki, na kwa hivyo hakuna haja ya kuihifadhi. Tengeneza nafasi zaidi kwa kuitoa kwenye friji yako.
5. Kahawa

Kahawa huokota harufu zinazo izingira, kwa hivyo kuihifadhi kwenye jokofu lako kutaiwacha ikiwa na ladha tofauti. Unyevu ulioko kwenye jokofu utachukua baadhi ya ladha iliyoko kwenye kahawa.
6. Kitunguu saumu

Sawa na viazi na vitunguu, kuhifadhi saumu kwenye jokofu kuta haribu hali yake na kuifanya ipate ukungu mbio.
7. Mkate

Kuweka mkate kwenye friji kutafanya ukose ladha na uharibike mbio. Badala yake, weka mkate wako kwenye karatasi isiyo kubalisha hewa kupita kwa temprecha za kawaida.
8. Peanut butter

Sawa na asali, unaweza iweka kwenye sehemu yako ya viungo bila kuwa na shaka kuwa itaharibika.
9. Mchele

Ni mchele tu ulio pikwa unao stahili kuhifadhiwa kwenye jokofu lako. Mchele ulio kauka unaweza wekwa kwenye sehemu yako ya viungo hadi kwa kipindi cha miaka 10 kwa mchele mweupe (ukiwekwa kwenye kontena isiyo pitisha hewa), na hadi miaka miwili kwa mchele wa hudhurungi.
10. Maharagwe iliyo kauka

Maharagwe yaliyo kaushwa, sawa na mchele, haya hitaji kuhifadhiwa kwenye jokofu. Kuyaweka kwenye jokofu kuta fanya yaanze kumea.
11. Ketchup
Hizi zinaweza dumu hadi mwezi mzima bila kuhifadhiwa kwenye jokofu kwanu acids zake huziweka mbali na kukua.
Soma Pia: Chakula Cha Mimba: Je, Ni Salama Kula Kitunguu Saumu Ukiwa Na Mimba?