Vyakula Vyenye Afya Vya Kuanzisha Uchungu Wa Uzazi Kiasili

Vyakula Vyenye Afya Vya Kuanzisha Uchungu Wa Uzazi Kiasili

Mafuta ya castor oil imekuwa ikitumika kwa miaka mingi na wanawake kuanzisha uchungu wa uzazi.

Wakati ambapo hakuna utafiti tosha kuegemeza imani kuwa vyakula vinaweza anzisha uchungu wa uzazi, wanawake wengi wana uhakika kuwa kuna vyakula vilivyo wasaidia kuanza uchungu wa uzazi. Hapa kuna baadhi ya vyakula vya kukusaidia kuanzisha uchungu wa uzazi kwa njia asili ambavyo wanawake wengi wamekiri kuwa vime wasaidia. Kwa hivyo ikiwa uko katika wiki zako za mwisho za ujauzito, na mtoto bado hajafika, hapa kuna baadhi ya vyakula vitakavyo kusaidia sana.

Orodha ya vyakula vyenye afya vya kukusaidia kuanzisha uchungu wa uzazi

  • Mananasi

matunda ya kuepuka katika mimba

Kulingana na baadhi ya wanawake, kula mananasi ni njia nzuri ya kufuata. Lakini, hakuna utafiti wa kudhibitisha haya. Enzyme ya proteolytic iliyoko kwenye mananasi freshi, na bromelain inaweza legeza tishu inayo zunguka mlango wa uke.

  • Papai

Papai za kijani ambazo hazija iva zina wingi wa enzyme ya papin. Majani ya papaya yana latex inayo fanya kazi sawa na prostaglandin na oxytocin na inaweza anzisha kubanwa. Kadri papai linavyo zidi kuiva, ndivyo papin inavyo zidi kupungua. Na ndiyo sababu kwa nini papai iliyo iva haiwezi athiri ama kusababisha kubanwa kwa uchungu wa uzazi.

  • Kitunguu saumu

vyakula vya kuanzisha uchungu wa uzazi

Kitunguu saumu huchechemua utumbo na kuusafisha na kunaweza saidia kuanzisha uchungu wa uzazi. Ni mojawapo ya chakula maarufu zaidi katika kutimiza lengo hili.

  • Chakula kilicho na pilipili

Wakati ambapo ni jambo maarufu kwa wanawake walio na mimba kula chakula kilicho na pilipili kuanzisha uchungu wa uzazi, ni kitu ambacho wanawake wanapaswa kuepuka, ikiwa wangependa kujifungua kwa njia asili bila kuhisi uchungu mwingi. Mtoto anapo zaliwa kwa njia asili, shinikizo inayo achiliwa mtoto anapo zidi kushuka chini ya kanali ya kujifungua, endorphins zina achiliwa na kutuliza uchungu.

  • Mafuta ya castor

kuanzisha uchungu wa uzazi

Mafuta ya castor oil imekuwa ikitumika kwa miaka mingi na wanawake kuanzisha uchungu wa uzazi. Hata kama ulaji wa mafuta ya castor oil sio salama, yanaweza sababisha kutapika na kuharisha kwa kesi nadra, na hautahisi starehe unapo shuhudia uchungu wa uzazi.

  • Zabibu

vyakula vya kuanzisha uchungu wa uzazi

Zabibu ni vyanzo vizuri vya nishati kwa wanawake walio chelewa kujifungua kufuatia kiwango cha juu cha wanga. Na kufanya zabibu ziwe chanzo kizuri cha nishati inayo kusaidia kuwa na nishati tosha ya kujifungua. Kulingana na utafiti uliofanyika, kula zabibu katika siku za mwisho za ujauzito kunaweza boresha kupanuka na kulegeza kwa mlango wa uke.

Hitimisho

Kumbuka kuwa sio utafiti mwingi uliofanyika kuhusu vyakula vinavyo saidia kuanzisha uchungu wa uzazi. Ila tulivyo dokeza vimetumika kwa muda mrefu na vime fanyiwa utafiti.

Soma Pia: Jinsi Tunavyo Fikiria Kuhusu Uchungu Wa Uzazi Kunaweza Badili Tunavyo Hisi

Written by

Risper Nyakio