Fibroids ni aina ya uvimbe unaotokea kwenye mfuko wa uzazi. Uvimbe huu huwa kwenye sehemu tofauti za fuko la uzazi, ndani ama juu. Kwa kimombo, uzimbe huu unafahamika kama uterine fibroids. Uvimbe huu huwa mgumu kadri unavyozidi kubaki mwilini. Hata kama hufanya mama atatizike kujifungua, mwanamke anaweza kushika na kubeba mimba hadi kujifungua hata akiwa na fibroids. Kuna baadhi ya vyakula vinavyo tibu uvimbe wa fibroids ambavyo wanawake wanapaswa kuzingatia.
Chanzo cha mama kupata fibroids hakija dhihirika, ila kuna baadhi ya sababu zinazo changia katika mwanamke kupata fibroids.
Vinavyo changia katika kupata fibroids

- Uzito wa mwili uliopitiliza
- Jeni, mwanamke kutoka kwa familia iliyo na historia ya kuwa na fibroids
- Ongezeko la viwango vya homoni za progesterone na estrogen
- Viwango vya sumu vilivyo pitiliza
- Kula lishe hafifu
Dalili za kuwa na uvimbe kwenye mfuko la uzazi
- Kuwa na hedhi ya kipindi kirefu ama kifupi zaidi, kisicho sawa
- Maumivu makali ya tumbo katika hedhi
- Kuhisi kana kwamba una mimba
- Maumivu katika tendo la mapenzi
- Kuhisi kuvimbiwa na tumbo
- Kuvuja damu nyingi zaidi katika hedhi
- Kuvuja damu iliyo na mabonge katika hedhi
- Kuumwa na kichwa
- Kuvimba miguu na kuumwa unapotembea
- Kutatizika kushika mimba
- Kuharibika kwa mimba
- Kuumwa na nyonga
Vyakula vinavyo tibu uvimbe wa fibroids

Limau linasifika kwa faida zake nyingi za kiafya. Sharubati ya limau ina uwezo wa kuondoa uvimbe wa fibroids. Ongeza kijiko kimoja cha sharubati ya limau kwenye glasi iliyo na maji ya vuguvugu kisha uongeze baking soda. Kunywa mchanganyiko huu kila siku kwa wiki chache

Tangawizi ina manufaa mengi kama vile kupunguza maumivu na kuboresha msukumo wa damu mwilini. Fibroids huambatana na maumivu kwenye tumbo, ambayo yanapuuzwa na utumiaji wa tangawizi. Mwanamke anaweza kunywa tangawizi kwa kuiongeza kwenye chai yake ili kuondoa uvimbe kwenye mirija ya uzazi na uterasi.

Asali ni muhimu katika kuondoa maji zaidi kwenye mirija ya uzazi. Kunywa asali badala ya sukari kwenye vinywaji kama kaffeini ama chai.

Wingi wa vitamini B6 na C katika kitunguu saumu husaidia katika kusawasisha viwango vya homoni mwilini mwa mwanamke. Saumu ina uwezo wa kutoa sumu mwilini na kuondoa uvimbe mwilini hasa kwenye kizazi. Ongeza kitunguu saumu kwenye chakula chako, pia una hiari ya kula punje mbichi za saumu.

Samaki wana mafuta ya omega-3 fatty acids yanayo saidia kutatua hali ya uvimbe kwenye mfuko wa kizazi.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Jinsi Ya Kung’amua Iwapo Mwanamke Ana Fibroids {Dalili Za Fibroids}