Vyakula 7 Bora Vya Kuongeza Hamu Ya Kufanya Mapenzi

Vyakula 7 Bora Vya Kuongeza Hamu Ya Kufanya Mapenzi

Sayansi imedhihirisha kuwa ngono ni nzuri kwako! Ina faida za kukata uzito na kuimarisha hisia zako. Cha muhimu zaidi ni furaha unayo hisi na kutosheleka baada ya kitendo hiki. Iwapo huwa unatatizika kupata hamu, kuna vyakula vya kuongeza hamu ya ngono na vitakusaidia katika vitendo vyako vya chumbani cha kulala.

Nini kikuu kuhusu hamu ndogo ya ngono?

Hata kama ngono ina faida nyingi, watu wengi hutatizika kuwa na hisia za ngono. Hamu ya chini ya ngono, ndivyo hali hii inavyo tambulika kama, huenda ikawa ni kufuatia uchovu, fikira nyingi na baadhi ya matibabu. Sio lazima uishi maisha ya kulazimishwa kuishi bila ngono.

Vyakula vya kuongeza hamu ya ngono: Jinsi lishe yako ina athiri kufanya mapenzi

Watafiti wamethihirisha kuwa, kuongeza vyakula fulani kwenye lishe yako kuna ongeza hamu yako ya ngono. Nyingi kati ya vyakula hivi huwa na virutubisho vinavyo himiza utoaji wa homoni na mzunguko wa damu kwa viungo vya hamu mwilini. Ili kupunguza taabu ya kujua vyakula hivi ni vipi, tumefanya utafiti mkuu na kuorodhesha vyakula vinavyo boresha hamu ya ngono unapo vikula mara kwa mara.

 

1. Matawi ya yai la shambani (Garden Egg Leaves)

Ni rahisi kwa ulimi wako, mboga hizi za kijani zina pikwa na salads, supu ama hata smoothies. Ni vyakula vya kiasili vinavyo ongeza hamu yako ya kula. Vina wingi wa vitamini A na C. Rangi ya kijani iliyoo kwenye majani yake inasaidia kusafisha na kuboresha mzunguko wa damu kwa viungo vinavyo husika na utendaji wa ngono. Sio mboga nyingi zina uwezo huu.

2. Karafuu (Cloves)

Karafuu zilizo pikwa ama mbichi ama za kusiagwa ni vyakula vyema. Unaweza viongeza kwa chakula chochote kile. Hakuna hatari kuziweka kwa wali ama hata supu yako unapo itayarisha.

Weka viwango vikubwa kwenye vinywaji na vyakula vyako. Kula na mwenzio ama mchumba wako pia. Ngono ni bora zaidi wakati ambapo nyote wawili mna hamu.

Karafuu zimetumika kama dawa ya matatizo ya kutopata watoto ama changamoto za kufanya mapenzi. Somo lingine lime thibitisha kuwa kuna uhusiano kati ya kula cloves na kuongezeka kwa hamu ya ngono katika wanyama ambao hujifungua. Ili kuboresha hamu yako ya ngono, ongeza kiungo hiki kwenye orodha ya vyakula vya kuongeza hamu ya ngono.

vyakula vya kuongeza hamu ya ngono

3. Tende, njugu za chui na walnuts (Dates, Tiger nuts, walnuts)

Vyote hivi vina ladha. Vinakusaidia kuwa na uzito mdogo wa mwili na pia kuboresha hamu yako ya utendaji wa ngono. Ni maarufu sana katika sehemu tofauti za Africa hasa upande wa kaskazini mwa Nigeria. Tende na njugu za chui zinaweza siagwa pamoja kutengeneza sharubati tamu.
Kinywaji hiki kinajulikana sana kama fura de nunu kina wingi wa amino acids, sukari ya matunda na mafuta ya omega 3. Zote zina saidia katika kuwa na hamu ya juu ya kufanya mapenzi na mzunguko wa damu mwilini. Hakikisha kuwa mnafurahia kinywaji hiki na mchumba wako.

4. Kombe/ Chaza (Oysters)

Hizi ni mojawapo ya vyakula vinavyo julikana zaidi kwa kuongeza hamu ya ngono. Hakuna aliye na uhakika kwa nini vina uwezo mkuu wa kufanya hivi. Wataalum wengi wa ngono wana shangazwa na jambo hili.

Zina wingi wa zinc, madini na amino acids. Pia vitamini B iliyo muhimu sana katika mzunguko wa damu kwenye viungo vinavyo husika katika utendaji wa mapenzi.

Ongeza chaza kwenye supu zako na mboga ili uwe na chakula chenye ladha.

5. Tikiti

Tikiti na rangi yake nyekundu ya kupendeza na maji mengi ni tunda mwafaka la kuongeza hamu yako ya ngono. Tunda hili lina wingi wa vitamini na ni bora kwa afya yako.

Somo moja katika Kituoc Cha Uboreshaji wa Mboga cha Texas A & M kiligundua kuwa tikiti ina sifa za viaggra hasa katika kuboresha hamu ya utendaji wa ngono. Tunda hili lina lycopene na citrulline inayo ongeza viwango vya nitric oxide mwilini. Na kufanya uwe na viwango vya juu vya kufanya ngono

6. Tangawizi

Tangawizi ina sifa katika kila pande ya matibabu- hasa katika kukata uzito wa mwili na kuthibiti shinikizo la damu na kutibu homa. Walakini, haija julikana sana kwa kuboresha hamu ya ngono. Kwa karne nyingi, tangawizi imetumika kutibu matatizo ya ngono na changamoto zingine zinazo husika na ngono.

Wava tangawizi mbichi kwenye chai ama sharubati yako ya matunda. Pia, unaweza itumia kuongeza ladha kwa supu zako na nyama.

7. Chokleti nyeusi

Chokleti ina phenylethylamine ambayo inaongeza viwango vya serotonin na endorphin. Kwa hivyo ikiwa unataka hamu yako ya ngono kuongezeka, nunua saduku la chokleti.

Ni vyema kula vyakula vinavyo ongeza hamu ya ngono, ila ni muhimu pia kuepuka vyakula vinavyo punguza hamu ya ngono. Vileo vingi, kahwa na baadhi ya matibabu huenda vikaathiri hamu yako ya ngono. Hakikisha kuwa unakula vyakula vitaavyo ongeza hamu yako ya utendaji ngono mara kwa mara.

Kumbukumbu: US National Library of Medicine National Institutes of Health

WebMD

Soma pia: My husband ignores me sexually, what should I do?

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Julie Adeboye kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio