Vyakula 5 Bora Zaidi Katika Kuongeza Hamu Ya Tendo La Wanandoa

Vyakula 5 Bora Zaidi Katika Kuongeza Hamu Ya Tendo La Wanandoa

Mchicha unasaidia kuongeza idadi ya L-arginine mwilini na kubadilishwa kuwa nitric oxide inayo saidia katika tendo la ndoa kwa wanaume.

Maisha ya mapenzi ni muhimu sana kwa wanandoa. Kwa sababu hii, binadamu wamezidi kufanya utafiti zaidi jinsi ya kuboresha utendaji kazi wako katika nyanja hii. Ili kuwa na maisha bora ya kimapenzi, ni muhimu kuhakikisha kuwa unakula lishe yenye afya na kujitenga na vyakula vyenye athari hasi kwenye afya yako. Kama vile vileo, mihadarati na sigara. Kuna vyakula vinavyo husishwa na kuboresha tendo la wanandoa. Soma zaidi.

Vyakula Bora Katika Kuboresha Tendo La Wanandoa

  1. Njugu

kuboresha tendo la ndoa

Hivi ni vitamu tamu vizuri zaidia kwa watu wazima na wanao lenga kula kitu chepesi kupata nguvu zaidi chumbani cha kulala.

Kuna aina tofauti za njugu na hasa kuna fulani iliyo na idadi kubwa ya L-arginine. Jukumu la amino acid hii ni kusaidia katika utoaji wa nitric oxide inayo saidia na mzunguko wa damu kwenye kibofu. Pia, zina omega-3 inayo saidia kupunguza kolesteroli mbaya mwilini na kuboresha mzunguko wa damu mwilini mwako.

2. Mboga za mchicha

kuboresha tendo la ndoa

Mchicha unasaidia kuongeza idadi ya L-arginine mwilini na kubadilishwa kuwa nitric oxide inayo saidia katika tendo la ndoa kwa wanaume. Hii ndiyo sababu kwa nini wanandoa wanashauriwa kuongeza mchicha kwenye lishe yao. Kuna njia nyingi za kuongeza mboga hii kwenye lishe yenu. Unaweza kaanga, kula kama saladi ama kusiagwa iwe smoothie.

3. Sharubati ya beetroot

Beetroot ni mboga inayo patikana kwenye mizizi. Ina saidia kuongeza stamina ya mwanamme na kumsaidia kudumu kwa wakati zaidi anapokuwa katika tendo la ndoa. Watafiti wamegundua kuwa mboga hii ina viwango vingi vya nitrates zinazo saidia kupunguza utumiaji wa hewa, na kwa sababu hii, mwanamme hachoki sana anapokuwa katika kitendo cha wanandoa.

Nitrates hizi zinapo fika mwilini, zina badilishwa na kuwa nitric oxide inayo saidia kutuliza mishipa ya damu na kuhimiza damu kuzunguka kwa urahisi mwilini hadi kwa kibofu. Hakikisha kuwa unakunywa sharubati hii angalau mara mbili kwa wiki.

4. Kitunguu saumu

Garlic

Huenda ukawa umesikia watu wanavyo onywa wasikule kitunguu saumu wanapo enda kuonana na wachumba wao. Lakini ukweli ni kuwa, kiungo hiki chenye harufu kali kina miujiza mingi. Kinasaidia kufanya damu iwe nyembamba na kuepusha shinikizo la juu la damu, kolesteroli nyingi na maradhi ya moyo.

Damu inapokuwa nyembamba, inakuwa rahisi kuzunguka mwilini kwa urahisi na kufika kwenye sehemu za kiume. Ili kufaidi zaidi kutokana na kiungo hiki, wanandoa wanapaswa kuhakikisha kuwa wanapika kwa kutumia kitunguu saumu pamoja na kitunguu maji wanapo tayarisha vyakula vyao.

5. Tikiti maji

food to last longer in bed

Tunda hili linasifika sio kwa utamu wake tu, mbali pia kwa umuhimu wake katika tendo la wanandoa. Viwango vya nitric oxide katika tunda hili vinasaidia kutuliza mishipa ya damu. Inafanya kazi sawa na viagra. Kwa wanaume wanao tatizika kitandani, tunda hili litawasaidia kutatua tatizo hilo.

Soma Pia: Makosa 5 Ya Kingono Ambayo Wanaume Hufanya!

Written by

Risper Nyakio