Unavyo anza siku yako kutadhibitisha jinsi siku yako itakavyo kuwa. Kwa sababu hii, watu wanashauriwa kuhakikisha kuwa wanachukua kiamsha kinywa chenye afya wanapo anzia siku yao. Kuchukua kiamsha kinywa kizuri kutakusaidia kuwa na nishati tosha ya kuhimiza utendaji kazi wa mwili wako wa kawaida siku nzima. Kuna vyakula vingi sana ambavyo unaweza kula vya kiamsha kinywa chako.
Umuhimu wa kiamsha kinywa
Kwa watu wanao hitajika kuwa kazini mapema, huenda wakatatizika kupata wasaa tosha asubuhi kutengeneza kiamsha kinywa. Na kwa sababu hii, kukosa kula kitu chochote asubuhi kabla ya kutoka nyumbani. Kukosa kula kiamsha kinywa kuna athari hasi kwa wanao lenga kupunguza uzito wa mwili. Pia, utakosa nishati tosha, mhemko wako uathiriwe na hutaweza kufanya kazi zako za siku unavyo paswa.
Kumbuka kuwa, sio tosha kula kiamsha kinywa tu, mbali unapaswa kuhakikisha kuwa unakula vyakula vyenye afya. Hakikisha kuwa kiamsha kinywa chako kina protini, vitamini, kiwango cha fiber na wanga wenye afya.
Ikiwa una tatizika na vyakula vyenye afya vya kiamsha kinywa unavyo stahili kula, tume orodhesha baadhi ya vyakula ambavyo unaweza ongeza kwenye ratiba yako ya lishe ya asubuhi.
Vyakula vya kiamsha kinywa
- Oatmeal

Kwa wanao penda nafaka, oatmeal ni chaguo bora kwao. Ni nafaka nzima na iliyo na fiber, protini inayo tokana na mimea, vitamini B na madini kama vile iron na kalisi. Virutubisho hivi vinakusaidia kwa kupunguza hatari ya kupata maradhi ya moyo. Kufuatia viwango vyake vya fiber, utahisi kuwa umeshiba kwa muda mrefu.
2. Maziwa ya bururu
Maziwa ya bururu ni anuwai nzuri ya kiamsha kinywa. Ina virutubisho kama vile kalisi na vitamini B, protini na pia ina kalori chache. Hakikisha kuwa unachagua maziwa ya bururu yasiyo na ladha za kuongezwa ama matunda. Ukipenda unaweza ongeza matunda kama vile ndizi ama hata njugu.
3. Mayai

Badala ya kununua mikate ya kuoka iliyo na sukari na wanga nyingi, kula mayai kama kiamsha kinywa chako. Mayai yana vitamini A, D na B12, na protini. Mayai yana kusaidia kwa kuboresha mhemko wako, uwezo wako wa kukumbuka na uponaji wa misuli yako.
4. Viazi vitamu

Viazi vitamu vina wingi wa vitamini A na beta-carotene inayo saidia mfumo wako wa kinga. Pia ni muhimu katika kupunguza viwango vyako vya kolesteroli mbaya. Badala ya mikate, keki na bidhaa zingine za kuoka, hakikisha una kula vyakula asili kama viazi vitamu.
5. Ndizi mbivu

Wataalum wa lishe wana shauri kuwa kila lishe inapaswa kuwa na tunda. Ndizi ni tunda bora kula unapo anza siku yako. Utashudia upungufu wa mawazo mengi na pia mhemko wako utakuwa bora.
Soma Pia: Jinsi Ya Kutengeneza Ratiba Ya Lishe Nchini Kenya