Vyakula 8 Vinavvyo ua Manii Vilivyo Hatari Kwa Wanaume

Vyakula 8 Vinavvyo ua Manii Vilivyo Hatari Kwa Wanaume

Soy ina manufaa mengi ya kiafya na pia ina ladha ya kupendeza. Ila ikiwa wewe na mchumba wako mko katika juhudi za kutunga mimba, ni vyema kukaa mbali.

Kuna baadhi ya vyakula ambavyo ni hatari sana kwa wanaume. Hata ingawa hawafahamu athari hasi ya vyakula hivi. Hasa kama wanandoa wana jaribu kupata mtoto, ni vizuri kujitenga na vyakula hivi kwani vinaua manii na kupunguza nafasi yao ya kupata mtoto. Je, unavifahamu vyakula vinavyo ua manii mwilini mwa wanaume.

Vyakula 5 vinavyo ua manii mwilini

  1. Switi na vinywaji vyenye sukari nyingi

vyakula vinavyo ua manii mwilini

Kwa miaka mingi na kufuatia utafiti, sukari nyingi imehusishwa na athari hasi mwilini kama vile ongezeko la uzito mwilini, matatizo ya moyo na kupunguza utendaji kazi wa akili yako. Mbali na hayo, utafiti wa hivi majuzi una dhibitisha kuwa kula sukari nyingi ama bidhaa za sukari kuna punguza idadi ya manii na ubora wa manii. Ni muhimu kwa mwanamme kupunguza ulaji wake wa sukari ama bidhaa za sukari.

2. Nyama iliyo chakatwa

vyakula vinavyo ua manii mwilini

Nyama inaweza kuliwa kwa njia tofauti. Kama vile baada ya kuchakatwa inapo tengenezwa kuwa vitu kama bacon, ham na hotdogs. Bidhaa hizi zina kemikali nyingi za kuzisaidia kuzihifadhi kwa muda mrefu. Kemikali hizi ni hatari kwa manii na zinapunguza ubora wake. Baadhi ya nyama zingine za kuchakatwa huwa na homoni nyingi iki linganishwa na nyama ya kawaida na hivi basi kuathiri viwango vya testosterone mwilini ambayo ni homoni inayo saidia na utengenezaji wa manii mwilini.

3. Vileo

Vyakula 8 Vinavvyo ua Manii Vilivyo Hatari Kwa Wanaume

Unywaji wa viwango vingi vya pombe na vileo vingine vina ongeza kiwango cha homoni ya estrogen mwilini mwa mwanamme. Homoni hii ina sababisha ama kupunguza idadi ya manii yanayo tolewa. Mbali na kupunguza manii mwilini, pombe ina athiri maini. Ikiwa mna jaribu kupata mtoto, ni vyema kujitenga na unywaji wa pombe.

4. Bidhaa za soybean

Soy ina manufaa mengi ya kiafya na pia ina ladha ya kupendeza. Ila ikiwa wewe na mchumba wako mko katika juhudi za kutunga mimba, ni vyema kukaa mbali na viwango vingi vya soy na bidhaa za soy. Kwani idadi kubwa ya bidhaa hii huiga athari za estrogen mwilini na kupunguza kiwango cha manii kinacho tolewa mwilini. Manii yanapo pungua, nafasi zenu za kutunga mimba pia zina pungua.

5. Mboga na matunda yenye bidhaa za kuhifadhi 

Bidhaa za kuhifadhi matunda, mboga na vyakula vingine vina saidia sana katika kufanya chakula hicho kidumu kwa muda zaidi. Ila, vina athari hasi kwa mwili wako, hasa baadhi ya madawa yanayo tumika, huenda yaka sababisha mwanamme kushindwa kuzalisha. Kwa hivyo ni vyema kula mboga na matunda yanayo limwa bila utumiza wa kemikali.

Chanzo: healthline

Soma PiaVyakula 5 Vya Kuboresha Ubora Na Idadi Ya Manii Mwilini Mwako

Written by

Risper Nyakio