Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Vyakula Vya Mama Mwenye Mimba Ili Kupata Mtoto Mrembo

3masomo ya dakika
Vyakula Vya Mama Mwenye Mimba Ili Kupata Mtoto MremboVyakula Vya Mama Mwenye Mimba Ili Kupata Mtoto Mrembo

Orodha hii ya vyakula vya mama mwenye mimba vitakusaidia kujifungua mtoto mrembo na mwenye busara.

Lishe ni muhimu sana kwa mama aliye na mimba, sio kwa afya yake tu, mbali hata kwa maisha ya kiumbe kinacho kua tumboni mwake. Wakati huu ni muhimu sana kwa afya ya mtoto aliye tumboni mwake na afya yake baada ya kuzaliwa italingana na vyakula vya mama mwenye mimba ambavyo anakula na utunzaji ambao mama mwenye mimba anafuata. Ni muhimu kwa mama mwenye mimba kuanza kuchukua hatua za utunzaji wa mtoto mdogo punde tu anapo gundua kuwa ana mimba. Kuanza na kula vitamini ama kuanza darasa zake za utunzaji wa kabla ya kujifungua. Ni vyema kuanza safari hii ya ujauzito na daktari wako ili aweze kukushauri katika kila hatua.

Vyakula vya mama mwenye mimba

Maji

Hatuwezi sisitiza vya kutosha umuhimu wa kunywa maji tosha. Na si kwa mama aliye na mimba tu ila hata kwa watu wengine wote. Maji tosha ni muhimu sana mwilini na ina majukumu mengi. Pia yana saidia kuhakikisha kuwa hauna choo kigumu ama kupata maambukizi ya mfumo wa mkojo.

vyakula vya mama mwenye mimba

Mboga

Mboga hasa za kijani ni muhimu sana kwa mama mwenye mimba. Ni muhimu sana katika kuongeza damu mwilini. Baadhi ya mboga hizi ni kama vile za kunde, mchicha, managu, mrendaa na kadhalika. Una shauriwa kupunguza kiwango cha nyama na kuongeza kiwango cha mboga unacho kula.

Kukosa mboga tosha za kijani mwilini kunaweza sababisha ukosefu wa damu mwilini maarufu kama Anaemia.

Matunda

Matunda ni vyanzo vikuu vya vitamini ambazo ni muhimu sana mwilini wako na wa mtoto anaye kua tumboni mwako. Hakikisha kuwa chakula chako kina tunda. Matunda unayo shauriwa kula wakati huu ni kama vile mandizi, machungwa, limau, tufaha na parachichi. Matunda kama parachichi ni muhimu sana katika kupunguza mafuta zaidi mwilini. Pia linasaidia katika ukuaji wa akili/ubongo na misuli ya mtoto mdogo.

Vyakula Vya Mama Mwenye Mimba Ili Kupata Mtoto Mrembo

Mayai

Protini ni muhimu sana unapokuwa na mimba ili kusaidia mwili wako katika kuzuia kupata maradhi tofauti na kukua kwa mwili. Mayai ni muhimu sana katika jukumu hili. Hakikisha kuwa unakula angalau mayai matatu kila wiki. Epuka kula mayai zaidi kwani huenda yakaanzisha changamoto tofauti mwilini.

Maziwa

Maziwa ni chanzo kikubwa cha protini, kalisi na vitamini ikiwemo virutubisho na madini mengineyo. Glasi moja ya maziwa kila siku ni muhimu sana kwa afya ya mtoto aliye tumboni mwako. Ili kukua mifupa na misuli yenye nguvu na pia katika mzunguko wa damu mwilini. Ila kwa watu ambao wana mzio wa maziwa na bidhaa za maziwa, ni vyema kuwasiliana na daktari wako.

Nafaka

Mimea kama mahindi, mtama na ngano ni mojawapo ya nafaka zinazo julikana na zilizo muhimu sana. Zina faida anuwai kwa mwili wa mama na wa mtoto na kuupa mwili nguvu za kufanya kazi.

vyakula vya mama mwenye mimba

Protini

Bidhaa kama vile za samaki, ama samaki mwenyewe, nyama laini ni muhimu unapokuwa na mimba. Ila kwa nyama nyekundu, hakikisha kuwa umepunguza kiwango chako.

Kuilinda afya yako ni muhimu sana unapo kuwa na mimba. Iwapo ungependa kujifungua mtoto mrembo na mwenye busara, orodha yetu ya vyakula vya mama mjamzito itakusaidia kujua aina ya vyakula ambavyo ni muhimu sana katika wakati huu. Ni matumaini yetu kuwa utakuwa na safari njema na ya kupendeza ya ujauzito.

Kumbukumbu: Webmd, Tuko.co.ke

Soma pia: Pregnancy Concerns: Being Pregnant Over 35 Years

img
Yaliandikwa na

Risper Nyakio

  • Nyumbani
  • /
  • Pregnancy
  • /
  • Vyakula Vya Mama Mwenye Mimba Ili Kupata Mtoto Mrembo
Gawa:
  • Lishe Ya Mama Mwenye Mimba: Ratiba Ya Lishe Ya Mama Mwenye Mimba

    Lishe Ya Mama Mwenye Mimba: Ratiba Ya Lishe Ya Mama Mwenye Mimba

  • Tazama Mavazi Haya Ya Anakara Ya Mama Mwenye Mimba

    Tazama Mavazi Haya Ya Anakara Ya Mama Mwenye Mimba

  • Vidokezo Vya Jinsi Ya Kupata Mtoto Mrembo Na Mwenye Busara

    Vidokezo Vya Jinsi Ya Kupata Mtoto Mrembo Na Mwenye Busara

  • Mavazi Ya Kupendeza Ya Mama Mwenye Mimba

    Mavazi Ya Kupendeza Ya Mama Mwenye Mimba

  • Lishe Ya Mama Mwenye Mimba: Ratiba Ya Lishe Ya Mama Mwenye Mimba

    Lishe Ya Mama Mwenye Mimba: Ratiba Ya Lishe Ya Mama Mwenye Mimba

  • Tazama Mavazi Haya Ya Anakara Ya Mama Mwenye Mimba

    Tazama Mavazi Haya Ya Anakara Ya Mama Mwenye Mimba

  • Vidokezo Vya Jinsi Ya Kupata Mtoto Mrembo Na Mwenye Busara

    Vidokezo Vya Jinsi Ya Kupata Mtoto Mrembo Na Mwenye Busara

  • Mavazi Ya Kupendeza Ya Mama Mwenye Mimba

    Mavazi Ya Kupendeza Ya Mama Mwenye Mimba

Pata ushauri wa mara kwa mara kuhusu ujauzito wako na mtoto wako anayekua!
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • Zaidi
    • TAP Jamii
    • Tangaza Nasi
    • Wasiliana Nasi
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2022 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
Kutuhusu|Timu|Sera ya Faragha|Masharti ya kutumia |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it