Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Umuhimu Wa Lishe Bora Mapema Katika Mimba Ni Upi?

3 min read
Umuhimu Wa Lishe Bora Mapema Katika Mimba Ni Upi?Umuhimu Wa Lishe Bora Mapema Katika Mimba Ni Upi?

Mayai husaidia kumpa mama protini mwilini. Vitamini A na madini ambayo itasaidia kuzuia kupatwa na maradhi na magonjwa mbalimbali.

Lishe bora kwa mama ni muhimu sana wakati wa ujauzito. Humpa mama virutubishi muhimu kwa ajili ya maendeleo yake ya kiafya na yale ya mtoto aliye tumboni. Vyakula vya mapema katika mimba huimarisha  afya ya mama.  Pia husaidia mtoto kukua vizuri kimwili na kiakili.

Vyakula Vya Mapema Katika Mimba

vyakula vya mapema katika mimba

Kipindi cha kwanza cha ujauzito ni chenye mabadiliko mengi sana kwa mama. Hii ni kwa sababu ya ongezeko la homoni mwilini. Mabadiliko haya hutofautiana kati ya mwanamke mmoja hadi mwingine na pia kutoka kwa kipindi kimoja cha ujauzito hadi kingine. Awamu ya kwanza ya ujauzito huwa na kichefuchefu sana. Ni vigumu kuzuia haya mabadiliko katika mama kwani mwili unajiandaa kupokea mtoto.

Vyakula kama vile:

  • Jamii kunde. Mbegu za makundekunde ni sehemu muhimu ya chakula cha mama mjamzito. kwa sababu huwa na kiwango kikubwa cha protini. Kwa watu wasiotumia nyama, mbegu za Jamii ya kunde hutosheleza mahitaji yote ya protini
  • Mayai husaidia kumpa mama protini mwilini. Vitamini A na madini ambayo itasaidia kuzuia kupatwa na maradhi na magonjwa mbalimbali
  • Maziwa na vyakula jamii ya maziwa. Maziwa huwa muhimu kwa protini, calcium, vitamini na virutubishi vingi. Husaidia katika ukuaji wa mifupa na misuli
  • Nafaka na vyakula vya wanga. Hivi huupa mwili nguvu ya kufanya kazi na pia ukuaji wa mtoto Hivi ni kama mahindi, mtama na mihogo
  • Mboga za majani. Hizi mboga ni kama vile spinach,kabeji, mchicha. Zinafaa kuwa zenye rangi ya kijani iliyokolea. Hizi humpa mama vitamini A na B
  • Mafuta ya samaki. Haya husaidia katika ukuaji wa ubongo na macho ya mtoto
  • Chipsi na viazi. Chumvi ilioko kwenye viazi husaidia kukausha mate ambayo huwafanya baadhi ya wajawazito kuhisi kutapika mara kwa mara. Wanga katika viazi husaidia kurekebisha kiwango cha sukari katika damu
  • Limau na ndimu. Limau na ndimu huwa na uchachu ambao husaidia kukata hali ya kichefuchefu. Kunusha limau halikadhalika husaidia kupunguza hali ya kutapika. Pia unaweza kukamulia limau kwenye maji unao kunywa ama kwenye chai. Pia kunusa magada au majani ya limau husaidia kupunguza hali ya kichefuchefu
  • Vyakula vyenye protini na vitamini B6. Vyakula vyenye protini kwa wingi na vitamini B6 husaidia mama kupunguza hali ya kichefuchefu. Hushauriwa kuwa mama mjamzito aepuke vyakula vyenye viungo na mafuta mingi. Hivi vyakula huzidisha hali ya kichefuchefu na hali ya kuhisi kutapika
  • Tangawazi pia ni muhimu sana kwa kusaidia katika kupunguza kichefuchefu. Hii unaweza kuongeza kwenye chai

vyakula vya mapema katika mimba

  • Kunywa maji mengi. Kunywa maji mara kwa mara ili kuzuia mwili kuishiwa na maji. Ni vizuri kunywa maji kwa wingi pamoja na juisi za matunda zisizo na sukari ya kuongezewa au kemikali za viwandani.

Ukosefu wa lishe bora husababisha matatizo mbalimbali ya kiafya:

  1. Mama kutoongeza uzito inavyotakikana
  2. Upungufu wa damu wakati wa ujauzito
  3. Kuharibika kwa mimba
  4. Kuzaa mtoto wenye uzito pungufu
  5. Mfumo wa kinga kuwa dhaifu

Vyakula huwa na nafasi kuu sana katika ujauzito haswa kwa sababu ya mtoto anayekua tumboni. Hivyo ni busara kuwa makini na vyakula vya mapema katika mimba.

Chanzo: healthline

Soma pia:Jinsi Ambavyo Mwanamke Anaweza Kufahamu Mimba Yake Ina Wiki Ngapi!

Got a parenting concern? Read articles or ask away and get instant answers on our app. Download theAsianparent Community on iOS or Android now!

img
Written by

Risper Nyakio

  • Home
  • /
  • Pregnancy
  • /
  • Umuhimu Wa Lishe Bora Mapema Katika Mimba Ni Upi?
Share:
  • Makosa Ambayo Wanawake Wajawazito Hufanya

    Makosa Ambayo Wanawake Wajawazito Hufanya

  • Vidokezo vya Ujauzito Wenye Afya kwa Mama Mjamzito

    Vidokezo vya Ujauzito Wenye Afya kwa Mama Mjamzito

  • Chakula Bora cha Kujifungua Mtoto Mrembo

    Chakula Bora cha Kujifungua Mtoto Mrembo

  • Makosa Ambayo Wanawake Wajawazito Hufanya

    Makosa Ambayo Wanawake Wajawazito Hufanya

  • Vidokezo vya Ujauzito Wenye Afya kwa Mama Mjamzito

    Vidokezo vya Ujauzito Wenye Afya kwa Mama Mjamzito

  • Chakula Bora cha Kujifungua Mtoto Mrembo

    Chakula Bora cha Kujifungua Mtoto Mrembo

Get advice on your pregnancy and growing baby. Sign up for our newsletter
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • More
    • TAP Community
    • Advertise With Us
    • Contact Us
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2023 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
About Us|Team|Privacy Policy|Terms of Use |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it