Hata ingawa kiwango zaidi cha urefu wa mtoto wako dhibitiwa na geni zaidi ya kitu chochote, wasaidie watoto wako kukua warefu kwa kuwalisha vyakula hivi. Kulingana na AOL, wanaume sasa hivi ni warefu inchi 4.5 kuliko walivyo kuwa miaka 100 iliyopita. Lishe inachangia kiasi kikubwa kwa hili. Hapa kuna aina ya vyakula ambavyo vitasaidia na kurefuka kwa watoto kwa kiasili na kuwaongeza nguvu kama ilivyo orodheshwa na Style Craze.
Vyakula vyenye wingi wa kalisi vitasaidia kurefuka kwa watoto zaidi kiasili

Kulingana na WebMD, kalisi haisaidii na ukuaji wa mifupa tu, mbali inasaidia na mzunguko na utendaji kazi wa misuli. Wape watoto wako vyakula vilivyo na wingi wa kalisi kama vile maziwa, maziwa ya bururu na mchicha.
Vyakula vilivyo na wingi wa protini
Protini zina jukumu la kujenga mwili. Ni kati ya vitu vinavyo hitajika zaidi kuweka mwili ukiwa na nguvu. Sio kumaanisha kuwa unapaswa kuwapatia watoto wako protini zaidi kwa matumaini kuwa watakuwa na urefu sawa na wachezaji wa mpira wa vikapu, kwa sababu, ikiwa haiko kwenye geni zako, haiwezekani.
Pia ng'amua kuwa haupaswi kumlisha mtoto wako protini nyingi sana, kwa sababu inaweza sababisha aina tofauti ya matatizo ya kimwili. Kusawasisha ni muhimu sana.
Vyakula vyenye wingi wa protini ni kama vile mayai, maziwa, oatmeal, nyama laini na soybeans.
Lishe bora

Binadamu hawezi ishi kwa kula protini na kalisi peke yake. Kula idadi kubwa ya virutubisho hivi vinaweza kufanya uwe mgonjwa. Tafuta vyakula vilivyo na wingi wa vitamini na madini tofauti. Vyote vitafanya kazi kusaidia ukuaji wa mtoto wako. Kwa mfano, vitamini A inasaidia protini kutumika mwilini. Vitamini D inasaidia na utumikaji wa kalisi mwilini na kuwa na mifupa yenye nguvu. Vitamini zingine zinasaidia kulinda dhidi ya magonjwa na kuusaidia mwili kuwa na nguvu tosha.
Hakikisha kuwa wakati wote unamlisha mtoto wako chakula kilicho na virutubisho vyote. Usiegemee sana kwa aina moja ya chakula. Na bila shaka utashuhudia ongezeko la urefu wake.
Soma pia: Maendeleo Na Ukuaji Wa Mtoto: Mtoto Wa Mwezi Mmoja