Vyakula 8 Vitakavyo Msaidia Mtoto Wako Kuongeza Uzito Wa Mwili

Vyakula 8 Vitakavyo Msaidia Mtoto Wako Kuongeza Uzito Wa Mwili

Oats zina kiasi kikubwa cha wanga na zina fiber nyingi. Zina baki tumboni kwa muda mrefu kwa sababu wanga huchakatwa pole pole zaidi.

Ulezi huja na majukumu mengi. Ni wakati katika maisha ya mzazi ambapo kutafuta usawa wenye mafanikio kwake ni muhimu. Mojawapo ya vitu vigumu zaidi kusawasisha ni lishe. Wazazi baadhi ya wakati huwaangalia watoto wao na kushangaa ikiwa wanapata lishe bora, hasa wanapo onekana wembamba kwa macho yao. Kuna vyakula vinavyo wasaidia watoto kuongeza uzito kwa njia yenye afya.

Hapa kuna vyakula vinavyo wasaidia watoto kuongeza uzito kwa njia inayo faa

Hata kama wazazi wangependa watoto wao wembamba kuongeza uzito zaidi, wako makini kutowalisha vyakula vya kuchakatwa. Kwa sababu hakuna afya na huenda waka pata tatizo la uzito mwingi. Changamoto ni kuchagua vyakula vilivyo na afya na vitakavyo msaidia mtoto kuongeza uzito.

Ikiwa una azimio la kuongeza uzito kwa watoto kwa kutumia vyakula vyenye afya, hapa chini kuna anuwai ya vyakula ambavyo hata kama watoto wako wana penda kuchagua chakula, hawawezi pinga.

  • Viazi

potatoes in the fridge

Watoto wengi wanapenda viazi. Vinaweza tayarishwa kwa njia tofauti kama vile kuchemshwa, kutayarisha vibanzi ama hata kubondwa kisha kupakuliwa na mboga ama nyama. Viazi vina amino acids na wanga nyingi inayo saidia kuongeza uzito.

  • Mandizi

matunda salama kwa mjamzito

Mandizi yana patikana kwa urahisi katika sehemu nyingi. Yana wingi wa wanga ambao unaweza wasaidia watoto kuongeza uzito. Mandizi yanaweza liwa ama kusiagwa pamoja na maziwa na matunda mengine kutengeneza smoothie.

  • Maziwa

vyakula vinavyo wasaidia watoto kuongeza uzito

Maziwa ni muhimu sana kwa mifupa. Yana kalisi, ufuta na vitamini zingine zinazo saidia mifupa kuwa na nguvu. Hata hivyo, kuna baadhi ya watoto walio na mzio wa maziwa. Ikiwa mtoto wako ana tatizika na mzio wa aina hii, ni vyema kumpa vyakula vingine tulivyo angazia.

  • Asali

vyakula vinavyo wasaidia watoto kuongeza uzito

Hata kama asali ina bei ghali, ni bidhaa ambayo itamsaidia pakubwa mtoto wako. Asali ina sukari asili, na unashauriwa kuitumia badala ya sukari ya kuchakatwa.

  • Oats

food for one year old baby in nigeria

Oats zina kiasi kikubwa cha wanga na zina fiber nyingi. Zina baki tumboni kwa muda mrefu kwa sababu wanga huchakatwa kwa upole zaidi. Zina patikana kwa urahisi kwenye maduka makubwa.

  • Mayai

eggs and heart disease

Watoto wengi wanapenda kula mayai. Yana afya, na ni chanzo kizuri cha protini. Unaweza yatayarisha kwa njia tofauti. Unaweza fanya uamuzi wa kuya kaanga, chemsha ama hata kutengeneza omelet. Na watoto wako watafurahia. Kuna baadhi ya watoto ambao wana mzio wa mayai, hakikisha kuwa hali mayai ikiwa yana m-athiri.

  • Kuku

vyakula vinavyo wasaidia watoto kuongeza uzito

Kwa watoto wengi nchini Kenya, hii ina ashiria sherehe ama siku kuu. Watoto wana pata furaha zaidi wanapo sikia kuwa kuku atachinjwa. Ila sio wote wanao ipendelea vile. Kuku ni chanzo kizuri cha protini na phosphorous. Virutubisho hivi vina saidia mfumo wa neva, meno na mifupa. Pia ni chakula kilicho na kalori nyingi na kinaweza saidia katika kuongeza uzito.

  • Maharagwe

Vyakula 8 Vitakavyo Msaidia Mtoto Wako Kuongeza Uzito Wa Mwili

Sio watoto wengi wanao furahia maharagwe. Lakini kama unaweza tayarisha kwa njia ya kuvutia, bila shaka mtoto wako atakuwa na hamu ya kuonja. Maharagwe yana protini na kalori nyingi na yana weza pakuliwa na mkate, mayai ama rojo.

Hitimisho

Kuna watoto ambao ni wembamba kiasili. Lakini ikiwa uzito wa mtoto wako ni kwa sababu ya kuto kula, unaweza ongeza baadhi ya vyakula hivi kwenye ratiba yako. Vyakula hivi vitawasaidia watoto kuongeza uzito na vina ladha ya kupendeza.

Soma Pia:Vyakula Vya Watoto Vya Soko Vina Sukari Nyingi Sana Kulingana Na WHO

Written by

Risper Nyakio