Epuka Kula Vyakula Hivi Usiku

Epuka Kula Vyakula Hivi Usiku

Chakula ni kizuri kwa afya yetu na unahimizwa kula chakula chenye afya. Ila, ni vyema kula usiku wa maanani? Baadhi ya vyakula usivyopaswa kula usiku.

Mambo tofauti huenda yakakufanya ule ukiwa umechelewa usiku. Baadhi ya mambo haya huenda huwezi kuwathibiti. Walakini kuna vyakula usivyopaswa kula kabisa wakati wa usiku. Baadhi ya wakati hata kama umekula muda mfupi kabla ya kulala, huenda ukahisi njaa sana. Unajua baadhi ya vyakula usivyopaswa kula usiku?

Huenda ukawa na kazi nyingi sana baada ya kufika nyumbani jioni na wakati ulipo hisi usingizi, ulienda kulala ukiwa njaa. Na ukaamshwa baadaye kula. Na huenda ulikuwa unatarajia kuto kula siku ijayo kwa hivyo ukabuni ni vyema kula katikati ya usiku ili usihisi njaa sana. Haijalishi kesi yako ni gani. Kula usiku sana sio jambo la busara na lina hatari nyingi. Iwapo ni lazima ule usiku, kuna vyakula usivyopaswa kula usiku.

Vyakula 5 Usivyopaswa Kula Usiku

Mkate

vyakula usivyopaswa kula usiku

 

Mojawapo ya vyakula rahisi zaidi kununua ni mkate. Ni vigumu sana kupata kuwa kuna upungufu wa mikate hata kwenye maduka. Maduka yote hujaza bidhaa hii kwani wanajua kuwa watu wana ipenda na wata inunua wakati wote. Huenda ukapata kuwa baadhi ya nyumba zina bidhaa hii wakati wote. Kwa hivyo ni bidhaa rahisi kufikia unapo hisi njaa wakati wa usiku. Kula mkate, siagi na chai ama chokleti sio jambo jipya. Hasa iwapo unahisi uzembe wa kutayarisha chakula usiku ama hauna kitu cha kupika kwa nyumba. Ila sio jambo la busara ki afya kula hivi wakati wa usiku. Mkate una viwango vya juu vya wanga na sukari ambavyo huenda vikapandisha viwango vyako vya sukari. Na huenda vikaingiliana na viwango vyako vya nashati na kuathiri usingizi wako.

Chakula cha kukaanga kwa mafuta

Fried Foods To avoid at night

 

Vyakula hivi viko kila mahali kwani ni rahisi sana kutayarisha na watu wanavipenda kwa urahisi wake wa kupatikana. Hasa wakati ambapo unahisi uchovu wa kupika, vyakula hivi ni rahisi kununua na kula badala ya jitihada zote za kupika. Vyakula kama vile viazi vya kukaanga. Ila ni vyema kufahamu kuwa vyakula hivi vina mafuta mengi na vigumu kwa tumbo kuvichakata mbio. Kuto chakata chakula vizuri husababisha kuumwa na tumbo, kiungulia na pia kuathiri usingizi wako. Kaa mbali na vyakula vilivyo kaangwa kwa mafuta wakati wa usiku.

Chakula chenye pilipili

vyakula usivyopaswa kula usiku

 

Watu wengi wanapendelea chakula chenye pilipili nyingi. Ikiwa kwa supu kama vile ya samaki ama nyama ili kuongeza ladha yake. Pilipili hii huwa na kemikali ambayo huenda ika athiri utaratibu wa kuchakata chakula tumboni. Kaa mbali na chakula chenye pilipili nyingi wakati wa usiku.

 

Nyama nyekundu

Watu wengi wana uraibu wa kula chakula kilicho na nyama nyekundu wakati wa usiku. Nyama nyekundu ina viwango vya juu vya protini na huwa na fiber nyingi isiyo rahisi kuchakata na huchukua muda mrefu kuchakata. Unapokula nyama wakati wa usiku inaifanya vigumu kukichakata na unataabika kupata usingizi usiku.

Kahawa

Kahawa ni nzuri wakati wa asubuhi ama alasiri. Ila unapo kunywa kinywaji hiki wakati wa usiku, inakua vigumu sana kwako kupata usingizi. Kahawa ina baki mwilini kwa masaa mengi. Kwa hivyo, ni jambo la busara kuepuka kunywa kahawa masaa mengi kabla ya kwenda kulala.

Soma pia: Vyakula Ambavyo Unapaswa Kuepuka Katika Mwezi Wako Wa Kwanza Wa Ujauzito

ChanzoJumia

Written by

Risper Nyakio