Kuna watu ambao hawana tatizo kulala. Punde tu wanapo ingia kitandani, wanapata usingizi kwa urahisi. Huku wengine iki wabidi kusikiza muziki ama kuhesabu kinyume nyume kutoka 100-0 ili wawe wamepata usingizi. Wakati ambapo wengine wanakaa usiku mzima bila kupata usingizi. Huenda watu kama hawa waka amua kutumia tembe kuwasaidia kupata usingizi.
Utafiti ulio fanyika katika nyanja hii umedhihirisha kuwa usingizi na kupata usingizi usiku una athiriwa pakubwa na chakula tunacho kula kabla ya kulala. Kwa hivyo unacho kula ama kunywa kabla ya kuingia kitandani kina athiri pakubwa uwezo wako wa kupata ama kukosa usingizi. Kwa hivyo ikiwa una tatizika na usingizi, makala haya yata kusaidia pakubwa kugundua kuhusu vyakula vinavyo kusaidia kupata usingizi.
Tazama orodha yetu ya vyakula vinavyo kusaidia kupata usingizi

- Ndizi

Ndizi ni vyanzo vikuu vya magnesium na potassium ambazo ni muhimu katika kukusaidia kutuliza misuli iliyo shinikizwa. Pia zina tryptophan inayo badili serotonin na melatonin ambavyo ni vichocheo vya kutuliza akili na kufanya tunda hili liwe bora katika kupata usingizi.
2. Asali
Asali ina viwango vya juu vya glukosi na fructose. Glukosi ina upa mwili wako viwango vidogo vya nishati katika sukari ya damu, wakati ambapo fructose huchukua muda zaidi. Kwa pamoja, kemikali hizi mbili husaidia viwango vyako vya glukosi unapo lala. Na kupunguza viwango vyako vya kuwa makini na kukufanya ulale.
3. Njugu
Kuna aina nyingi ya njugu, kulingana na sehemu unayo ishi. Na watu wengi wanapendelea njugu, lakini je, ulifahamu kuwa mbali na ladha, zina umuhimu mwingine? Njugu zina wingi wa magnesium ambayo ina kusaidia kulala kwa urahisi.
4. Oats
Oats zinafahamika kuwa na fiber nyingi na kuwa bora katika kupunguza uzito wa mwili. Na ni bora kama kiamsha kinywa. Zina melatonin, vitamini, amino acids na madini. Kwa hivyo kama una tatizika kupata usingizi usiku, tayarisha bakuli ya maziwa na asali kabla ya kulala.
5. Maziwa ya bururu
Maziwa ya bururu maarufu kwa kimombo kama yoghurt. Ina wingi wa kalisi inayo tumika katika uchakataji wa vichocheo vya usingizi ambavyo ni melatonin na tryptophan.
Jaribu mojawapo ya vyakula tulivyo angazia ili kukusaidia kutatiza suala lako la kukosa usingizi usiku! Je, una vyakula zaidi vinavyo kusaidia kupata usingizi? Tujulishe kwa kuwacha ujumbe mfupi hapa chini!
Soma Pia:Usingizi Wa Mtoto: Mambo Ya Kufanya Na Kuto Fanya