Kuzingatia lishe bora na yenye afya ni muhimu katika kupunguza shinikizo la damu. Kulingana na utafiti, kuna vyakula vya kupunguza shinikizo la damu ambavyo vinasaidia vikiongezwa kwenye lishe.
Vyakula vya kupunguza shinikizo la damu
1.Ndizi

Ndizi huwa na kiwango kingi cha potassium ambayo ni muhimu katika kudhibiti hypertension. Kulingana na utafiti, potassium huyapunguza mvutano kwenye kuta za mishipa ya damu. Vyakula vingine vilivyo na viwango vingi vya potassium ni parachichi, nyanya, tuna, uyoga, viazi vitamu, halibut na maharagwe.
2. Chokleti nyeusi
Chokleti imedhibitishwa kusaidia katika kupunguza shinikizo la damu, hasa kwa watu walio na hypertension.
3. Mboga za kijani
Mboga za kijani zina wingi wa nitrates zinazosaidia kudhibiti shinikizo la damu. Baadhi ya mboga hizi ni kama vile kabichi, sukuma wiki, collard greens, fennel na mchicha.
4. Tikiti maji

Tikiti maji huwa na amino acid ya citrulline inayosaidia kudhibiti shinikizo la juu la damu. Citrulline inasaidia mwili kutoa gesi ya nitric oxide inayopumzisha mishipa ya damu na kuhimiza kunyumbulika kwa ateri. Kulingana na utafiti, watu wanaochukua tikiti maji nyingi wana mioyo yenye afya bora zaidi.
5. Oats
Oats huwa na fiber inayofahamika kama beta-glucan inayopunguza viwango vya kolesteroli kwenye damu na hivyo basi kupunguza shinikizo kwenye damu. Chukua oats kama kiamsha kinywa chako.
6. Maziwa ya bururu

Watafiti wamegundua kuwa maziwa ya bururu inasaidia kupunguza shinikizo la damu hasa katika wanawake. Wanawake wa miaka kati ya 18-30 walidhihirisha punguko la asilimia 20 la hatari ya hypertension ikilinganishwa na wanawake ambao hawakunywa maziwa ya bururu.
7. Cinnamon
Cinnamon inasaidia kupunguza shinikizo la damu kwa muda mfupi. Ongeza cinnamon kwa chakula chako kwa kunyunyizia ama kwenye matunda na maji yako badala ya sukari.
Jitenge na vyakula hivi
1. Kaffeini
Kaffeini iliyoko kwenye chai, kahawa na soda kama cola husababisha ongezeko la shinikizo ya damu. Kunywa vikombe viwili vya kaffeini kwa siku kunaweza ongeza shinikizo ya damu.
2. Chumvi
Chumvi ina sodium inayoongeza shinikizo la damu. Kuongeza kiwango kikubwa cha chumvi kwenye chakula kuna athari hasi.
3. Pombe
Kunywa viwango vidogo vya mvinyo kuna manufaa ya kiafya. Hata hivyo, viwango vingi vya pombe vina athiri shinikizo ya damu na pia kuongeza hatari ya moyo kutofanya kazi, saratani na kuongeza uzito mwingi wa mwili.
Soma Pia:Manufaa Ya Kula Kitunguu Saumu Kwa Afya Yako