Vyakula 7 Hatari Kwa Afya Yako Vinavyo Sifiwa Kuwa Na Afya

Vyakula 7 Hatari Kwa Afya Yako Vinavyo Sifiwa Kuwa Na Afya

Katika juhudi za kufanya familia iwe na mtindo wa maisha wenye afya, wazazi huwa katika juhudi zisizo isha za kuongeza vyakula visivyo na afya kwenye lishe ya familia.

Katika juhudi za kufanya familia iwe na mtindo wa maisha wenye afya, wazazi huwa katika juhudi zisizo isha za kuongeza vyakula visivyo na afya kwenye lishe ya familia.

Lakini kufanya familia ile vyakula hivi ni vigumu, na matokeo huwa kuongeza vitu vinavyo wapatia hamu zaidi ya kula. Kwa bahati mbaya, hiari hizi huwa zimejificha chini ya kuwa za afya, lakini ukweli ni kuwa sio nzuri kwa afya yako.

Vyakula visivyo na afya vinavyo onekana kuwa na afya:

Hapa kuna hiari 7 zisizo na afya kulingana na listverse.

1.Mafuta ya kupikia

vyakula visivyo na afya

Katika somo la kemia, tulifunzwa kuwa ikiwa ufuta una uowevu zaidi, ndivyo ulivyo na afya. Kama sharti kuu, mafuta ya viowevu zaidi huwa rahisi kufika kiwango cha kuchemka kwa sababu ya kuwa na ufuta usio saturated. Mafuta kama vile ya mnazi huwa na aina mbaya ya ufuta(saturated) na yana tumika sana kupikia vyakula vya kukaanga. Watu wengi wana yapendelea mafuta haya kwa sababu ni ya bei ya chini.

2. Pasta

spinach

Image Credit: Crazy Vegan Kitchen

Pasta ni mbadala wa mchele na watu wengi hula wakidhani kuwa ina afya zaidi ikilinganishwa na wali. Ni kweli kuwa ina afya zaidi kuliko wali, lakini pale ambapo ni ya kutoka kwa nafaka nzima ama oat bran. Kwa bahati mbaya, pasta zinazo patikana sana katika nyumba nyingi huwa zimetengenezwa kutoka kwa unga ngano, kuchanganywa na maji na mayai.

Pasta ya kawaida huwa na viwango vya juu vya wanga tupu, vitamini kidogo na madini na haina fiber.

3. Mkate mweupe

Kama sharti la gumba, vyakula vyeupe ni vibaya kwako. Hivi ni kama vile, pasta nyeupe, mchele mweupe, mkate mweupe- kwa sababu zote hizi zina wanga tupu na havikuongezi virutubisho vyovyote kwenye lishe yako. Vinapo mmeng’enywa mwilini, vina badilika kuwa sukari, na isipo chomwa haibadiliki kuwa ufuta. Ikiwa lazima ule mkate, hakikisha kuwa unakula mkate ulio na viwango vya juu vya fiber na ulio tengenezwa kutoka kwa nafaka nzima.

4. Ketchup

Watu wengi hujadili kuwa ketchup ina afya. Hata kama ina viwango vya juu vya lycopene, ketchup zina idadi ya juu ya sukari. Na si hayo tu, ina kiwango cha juu cha chumvi pia. Ni vyema kutumia nyanya nzima na freshi ikilinganishwa na ketchup iliyo chakatwa na kuongezwa kemikali.

5. Diet soda

Soda ni mbaya kwa afya yako. Hata kama kuna aina mpya ya soda inayo fahamika kama diet soda ambayo ina aminika kuwa nzuri na yenye afya. Kulingana na utafiti, huenda diet soda zikakufanya upate hamu zaidi ya kula, na kusababisha kuongeza kalori zaidi ulizo jaribu kuhifadhi kwa kunywa diet soda.

Baadhi ya diet soda huwa na sukari ya kuongeza inayo fahamika kama aspartame, inayo husishwa na aina ya saratani.

6.Peanuts

vyakula visivyo na afya

Kwa jumla, njugu nyingi huwa na afya. Huenda zikawa na kalori, lakini zina vitamini, madini na fiber. Isipokuwa peanuts. Hizi ni njugu zilizo karangwa kwenye ufuta hatari kisha zika siagwa. Ikiwa una zingatia lishe yako, hakikisha kuwa unakula njugu karanga bila kuongeza chumvi.

7. Sharubati ya matunda

Kwa sababu tu lina neno ‘matunda’ haina maana kuwa ina afya. Baadhi ya watu hunywa sharubati badala ya tunda lenyewe, bila kufahamu kuwa aina hii ya sharubati huwa na sukari nyingi za kuongezwa. Badala ya sharubati iliyo chakatwa, una shauriwa kula matunda freshi kutoka shambani.

Soma Pia:Ratiba ya lishe bora ya kuzingatia nchini Kenya ya mama mja mzito

Written by

Risper Nyakio