Jinsi Ya Kuboresha Utoaji Wa Maziwa Ya Mama Kwa Njia Asili

Jinsi Ya Kuboresha Utoaji Wa Maziwa Ya Mama Kwa Njia Asili

Njia bora ya kuongeza maziwa ya mama ni kumnyonyesha mtoto wako zaidi na kula lishe bora na vinywaji vingi. Orodha ya vyakula vinavyo ongeza maziwa ya mama.

Kunyonyesha huenda kukawa na changamoto kwa baadhi ya wamama. Tofauti na inavyo aminika na wengi, kunyonyesha hakulingani na saizi ya chuchu. Wingi wa maziwa ya mama unalingana na idadi ya wakati ambao mtoto wako anatumia kunyonya matiti yako na pia vinywaji unavyo vinywa. Walakini, kuna wakati ambapo huenda ukahisi kana kwamba hautoi maziwa tosha ya mtoto wako. Unapaswa kuangalia lishe yako. Unakula nini? Tume tayarisha orodha ya vyakula vinavyo ongeza maziwa ya mama, kulingana na ushauri wa wamama wanao nyonyesha.

Kwa kitu chochote cha dharura, tafadhali usisite kumtembelea mtaalum wa wamama wanao nyonyesha. Daktari wako atakusaidia.

Baadhi ya vyakula vinavyo ongeza maziwa ya mama

Pap

Jinsi Ya Kuboresha Utoaji Wa Maziwa Ya Mama Kwa Njia Asili

Baadhi ya wamama wanao nyonyesha wana amini kuwa kunywa pap inaweza fanya upate maziwa ya mama nyingi iwapo utaikunywa mapema asubuhi na usiku. Hiki huwa chakula kikuu kwa wamama wanao nyonyesha huko Nigeria.

Kunu

Jinsi Ya Kuboresha Utoaji Wa Maziwa Ya Mama Kwa Njia Asili

Hiki ni kinywaji cha upande wa Kaskazini. Viungo vyake ni nafaka kama vile guinea corn, mtama, tiger nuts na viazi vitamu. Pia kinywaji hiki kina sukari na tangawizi.

Supu ya pilipili

Jinsi Ya Kuboresha Utoaji Wa Maziwa Ya Mama Kwa Njia Asili

Chakula hiki kinajulikana sana hasa, nchini Nigeria. Wamama wanao nyonyesha mara nyingi hulishwa supu ya pilipili kwa sababu inapaswa kusaidia katika unyonyeshaji. Kinasaidia kumpa nguvu baada ya kujifungua.

Maziwa ya ng'ombe

Jinsi Ya Kuboresha Utoaji Wa Maziwa Ya Mama Kwa Njia Asili

 

Ina maana kuwa unapo hitaji maziwa, unapaswa kuyanywa! Siri ni kupata maziwa yenye afya yaliyo ya ng'ombe pekee. Fulanis huichemsha na kuichanganya na fura. Huu ni mlo wa upande wa kaskazini mwa Afrika.

Mchele wa hudhurungi

Jinsi Ya Kuboresha Utoaji Wa Maziwa Ya Mama Kwa Njia Asili

 

Mbali na kukusaidia na kukupatia nishati zaidi inayo hitajika baada ya kujifungua, pia ina hormoni za kuboresha utoaji wako wa maziwa. Kubadilisha kutoka mchele mweupe hadi wa hudhurungi. Mbali na kuwa na ladha bora, inaweza saidia kupunguza uzito baada ya kujifungua.

Oats

vyakula vinavyo ongeza maziwa ya mama

Kula oats huenda kukasaidia na utoaji wako wa maziwa ya mama, oats zina viwango vya juu vya saponins na zina egemeza mfumo wa kinga mwilini. Na pia ni homoni za utengenezaji wa maziwa, kwa hivyo, ongeza oatmeal kwenye lishe yako. Pia ni muhimu sana katika kuboresha uchakataji wa chakula. Na huku ziki saidia kuthibiti uzito mwingi wa mwili wakati wa ujauzito. Ina faida nyingi za kuongeza viwango vyako vya maziwa ya mama unayotoa.

Divai iliyo na chachu

Jinsi Ya Kuboresha Utoaji Wa Maziwa Ya Mama Kwa Njia Asili

Kunywa glasi ya divai mara kwa mara (iwapo unaipendelea) itakusaidia na viwango vyako vya maziwa ya mama kwani inasaidia katika utoaji wa maziwa. Ina viungo vya protini na vyuma ambavyo ni muhimu sana katika utoaji wa maziwa.

Kitunguu saumu

vyakula vinavyo ongeza maziwa ya mama

Kitunguu saumu ni mzizi wenye faida za kimatibabu na pia ina ladha nzuri kwa chakula chako. Kinapo liwa kwa viwango vinavyo faa, huenda kikawa na faida za kuboresha maziwa ya mama kwa sababu watoto wanapenda ladha yake. Unapo pika, ongeza kitunguu saumu kwa chakula chako, ila sio kingi sana. Ime gunduliwa kuwa watoto hunyonya zaidi wakati ambapo mama anaongeza kitunguu saumu kwa lishe yake.

Chai

Chai ina mchanganyiko wa galactagogues. Kuna chai za kuboresha maziwa ya mama hasa zilizo tengenezwa kukusaidia kwa jukumu hili. Iwapo unataka kunywa chai, fuata maagizo yaliyo kwenye kifurushi. Viungo vingine vinavyo patikana kwenye chai hii mbegu za anise, red raspberry leaf, marshmallow root, goat's rue na zinginezo. Chai bora zaidi ni zilizo freshi.

Njugu

vyakula vinavyo ongeza maziwa ya mama

Zina kiwango cha juu cha protini na asidi za ufuta na zinaweza liwa na lishe yoyote. Njugu zina amino acids zinazo tengeneza serotonin ambayo ni muhimu kwa kunyonyesha. Njugu ni njia bora zaidi ya kuimarisha utoaji wako wa maziwa ya mama iwapo unataka kitu kitamu unaweza chagua marzipan.

Wamama walio nyonyesha pekee ni vigumu kuwa na viwango vya chini vya maziwa ya mama hasa wanapo kula vyakula vya afya. Boresha utoaji wako wa maziwa ya mama kwa kula vyakula hivi.

Tujulishe ulivyo kumbana na tatizo la kiwango kidogo cha maziwa ya mama.

Vyanzo: Legit NG

Soma pia: Secrets of the best breastfeeders in the world

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Ayeesha kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio