Kusafisha kizazi cha mwanamke ni muhimu anapojitayarisha kushika mimba. Ni mojawapo ya njia za kuandaa mwili kubeba mimba. Kizazi kina sehemu tatu, kuta ya nje ama perimetrium, kuta ya ndani ama myometrium na kuta zilizo ndani ya myometrium. Mwanamke asipo shika mimba, kuta ya ndani huporomoka na kutoka kama hedhi. Kuna njia kadha wa kadha ambazo mwanamke anaweza kutumia kama vile, kuzingatia ulaji wa vyakula vinavyosafisha mirija ya uzazi.
Je, kipi kinacho zuia kizazi kuwa na uwezo wa kushika mimba?

Fibroids husababishwa na vitu tofauti. Visa vya wanawake kutatizika na fibroids vimeongezeka katika miaka michache iliyozidi. Kubadilika katika mitindo ya maisha na lishe ni baadhi ya sababu zinazo wafanya wanawake kuwa na fibroids. Fibroids ni uvimbe unaofanyika kwenye kuta za uzazi. Ishara maarufu zaidi ya mwanamke kuwa na fibroids ni kushuhudia maumivu makali kabla ya hedhi na anapokuwa na kipindi chake cha hedhi. Kipindi cha hedhi pia huwa kizito kuliko cha kawaida. Wanawake wengi wanaougua hali ya fibroids hutatizika kupata mimba. Hata hivyo, mwanamke anaweza kutunga mimba akiwa na fibroids kisha kufanyiwa upasuaji wa kuzitoa baada ya kujifungua.

Afya ya mwanamke ni muhimu sana katika kuwa na maisha mema na afya bora ya kizazi. Mazoezi ni muhimu kwa afya ya mwanamke. Kutofanya mazoezi kwa muda mrefu kunapunguza nafasi za mwanamke kushika mimba. Kutofanya mazoezi kunapunguza mzunguko wa damu mwilini na kiwango cha damu kinacho fika kwenye kizazi. Kufanya mazoezi mara kwa mara kunaipa pelviki nguvu za kubeba na kustahimili kipindi cha mimba.
- Viwango vya homoni kutokuwa sawa mwilini
Homoni huchangia pakubwa katika mwanamke kushika mimba. Kuna mambo mengi yanayochangia homoni mwilini kutokuwa sawa. Hivi basi kuvuruga utendaji kazi wa sehemu zote za mwili inavyopaswa. Mwanamke aliyemakini kugundua mabadiliko yanayofanyika mwilini mwake atafahamu wakati ambapo homoni sio sawa mwilini. Kama vile:
- Kuvurugika kwa hedhi
- Hedhi inayo uma zaidi
- Hedhi ndefu zaidi ya wiki moja ama fupi ya siku mbili
- Kuwa na libido ya chini zaidi
- Kuhisi uchungu wakati wa tendo la ndoa
Jinsi ya kuongeza nafasi za kushika mimba

Mazoezi ni muhimu katika kuimarisha utendaji kazi wa mwili inavyo stahili. Mazoezi yanasaidia na kusawasisha homoni mwilini na pia kuipa misuli ya kizazi nguvu za kubeba mimba.
- Vyakula vinavyosafisha mirija ya uzazi

Chakula ni muhimu mama anapojitayarisha kutunga mimba. Zingatia ulaji wa chakula kinacho safisha mwili. Daktari wako atakushauri chakula bora katika safari hii.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Matibabu Asili Ya Fibroids Na Umuhimu Wa Lishe Bora