Vyakula Visivyo Kubalika Kwa Mama Mjamzito

Vyakula Visivyo Kubalika Kwa Mama Mjamzito

Mtoto anaye zaliwa kwa mama aliye kuwa akitumia vileo akiwa na mimba, huenda akawa na uzani wa chini, matatizo ya kiafya.

Mama mjamzito anastahili kuwa makini na mlo sahihi wenye afya bora ili kuhakikisha kuwa anajifungua mtoto mwenye afya. Tazama orodha yetu ya vyakula vya kuepuka katika mimba.

Mama mjamzito anapaswa kujiepusha na vyakula hivi

vyakula vya kuepuka katika mimba

Nyama mbichi

Mama mjamzito ana onywa dhidi ya kula nyama mbichi ama ambayo haija iva vizuri. Nyama huenda ikawa na bakteria wengi wanao weza kusababisha magonjwa sugu na kumwathiri mtoto anaye kua tumboni. Ni vyema kuhakikisha kuwa nyama imepikwa ikaiva vizuri.

Mayai ambayo haijaiva

Chakula kingine ambacho mama mjamzito anapaswa kujitenga nacho ni mayai ambayo hayaja pikwa. Ni vyema kujitenga na vyakula na bidhaa za vyakula zilizo tengenezwa na mayai mbichi kama vile mayonnaise na ice krimu.

Samaki walio na mercury

sahani ya mlo ya mama mjamzito

Samaki ni chanzo kizuri cha omega-3, ila sio samaki wote walio na manufaa chanya kwa mwili. Mama mjamzito ana stahili kujitenga na ulaji wa samaki wenye idadi kubwa ya mercury kama vile papa ama dagaa kwani wana athiri mtoto aliye tumboni na huenda akakua akiwa na matitizo ya kiafya.

Maziwa mbichi

Maziwa mbichi huenda ikawa na bakteria inayo fahamika kama listeria na inayo sababisha maradhi ya listeria katika ujauzito. Maradhi haya yana athari hasi kwa afya ya mama na mtoto. Maziwa ya mama mjamzito yanapaswa kuchemshwa vyema kabla ya kuyanywa.

Maini

Nyama ya maini ni chanzo kikubwa cha madini ya chuma na vitamini A. Ila wakati ambapo viwango hivi vinapo zidi, mtoto huenda akaathiriwa pakubwa.

Vileo

Pombe imehusishwa na kuwa na athari hasi katika ukuaji wa mtoto tumboni mwa mama. Mtoto anaye zaliwa kwa mama aliye kuwa akitumia vileo akiwa na mimba, huenda akawa na uzani wa chini, matatizo ya kiafya na kiakili ama kuchukua muda kukua. Mbali na hayo, mtoto huyo huenda akazaliwa kabla ya wakati kufika. Watoto wanao zaliwa kabla ya kukomaa vyema huwa na matatizo ya kupumua.

Hitimisho:vyakula vya kuepuka katika mimba

Lishe na siha ni muhimu sana kwa mama mwenye mimba. Lishe bora ina himiza ukuaji unaofaa wa mtoto akiwa tumboni na hata baada ya kuzaliwa. Mbali na hayo, mama anapaswa kuhakikisha kuwa anapunguza utumiaji wa kafeini kwani viwango vingi huenda vika changia katika kuharibika kwa mimba.

Soma PiaJinsi Ya Kuboresha Lishe Na Siha Kwa Mama Mjamzito

Written by

Risper Nyakio