Aina Za Vyakula Vinavyo Kuweka Katika Hatari Ya Kuugua Kisukari

Aina Za Vyakula Vinavyo Kuweka Katika Hatari Ya Kuugua Kisukari

Boresha afya yako kwa kujitenga na vyakula vinavyo sababisha kisukari. Tumia asali mbadala wa sukari, pika chakula chako badala ya kununua hotelini.

Ni muhimu sana kuwa na afya bora, inayo changiwa pakubwa na aina ya vyakula unavyo kula. Fahamu vyakula vinavyo sababisha kisukari ili kujitenga navyo.

Vyakula vinavyo sababisha kisukari

  • Vyakula vyenye wanga wa kuchakatwa

 

vyakula vinavyo sababisha kisukari

Vyakula vinavyo tokana na ngano, sukari, mchele mweupe huwa vimetolewa kiungo muhimu cha fiber na madini na vitamini zenye afya. Vyakula vya wanga visivyo na virutubisho muhimu na vyenye sukari nyingi ndivyo adui wakubwa. Ni rahisi kuchakata na kuchangia pakubwa katika ongezeko la sukari kwenye damu na kuongeza insulin mwilini. Baada ya wakati huenda vikasababisha aina ya pili ya kisukari.

Badala ya vyakula hivyo, watu wana shauriwa kula mchele wa hudhurungi, ngano nzima na kuepuka matumizi ya sukari. Punguza ulaji wa vyakula vya kuoka kama keki, mandazi, na mikate.

  • Nyama nyekundu

vyakula vinavyo sababisha kisukari

Nyama nyekundu na iliyo chakatwa ni baadhi ya vyakula vinavyo sababisha kisukari. Nyama za kuchakatwa kama vile hot dogs na bacon huwa na viwango vya juu ya nitrates.

Kuna aina nyingi ya protini zenye afya, kama vile samaki, nyama laini ama nyeupe, mayai na nyama ya ng'ombe mara kwa mara. Kuna protini za mimea kama vile maharagwe, mbaazi na kadhalika ambazo unaweza tumia.

  • Vinywaji vyenye sukari nyingi

vyakula vinavyo ua manii mwilini

Vinywaji vyenye sukari nyingi kama vile soda, chai, kahawa, ice cream na kadhalika huongeza hatari ya kuugua aina ya kisukari cha pili. Vinywaji hivi huwa na kalori nyingi inayo sababisha ongezeko la uzito na kwa sababu sukari huenda ika sababisha insulin resistance.

Badala ya vinywaji hivi, tumia sharubati ya matunda freshi kutoka shambani. Kunywa maji angalau glasi nane kwa siku. Punguza matumizi ya sukari nyingi, kwa mbadala, tumia asali.

  • Saturated na Trans fats

vyakula vinavyo sababisha kisukari

Hivi ni vyakula vilivyo na viwango vikubwa vya mafuta yasiyo na afya. Huchangia katika ongezeko la cholestrol mwilini inayo sababisha kisukari. Trans fats hupatikana kwa wingi kwenye vyakula vya kuoka, vya kukaanga, vyenye mafuta sana na hata cheese.

Kama vile burgers, na butters. Badala ya kununua vitamu tamu kwenye hoteli na bara bara, nunua vyakula vyenye afya kama vile njugu.

Boresha afya yako kwa kujitenga na vyakula vinavyo sababisha kisukari. Tumia asali mbadala wa sukari, pika chakula chako badala ya kununua hotelini na uhakikishe kuwa una nunua vitamu tamu vya afya kama njugu.

Soma Pia: Faida Za Kiafya Za Kula Njugu Usizo Zifahamu

Written by

Risper Nyakio