Vyakula Visivyo Na Acid Vinavyo Paswa Kuwa Kwenye Lishe Yako Wakati Wote!

Vyakula Visivyo Na Acid Vinavyo Paswa Kuwa Kwenye Lishe Yako Wakati Wote!

Kwa wanao tatizika na asidi nyingi mwilini, orodha hii vyakula visivyo na acid itakusaidia kufahamu vyakula unavyo paswa kula.

Unapo kuwa na asidi nyingi mwilini, ni ishara kuwa una tatizo la kiafya usilo fahamu. Kwa mfano kisukari, matatizo ya figo, mafua ama maini. Ni vyema kufahamu vyakula visivyo na acid na vilivyo na asidi ili ujue unacho paswa kula.

Vyakula vinavyo ongeza asidi mwilini:

vyakula visivyo na acid

 

  • bidhaa za maziwa
  • vyakula vya kuchakatwa vyenye sodium
  • samaki
  • nyama freshi na za kuchakatwa kama bacon
  • bidhaa za wanga kama mchele mweupe
  • vinywaji vyenye sukari nyingi

Kulingana na utafiti mpya, protini zinazo tokana kwa wanayma kama vile nyama nyekundu ina athiri pH mwilini na kuhusishwa na matatizo ya kiafya.

Vinywaji vyenye asidi:

Vinywaji kama vileo na mvinyo, chokleti moto na vinywaji vyenye sukari nyingi kama soda huwa na viwango vya juu vya asidi. Kunywa maji badala ya vinywaji hivi.

Vinywaji visivyo na acid

vyakula visivyo na acid

Maziwa ya bururu, maziwa, soy, na vinywaji vyenye herbs

Mboga za alkaline zinazo punguza asidi mwilini:

Mchicha, sukuma wiki isiyo pikwa, cucumber, uyoga, viazi, radish na zucchini

Athari za kula vyakula vyenye asidi nyingi

Lishe yenye asidi nyingi ni kama vile protini kutoka kwa wanayama ama vinywaji vyenye sukari ya kuongeza. Zina sababisha asidi kwenye mkojo na athari hasi kwenye afya. Na kukuweka katika hatari ya kuugua kidney stones.

Asidi nyingi mwilini pia ina sababisha mifupa na misuli kukosa nguvu. Punguza vyakula hivi kwenye lishe yako kwani vina athiri kiwango cha acid mwilini mwako na kuwa na athari hasi mwilini mwako.

  • Chumvi
  • Cheese
  • Ngano, nafaka na mchele mweupe

Hakikisha kuwa lishe yako ina virutubisho vyote muhimu, protini, wanga, vitamini na madini kisha uambatinishe na glasi ya maji. Punguza kiwango cha ufuta kwenye chakula chako. Zoea kula protini zinazo tokana na mimea. Matunda na mboga ni vyakula visivyo na acid na muhimu kwenye lishe yako. Kila mara unapo kula chakula, kina paswa kuwa na matunda na mboga. Kiwango cha asidi ama alkaline kwenye chakula sio muhimu kama kiwango kinacho tolewa mwilini baada ya kukichakata.

Soma Pia: Hakikisha Kuwa Sahani Ya Mlo Ya Mama Mwenye Mimba Ina Chakula Hiki!

Written by

Risper Nyakio