Kuna mabadiliko mengi ambayo mama anapaswa kufanya anapo jitayarisha kuwa mama. Kuwa tayari kifedha, kihisia, kifizikia na pia kuhakikisha kuwa anachukua lishe bora. Lishe ni muhimu kwa afya yake na pia ina uwezo wa kuongeza nafasi zake za kutunga mimba. Tuna angazia vyakula vya kusaidia kupata mimba ambavyo mwanamke anapaswa kuchukua. Hivi ni vyakula vinavyo mwezesha mwanamke kutunga ujauzito kwa urahisi zaidi.
Vyakula vya kusaidia kutunga mimba
Vikundi hivi vya vyakula vina umuhimu ufuatao.
- Mboga za majani ya kijani na matunda

Umuhimu wake
- Kuongeza nafasi za kutunga ujauzito na kuongeza ubora wa mayai ya mwanamke. Ni vyema kuhakikisha kuwa sahani yako wakati wote ina mboga na matunda
- Matunda yana saidia kusafisha mwili na hasa mfumo wa uzazi. Mchakato huu ni muhimu sana mama anapo azimia kuwa na mtoto
- Matunda kama vile ndizi, tikiti maji na parachichi ni bora
- Mboga za kijani zina saidia kuongeza kingamwili
2. Protini

Kuna bidhaa nyingi za vyakula zinazo kuwa na wingi wa protini. Protini za wanyama na za mimea.
Mama anaye azimia kutunga mimba ana shauriwa kupunguza ulaji wa nyama nyekundu. Badala yake, ana shauriwa kula nyama laini ama nyeupe. Vyanzo vya protini huongeza zinki mwilini.
- Kula nyama kutoka kwa samaki hasa wa baharini. Samaki wa viwango vya juu vya omega-3. Muhimu katika kuboresha mfumo wa neva katika fetusi
- Samaki kama vile tuna, tilapia na samoni ama salmon kwa kimombo
- Kuku wa kienyeji, nyama ya nguruwe na mayai
- Mayai ni muhimu katika kukuza ubongo wa mtoto. Mama anashauriwa kula angalau yai moja kila siku
- Mayai hufanya uhisi shibe kwa muda mrefu na kupunguza hamu ya kula mara kwa mara. Jambo linalo sababisha mama kuongeza uzito mwingi
3. Maziwa na bidhaa za maziwa

Kunywa kikombe kimoja cha maziwa angalau kila siku ni muhimu sana kwa mama anaye taka kutunga mimba.
Maziwa pia ni chanzo kizuri cha protini. Bidhaa za maziwa kama vile maziwa ya bururu ni bora kwa afya ya mwanamke. Yana saidia kupigana dhidi ya maambukizi na kusafisha mfumo wa uzazi katika wanawake.
Ni muhimu kwa mama kuhakikisha kuwa anapo kula wanga, anakula wanga ulio meng'enywa. Kuchukua mkate wa hudhurungi badala ya mweupe. Na kutoa vyakula vyenye sukari nyingi kwa lishe yake. Hivi ni baadhi ya vyakula vya kusaidia kupata mimba ambavyo mama anaweza kuongeza kwenye lishe yake ili kuongeza nafasi ya kutunga mimba kwa kasi zaidi.
Chanzo: WebMD
Soma Pia:Jinsi Ambavyo Mwanamke Anaweza Kuongeza Nafasi Zake Za Kutunga Mimba