Virutubisho vya chuma ni muhimu kwa mama mjamzito ili kuwa na seli za damu nyekundu zenye afya kwa mama na mtoto. Lishe ya mama inapaswa kuwa na vyakula vya kuongeza damu kwa mjamzito. Seli za damu nyekundu zina jukumu la kusafirisha oxygeni kwenye viungo vya mwili na kwa mtoto. Kiwango cha damu mwilini huongezeka kwa asilimia 50 mwanamke anapokuwa na mimba.
Iwapo mwanamke hatakuwa na damu tosha, hutatizika kutokana na anemia katika mimba. Inayomfanya mama kukosa nguvu tosha na kuhisi uchovu wakati wote.
Wanawake wajawazito wanahitaji miligramu 18 za chuma kwa siku. Lishe bora huwa chanzo bora cha vitamini, madini na virutubisho muhimu katika ukuaji wa mama na mtoto.
Vyakula vya Kuongeza Damu kwa Mjamzito
Matunda

- Strawberries
- Tikiti maji
- Prunes
- Raisins
Mboga

- Mchicha
- Sukuma wiki
- Broccoli
- Nyanya
- Viazi vitamu
- Collards
Nyama na mayai

- Nyama ya ng'ombe
- Maini
- Nyama ya nguruwe
- Mayai
- Kuku
- Oysters
- Shrimps zilizopikwa vizuri
Wanga

- Mikate
- Oats
- Wali
- Ugali
- Viazi vitamu vya kuoka
Mbali na kula vyakula vyenye chuma, ni muhimu kula vyakula vinavyosaidia kutumia chuma mwilini. Vyakula vyenye vitamini C huwa bora zaidi. Baadhi ya vyakula hivi ni kama:
- Machungwa
- Viazi
- Brussels sprouts
- Matunda ya kiwi
- Broccoli
- Cauliflower
Manufaa ya chuma kwa mama mjamzito na fetusi
- Kumpa mama nguvu na nishati
- Kusaidia katika ukuaji wa ubongo wa fetusi
- Ukuaji wa seli za damu za mtoto
- Kulinda dhidi ya kupata anemia katika mimba
Mara nyingi, huenda lishe ya mama ikakosa kumpa viwango hitajika vya chuma kufuatia mahitaji yaliyozidi. Kwa sababu hii, wajawazito wanahitajika kuchukua tembe za virutubisho vya kuongeza ama supplements kufikisha viwango hitajika.
Vyakula hasa vya baharini kama shrimps vinapaswa kupikwa hadi viiwe kabisa. Pia kuangazia ulaji wa vyakula vya baharini visivyokuwa na viwango vya juu vya zebaki. Matunda na mboga zinapaswa kusafishwa vyema ili kupunguza hatari ya mama kupata maambukizi yanayotokana na uchafu kwenye vyakula.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Vidokezo 7 Vya Kuwa na Mimba Salama na Yenye Afya