Miezi ya kwanza ya ujauzito huwa migumu sana kwa mama. Katika trimesta ya kwanza, huu ndiyo wakati ambapo hatari ya kupoteza mimba huwa juu. Mama anatatizika na ugonjwa wa asubuhi na kuhisi kichefuchefu. Mama anapaswa kuwa na maarifa ya vyakula vya mama mjamzito wa miezi 3 anazopaswa kuzingatia ili kudumisha afya yake na ya fetusi. Lishe ni muhimu katika safari yote ya mimba kwani inasaidia na ukuaji wa mtoto.
Vyakula Vya Mama Mjamzito wa Miezi 3

Wakati wote, lishe ya mama inapaswa kumpa virutubisho muhimu ili kuendeleza afya boramama anapaswa kula vyakula hivi kuhakikisha kuwa mtoto anayekua tumboni ana afya bora.
- Vyakula vyenye folate
Folic acid ama folate ni muhimu katika mimba kwani inasaidia na ukuaji wa akili ya mtoto na uti wa mgongo. Vyakula vyenye folate ni kama vile maharagwe, broccoli, parachichi, mchicha, sukuma wiki na okra. Kwa mama asiyeweza kufikisha viwango hitajika vya folate, anaweza kutumia tembe za folic acid.
2. Vyakula vyenye vitamini B6

Ugonjwa wa asubuhi huwa kileleni katika mwezi wa tatu wa mimba. Vitamini ya B6 husaidia kupunguza hisia za kichefuchefu na kutapika. Vitamini hii inaweza kupatikana kwenye vyakula kama vile, nyama laini, nyama za ndege wa nyumbani, parachichi, njugu, matunda ya citrus na maharagwe ya soy.
3. Mboga
Mama mjamzito anahitajika kula mboga angalau mara tatu kwa siku. Kuna anuwai ya hiari ambazo anaweza kuchagua kutoka kwake. Kama vile sukuma wiki, mchicha, kabeji na zinginezo.
4. Wanga
Wanga ni kirutubisho muhimu mwilini, na kinasaidia katika kuupa mwili nishati. Mwanamke mjamzito anashauriwa kula wanga nzima na kujitenga na zilizochakatwa kwani zina kemikali nyingi.
5. Protini

Protini zinasaidia katika ukuaji wa mwili pamoja na fetusi, kutengeneza tishu, misuli na DNA. Vyanzo bora vya protini ni kama vile njugu, kuku, nyama, soybeans na maharagwe.
6. Matunda freshi
Matunda yana virutubisho vingi muhimu kwa afya ya mtoto na mamake. Katika ujauzito, mama anahimizwa kula matunda freshi ikilinganishwa na yaliyohifadhiwa. Kama vile parachichi, tikiti maji, ndizi, machungwa, tufaha na strawberries.
7. Vitamini D

Muhimu katika ukuaji wa mfumo wa kinga, mifupa, meno, na kugawana kwa seli mwilini wa mtoto. Mifano ya vyakula vilivyo na vitamini ni kama samaki wa tuna, tilapia na salmon, nafaka, maziwa na mafuta ya cod liver.
8. Bidhaa za maziwa

Muhimu kwa ukuaji wa mifupa yenye nguvu na siha. Bidhaa za maziwa ni kama vile maziwa, maziwa ya bururu na cheese. Zina wingi wa kalisi.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Matibabu Asili Ya Fibroids Na Umuhimu Wa Lishe Bora