Vyakula Vya Mimba: Umuhimu Wa Kalisi Katika Ujauzito

Vyakula Vya Mimba: Umuhimu Wa Kalisi Katika Ujauzito

Ujauzito ni kipindi muhimu sana kwa mama na unapaswa kuhakikisha kuwa unachukua viwango tosha vya kalisi.

Mama mjamzito anastahili kuwa makini sana na lishe yake. Kwani anacho kula kina saidia na utendaji kazi mwilini mwake na katika kiinitete kinacho zidi kukua tumboni mwake. Je, una vifahamu vyakula vya mimba? Tuna kuelimisha zaidi kuhusu vyakula ambavyo mjamzito ana paswa kula ama kujitenga navyo.

Vyakula vya mimba: jitenge na vyakula hivi ukiwa mjamzito

vyakula vya mimba

 • Epuka kunywa mvinyo ukiwa na mimba. Kwani pombe zime husishwa na kujifungua kabla ya wakati kutimia na mtoto kuwa na matatizo ya kiakili, matatizo ya kimwili na kujifungua mtoto mwenye uzito wa chini.
 • Punguza unywaji wako wa kafeini na usizidishe miligramu 300 kwa siku.
 • Punguza ulaji wako wa ufuta unao kula kwa siku, na pia kiwango cha kalori unacho kula.
 • Punguza ulaji wa vyakula vyenye kalori, hakikisha kuwa haupitishi miligramu 300 kwa siku.
 • Jitenge na cheese kwani aina nyingi huwa hazija chakatwa na huenda zikawa na maambukizi.
 • Kamwe usile samaki mbichi
 • Kuwa makini unapo kula vyakula vya baharini na ujitenge na vitu kama swordfish ama mackerel kwani vina viwango vingi vya mercury.

Vyakula vya  mimba usipo hisi vizuri

Ukiwa na mimba, kuhisi kichefu chefu, kuharisha ama kukosa maji tosha mwilini. Huenda ikawa vigumu kubaki na chakula unacho kila ama ukahisi mgonjwa sana kula. Soma zaidi:

 • Kichefu chefu: Epuka kula vyakula vyenye pilipili nyingi, ufuta mwingi, ama mafuta nyingi. Badala yake, kula nafaka ama crackers kabla ya kutoka kitandani
 • Kukosa maji tosha mwilini: Kula matunda na mboga. Kunywa angalau glasi 6 ama 8 za maji kwa siku. Unaweza kunywa tembe za fiber pia
 • Kuendesha: Kula chakula zaidi kilicho na pectin na gums zinazo saidia mwili kutumia maji zaidi. Kama vile mandizi, mchele mweupe, oatmeal na mkate wa nafaka nzima
 • Kiungulia: Kula viwango vidogo vya chakula mara nyingi kwa siku, siku nzima. Jaribu kunywa maziwa kabla ya kula na upunguze kula vyakula vilivyo na kafeini na vilivyo na pilipili.

Vitamini muhimu ukiwa na mimba

vyakula vya mimba

Kalisi ni mojawapo ya virutubisho muhimu sana mwilini. Ina saidia kutengeneza meno na mifupa yenye nguvu. Pia inasaidia damu kuzunguka mwilini kwa urahisi, misuli na neva zina fanya kazi vyema na moyo kupiga kwa kawaida.

Kiinitete kina hitaji kalisi ili kukua. Na mama mjamzito asipo kula kalisi tosha kutosheleza mahitaji ya mtoto, mwili wake utatoa kalisi kutoka kwa mifupa yake, na kupunguza uzito wa mifupa. Mama ako kwa hatari ya kuugua maradhi ya mifupa isiyo na nguvu.

Ujauzito ni kipindi muhimu sana kwa mama na unapaswa kuhakikisha kuwa unachukua viwango tosha vya kalisi. Hata kama hakuna matatizo yanayo ibuka katika ujauzito wako. Ikiwa una matatizo ya kula vyakula vilivyo na kalisi, zungumza na daktari wako ili akushauri tembe za kalisi zitakazo kufaa.

Soma Pia: Ratiba ya lishe bora ya kuzingatia nchini Kenya ya mama mja mzito

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio