Kwa miaka mingi, binadamu wamekuwa wakifanya utafiti kuhusu jinsi ya kuboresha maisha yao ya kingono ikiwemo, vyakula bora vya kuboresha ngono.
Kulingana na utafiti, kuna baadhi ya vyakula ambavyo watafiti wamehusisha na vitendo bora kitandani. Kwa wanaotatizika na maisha yao ya kingono, makala haya yanadokeza vyakula ambavyo wanapaswa kuongeza kwenye ratiba yao.
Vyakula vya kudumu kitandani

Kudumisha mfumo wa mzunguko mwilini ni muhimu kwa maisha bora ya kingono. Mzunguko bora wa damu na hewa mwilini unaongeza hamu ya kufanya tendo la ndoa katika wanaume na wanawake. Hasa kwa wanaume wanaotatizika kuwa na kibofu wima katika ngono. Moyo unaofanya kazi vyema ni muhimu kwa stamina na maisha bora ya ngono.
Lishe inapaswa kuwa na matunda na mboga nyingi. Ufuta wenye afya kama olive oil, nafaka nzima, fiber, legumes, njugu na seafood.
Vyakula kama parachichi, njugu, chakula cha baharini, matunda na asparagus zimedhibitika kusaidia katika maisha ya kingono.
Chakula cha kuboresha ashiki

Vyakula vinavyosaidia kuboresha ashiki vinafahamika kama aphrodisiacs.
Zinc ni baadhi ya madini ya mwili yanayohitajika katika utendakazi wa mwili wa kila siku kudumisha stamina na kudhibiti viwango vya testosterone. Oyster inafahamika kuwa aphrodisiac bora kwani ina viwango vingi vya zinc. Vyakula vingine vyenye zinc nyingi ni kama vile, njugu, nyama nyekundu, lobster, nafaka nzima na crab.
Hamu ya kufanya mapenzi inategemea vitu vingi kama lishe, hali ya uhusiano, mawazo mengi ya kimaisha ama kikazi.
Sababu zinazoathiri hamu ya kudumu kwa uume katika mapenzi:
- Matatizo na damu kuzunguka na kufika kwenye kibofu
- Kuwa na mawazo mengi ama wasiwasi
- Kuharibika kwa neva za kibofu
- Athari hasi za dawa na matibabu
Vyakula vilivyo na wingi wa flavonoid husaidia katika kuboresha hali ya mwanamme kudumu muda mrefu kitandani. Kama vile, tufaha, strawberries, grapes, berries, chai, na bidhaa za cocoa.
Watu wengi huzingatia vyakula vya kuboresha maisha ya kingono, kudumisha hamu yao ya kingono na kufurahia ngono zaidi. Ni muhimu kula chakula bora na chenye afya ili kuwa na wakati bora kitandani.
Chanzo: Healthline
Soma Pia:Tendo La Ndoa Katika Ujauzito: Wakati Wa Kuacha Kufanya Mapenzi Katika Mimba