Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Umuhimu Wa Chakula Bora Katika Ukuaji Wa Mtoto Na Kuongeza Uzani Wa Mwili

3 min read
Umuhimu Wa Chakula Bora Katika Ukuaji Wa Mtoto Na Kuongeza Uzani Wa MwiliUmuhimu Wa Chakula Bora Katika Ukuaji Wa Mtoto Na Kuongeza Uzani Wa Mwili

Matunda pia ni chakula kinachohitajika sana katika mwili wa mtoto, kwani yanampa mtoto nishati na virutibisho vinavyofaa katika lishe yake.

Kuna chakula aina nyingi sana ambazo zinaweza kuongeza uzito wa mtoto, lakini swali ni, je ni chakula kipi ambacho kina manufaa kwa mtoto wako? Kuna aina ya vyakula vya kuongeza uzito kwa mtoto vilivyo muhimu sana kwa ukauji wake.

Vyakula Muhimu Katika Ukuaji Wa Mtoto

vyakula vya kuongeza uzito kwa mtoto

Wazazi wengi watakufanya chochote wanachoweza ili kusaidia watoto wao wanapoanza kula.Lakini hawana orodha ya chakula kinachowafaa watoto hawa. Mtoto anapoanza kupoteza kilo, wewe kama mzazi utaanza kupata usingizi wa mang’amu mang’amu.

Kuna sababu nyingi sana ambazo zinaweza sababisha mtoto kukosa kukua kama watoto wa wengine, suluhisho ni kumpa chakula chenye kiwango cha juu cha kalori (50-55). Kiwango hiki kinafaa kupatiwa watoto kwa muda wa miezi sita ya kwanza, kisha baadae unampa kalori 45.Ukigundua kwamba mtoto wako anapoteza kilo jambo la kwanza ni kumuona daktari, kwa sabau jambo hili inaweza kusababishwa na mambo mengi.

Wazo kwamba maziwa ya mama ndio chakula bora kwa mtoto limerudiwa miaka nenda miaka rudi. Hii ni kwa sababu maziwa ya mama humsaidia mtoto kukua kwa haraka. Lakini unapata kuwa kuna wanawake kadhaa ambao hawawezi kumnyonyesha mtoto kwa sababu nyingi tofauti tofauti. Kwa watoto waliozidi miezi 6 maziwa ya mifugo inaweza kutumika lakini kwa walio chini ya umri huo maziwa ya fomula inafaa.

  • Protini

Protini zinasaidia sana katika ukuaji wa watoto,zinaongeza misuli. Chakula kama samaki huwa na kiwango cha juu cha Omega-3, ambayo pia inasaidia katika ukuaji wa akili na maendeleo ya mtoto.

Maharagwe pia ni chakula muhimu sana katika kiwango hiki ambayo ina virutubisho na madini ambazo ni muhimu sana katika ukuaji wa mtoto. Mayai pia inaweza kuwekwa katika kategoria hii. Ni vyema kumpa mtoto yai moja baada ya siku moja ili kuweza kuongeza uzito wake.

  • Vitamini

Matunda pia ni chakula kinachohitajika sana katika mwili wa mtoto, kwani yanampa mtoto nishati na virutibisho vinavyofaa katika lishe yake. Matunda haya ni kama vile mandizi na parachichi. Yanaweza kutumiwa kutengeneza sharubati, ili iwe rahisi kwa mtoto kumeza.

Ni vyema kuongeza njugu katika chakula cha mtoto wako. Kwa sababu njugu zinaweza leta shida ya kutafunika unaweza siaga na kutengeza siagi au pia unaweza ongeza kwenye smoothie ya mtoto wako. Lazima pia uwe makini ili usimpe kiwango kikubwa kwani kuna njugu ambazo zina ufuta. Njugu zinazoweza kutumika ni kama vile mlozi.

vyakula vya kuongeza uzito kwa mtoto

Mtoto anaweza kupatiwa oats, kwa kuwa chakula hiki kina madini na faiba zinazohitajika. Chakula hiki kinaweza tayarishwa kwa kuchanganya na maziwa na matunda kama vile mandizi. Ukikitengeneza hivi kiwango cha kalori kitakuwa kimeenda juu.Kinahimizwa sana kwa kuwa watoto hawana shida ya kukitafuna na kukisiaga. Chakula hiki kina magnesium, thiamine manganese na phosphorus ambazo zinachangia pakubwa katika kuongeza uzito wa mtoto.

  • Wanga

Vyakula vya wanga kama vile mchele ni muhimu pia. Vyakula hivi vina kiwango cha juu cha sukari. Ni vyema kubadilishia mtoto wako chakula baada ya muda. Leo akila oats kesho mpe wali na matunda.

Mtoto anaweza pia kupatiwa maziwa ya bururu kwani haina ugumu wa kutafunwa au kumezwa. Chakula hiki kina manufaa mengi katika mwili wa mtoto kama vile kupigana na virusi  bali na hayo kiwango cha kalori pia kiko juu.

Jambo la muhimu ni kuangalia sana ni kuzingazia chakula zilizo na virutubisho vitakavyomsaidia mtoto wako. Lishe bora ndio lengo la maana sana unampo mchagulia mtoto chakula cha kumpa. Je, una madokezo zaidi kuhusu vyakula vya kuongeza uzito kwa mtoto? Tujulishe kwa kuwacha ujumbe mfupi.

Chanzo: Healthline

Soma Pia: Jinsi Ya Kudumisha Afya Bora Katika Mimba

Got a parenting concern? Read articles or ask away and get instant answers on our app. Download theAsianparent Community on iOS or Android now!

img
Written by

Risper Nyakio

  • Home
  • /
  • Development
  • /
  • Umuhimu Wa Chakula Bora Katika Ukuaji Wa Mtoto Na Kuongeza Uzani Wa Mwili
Share:
  • Ukuaji Wa Mtoto Wa Miezi Sita Na Kinacho Tendeka Katika Hatua Hii

    Ukuaji Wa Mtoto Wa Miezi Sita Na Kinacho Tendeka Katika Hatua Hii

  • Hatua Katika Ukuaji Wa Mtoto Wa Miezi Minne

    Hatua Katika Ukuaji Wa Mtoto Wa Miezi Minne

  • Hatua Katika Maendeleo Na Ukuaji Wa Mtoto Wako Wa Miezi Tano

    Hatua Katika Maendeleo Na Ukuaji Wa Mtoto Wako Wa Miezi Tano

  • Ukuaji Wa Mtoto Wa Miezi Sita Na Kinacho Tendeka Katika Hatua Hii

    Ukuaji Wa Mtoto Wa Miezi Sita Na Kinacho Tendeka Katika Hatua Hii

  • Hatua Katika Ukuaji Wa Mtoto Wa Miezi Minne

    Hatua Katika Ukuaji Wa Mtoto Wa Miezi Minne

  • Hatua Katika Maendeleo Na Ukuaji Wa Mtoto Wako Wa Miezi Tano

    Hatua Katika Maendeleo Na Ukuaji Wa Mtoto Wako Wa Miezi Tano

Get advice on your pregnancy and growing baby. Sign up for our newsletter
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • More
    • TAP Community
    • Advertise With Us
    • Contact Us
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2023 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
About Us|Team|Privacy Policy|Terms of Use |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it