Vyakula 5 Vinavyo Boresha Kuongezeka Kwa Maziwa Ya Mama

Vyakula 5 Vinavyo Boresha Kuongezeka Kwa Maziwa Ya Mama

Katika hatua hii, huenda ikawa usha gundua kuwa bila shaka, kunyonyesha mtoto mchanga ni kazi ngumu. Tofauti na inavyo onekana wakati unapo waona wazazi wengine waki walisha watoto wao. Mwili wako una hitaji chakula chenye afya na cha kutosha ili kuhakikisha kuwa una maziwa tosha ya kumlisha mwanao. Mojawapo ya vitu vikuu ambavyo ungependa kujua zaidi ni kuhusu vyakula vya kuongeza maziwa ya mama.

Una jiuliza kama vyakula unavyo kula vina saidia ama la. Na huenda ukawa hauna mama aliye pitia hapo wa kukueleza unayo hitajika kufanya. Usiwe na shaka, kwani katika makala haya, tuna kuelimisha zaidi kuhusu vyakula bora ambavyo kila mama anaye nyonyesha anapaswa kuhakikisha kuwa anakula. Ili kuhakikisha kuwa ana kichocheo tosha cha maziwa cha kumlisha mtoto wake.

Orodha Ya Vyakula Vya Kuongeza Maziwa Ya Mama

vyakula vya kuongeza maziwa ya mama

  1. Smoothie ya malenge

Njia rahisi ya kutengeneza ni kwa kuweka kipande cha malenge yaliyo pikwa ama kuchemshwa kwenye kifaa cha kutengenezea sharubati. Kisha uongeze maziwa kidogo na maji moto. Inasaidia sana katika kuboresha utoaji wa maziwa ya mama. Ina wingi wa vitamini A, D, kalisi na B12.

2. Muffins za blueberry za mama anaye nyonyesha

Ni rahisi kutengeneza na zina viungo vyenye afya kama mbegu za flax, mayai na blueberries. Zina kiwango kidogo cha sukari.

3. Chai ya herbal ya mama anaye nyonyesha

Kuhakikisha kuwa mwili wako una maji tosha unapo kuwa una nyonyesha ni muhimu sana. Hasa kwa sababu maji hayo yana tumika kutengeneza maziwa ya mtoto. Chai ya herbal iliyo na galactogen itamsaidia mama kuboresha utoaji wa maziwa.

vyakula vya kuongeza maziwa ya mama

4. Oats

Oats zime sifika kwa kuwa chakula kikuu, chenye afya na wingi wa fiber. Tengeneza oats kabla ya kulala kisha kuongeza matunda unayo yapenda ama mbegu za chia.

5. Supu iliyo pikwa kwa muda mrefu

Faida za kunywa supu iliyo pikwa kwa muda mrefu ni kuwa, ina virutubisho vingi. Ina amino acids, collagen na madini. Hizi sio muhimu kwa utoaji wa maziwa tu, mbali katika uponaji wa mwili wako baada ya kujifungua.

Kunyonyesha mtoto ni muhimu sana kwa mama na mtoto. Kupitia kwa maziwa ya mama, mtoto anapata kinga dhidi ya maradhi na virutubisho vinavyo msaidia kukua. Pia, yanamsaidia kumkinga dhidi ya kupata homa, kikohozi na maambukizi mengineyo. Kwa hivyo, hakikisha kuwa unamlisha mtoto maziwa ya mama pekee kwa muda wa miezi sita ya kwanza ya maisha yake.

Chanzo: WebMD

Soma Pia: Faida Za Kisaikolojia Za Kunyonyesha Kwa Mama

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio