Homoni mwilini zinachangia pakubwa katika afya ya kijumla na katika utendaji kazi mwilini. Kwa wanawake, kutokuwa sawa kwa homoni mwilini huenda kukamfanya atatizike kupata mimba. Homoni ya estrogen mwilini huwa na jukumu kubwa na kutokuwa sawa kwake huathiri utendaji kazi mwilini. Hushuhudiwa mara nyingi mwanamke anapo vunja ungo, kipindi cha hedhi, anapokuwa na mimba na anapofikisha umri wa kutoshaliza ama menopause. Kuna baadhi ya vyakula vya kurekebisha homoni ambavyo mama anaweza kutumia kumsaidia kutunga mimba kwa urahisi.
Vyanzo vya kubadilika kwa viwango vya homoni mwilini

- Kuongezeka kwa umri
- Kula lishe hafifu
- Kutofanya mazoezi
- Kusombwa na mawazo
- Kutolala vya kutosha
- Sumu mwilini
- Mbinu za kupanga uzazi
Dalili za homoni kutokuwa sawa mwilini
- Mhemko wa hisia
- Kuchoka ovyo
- Kuongeza uzito kwa kasi
- Upele kwenye uso
- Kuumwa na kichwa mara kwa mara
- Uke kukauka na kukosa hamu ya tendo la ndoa
- Kutatizika kulala na kupata usingizi usiku
- Kukasirika ovyo bila sababu
Jinsi ya kurekebisha homoni mwilini
Kufanya mazoezi

Kufanya mazoezi mepesi kama vile kutembea kwa dakika 30 kwa siku ni muhimu kwa mwili. Mazoezi yanapunguza mawazo mengi na kuongeza uzalishaji wa homoni za kuhisi vizuri. Kujishughulisha kimazoezi kunasaidia kupunguza uzito wa mwili unaozifanya homoni mwilini kutokuwa sawa.
Omega-3

Mafuta ya omega-3 yana umuhimu mwingi katika kusawasisha homoni mwilini. Yana saidia katika kurekebisha mzunguko wa hedhi na kuondoa sumu zaidi mwilini. Vyanzo vya omega-3 ni kama samaki, maharagwe ya soya, mafuta ya zeituni, walnuts na mafuta ya nazi.
Vitamini D

Vitamini D inapatikana kwa samaki, mboga, matunda, mayai, maziwa na kuota jua. Ina umuhimu wa kuwezesha tezi ya pituitary kufanya kazi inavyo faa. Inasaidia kudhibiti uzito wa mwili na kiwango tosha cha estrogen mwilini. Kichocheo kinachohusika na uzalishaji wa yai kwenye ovari.
Mafuta ya nazi
Mafuta ya nazi, hasa yale asili yasiyo kuwa yamechakatwa. Yanaiwezesha thyroid ama koromeo kutenda kazi vyema. Kusaidia katika kusawazisha sukari kwenye damu na kuongeza kinga mwilini. Tumia mafuta ya nazi kwenye chakula chako unapokitayarisha.
Orodha ya vyakula vya kurekebisha homoni tulivyo viangazia vinamsaidia mama anayetatazika kushika mimba. Vina boresha utendaji kazi bora mwilini na kusawasisha viwango vya homoni mwilini.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Afya Ya Kizazi: Mbinu Za Kutoa Uchafu Kwenye Kizazi