Vyakula Vyenye Virutubisho Vya Kusaidia Watoto Kuongeza Uzito

Vyakula Vyenye Virutubisho Vya Kusaidia Watoto Kuongeza Uzito

Ni vyakula gani bora vya kuongeza watoto uzito? Tume orodhesha vyakula bora vyenye afya na virutubisho ambavyo unaweza chagua kutoka.

Kwa asili, watoto huwa na nafasi za kuongeza uzito wanavyo zidi kukua. Baadhi ya wakati lakini, watoto huenda wakawa wadogo ama wakonde kufuatia jeni zao. Hata kama uzito na wanavyo onekana havionyeshi afya yao, watoto pia wana mahitaji yao ya uzito. Mahitaji haya yana ongozwa na masharti na mahitaji ya BMI. Vyakula bora vya kuongeza watoto uzito ni vyakula vilivyo na virutubisho vingi.

Ikiwa wewe ni mzazi wa mtoto aliye na uzito mdogo, bila shaka hauna hamu ya kumlisha chakula kilicho na viwango vya juu vya kalori ili kumfanya aongeze uzito. Lakini kula chakula chenye afya ni muhimu zaidi. Unacho hitaji kufanya ni kuhakikisha kuwa mtoto wako anapata virutubisho tosha kwenye lishe zake. Virutubisho ni muhimu zaidi kuliko kalori.

Lishe iliyo na virutubisho vingi itamsaidia mwanao kuongeza uzito. Na sio hilo tu, itamsaidia kumpa vitamini, madini na protini ili kuboresha ukuaji wake. Kutazama upande tofauti, kuwa na uzito mwingi huenda kukasababisha matatizo mengi ya kiafya katika umri mchanga. Ufuta ni muhimu kwenye lishe ya mtoto wako, lakini ni aina nzuri ya ufuta inayo saidia na ukuaji wa ubongo na homoni zake. Baadhi ya vyakula bora vya kuongeza watoto uzito vina orodheshwa hapa chini:

Tazama Vyakula Hivi Vyenye Virutubisho Vya Kuongeza Watoto Uzito

Vyakula vyenye wingi wa protini

Vyakula Vyenye Virutubisho Vya Kusaidia Watoto Kuongeza Uzito

 

Protini zinawasaidia watoto kukua. Zina saidia watoto kukuza misuli. Samaki ni chanzo bora cha protini kwa sababu zina wingi wa Omega-3. Omega-3 ina saidia katika kila nyanja ya ukuaji wa mtoto wako na maendeleo yake. Maharagwe na vyakula vya familia hii vina wingi wa vitamini na madini. Mayai ni chanzo kingine kikubwa cha protini. Jaribu kumpa mwanao yai moja baada ya siku moja iwapo unaweza.

Vyakula vyenye maziwa

Vyakula Vyenye Virutubisho Vya Kusaidia Watoto Kuongeza Uzito

 

Vyakula kama maziwa na cheese zina viwango vingi vya kalisi, kitu ambacho mtoto wako anahitaji kupata mifupa yenye nguvu. Pia, watoto wengi wanapenda vyakula hivi. Maziwa ni nzuri kwa watoto walio na uzito wa chini kwa sababu yana wingi wa ufuta na kalisi. Ufuta ulioko kwenye maziwa utawasaidia kuongeza uzito.

Matunda ya nishati

best foods to help kids gain weight

 

Matunda kama vile mandizi na parachichi yana virutubisho muhimu vya nishati na pia viwango vya juu vya kalori. Na sio hayo tu, ni bora ya kujitibu. Watoto wanapenda kula matunda kwa njia yoyote ile kwa sababu yana sukari. Itakuwa rahisi kumlisha mtoto wako ukiyatengeneza yawe smoothie ama dessert. Kama vile mandizi na parachichi.

Oats

vyakula vya kuongeza watoto uzito, oats

 

Oats zina wingi wa fiber, vitamini na madini. Ukiongeza oats kwa maziwa na matunda kidogo, haijalishi ikiwa ime kauka ama freshi, utakuwa umemtengenezea mtoto wako lishe yenye virutubisho. Oats zina wingi wa magnesium, thiamine, phosphorous na manganese. Pia zina viwango vidogo vya kolestroli na ufuta, Na mtoto mwenye umri mdogo, unaweza zisiaga ama ununue oats zilizo siagwa.

Vyakula vya wanga

Vyakula Vyenye Virutubisho Vya Kusaidia Watoto Kuongeza Uzito

 

Wanga zilizo chakatwa kama vile mchele mweupe zina sababisha kuwa na viwango vya juu vya sukari mwilini, kwa hivyo badala ya kumjazia mtoto wako wali nyingi kwenye sahani yake, chagua vyakula vyenye virutubisho zaidi. Nafaka huwa na viwango vya juu vya fiber na manufaa mengi ya kiafya, ila ni vigumu sana kwa watoto wachanga kuvichakata mwilini. Huenda vikawa fanya washibe haraka. Chagua viazi, malenge na mboga za mizizi.

Maziwa ya bururu

Vyakula Vyenye Virutubisho Vya Kusaidia Watoto Kuongeza Uzito

 

Kwa sababu maziwa ya bururu (yoghurt) ni rahisi kula na pia ina manufaa ya kiafya kwenye utumbo, inawafaa watoto wachanga. Walakini, kaa mbali na hiari zenye sukari nyingi ya kuchakatwa, chagua maziwa ya bururu yasiyo na ladha za kuongezea.

Njugu na Mbegu

vyakula vya kuongeza watoto uzito

 

Iwapo mtoto wako anapenda vitamu tamu vya kutafuna, huenda wakapenda njugu, almonds na aina yoyote ile ya njugu zenye afya. Hakikisha kuwa njugu unazo walisha hazina viwango vingi vya ufuta. Ufuta wa aina ya mono- na polyunsaturated husaidia na kolestroli. Iwapo mtoto wako angali mchanga, hakikisha kusiaga njugu ziwe smoothie ama utengeneze siagi ya njugu.

Mara nyingi, kumsaidia mtoto wako kuongeza uzito ni jambo la kuongeza kalori kwenye lishe yake, na kuwa makini kwa virutubisho. Ni muhimu kukumbuka kuwa hitaji hili halimaanishi kuwa hawakuli vyema ama hawana afya. Wazazi wengi hujaza lishe ya watoto wao na vyakula vilivyo na sukari na mafuta mengi ili kuongeza uzito wa watoto wao. Kufanya hivi kutaharibu hamu yao ya kula vyakula vyenye ladha na virutubisho.

Chanzo: Klay Schools

Soma pia: Mbadala Bora Wa Maziwa Na Wenye Afya Kwa Watoto Wachanga

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio