Vyakula Vya Watoto Vinavyo Tengenezwa Nchini Nigeria

Vyakula Vya Watoto Vinavyo Tengenezwa Nchini Nigeria

Hii ni orodha ya kampuni nchini Nigeria zinazo tengeneza chakula cha watoto.

Vyakula vya watoto  Nigeria hapo awali kilikuwa kutoka kwa kampuni za nje kama vile Cerelac, Gerber, na Nutrend. Na wakati huo, kampuni hizi ndizo zilikuwa zikiongoza. Cha kuhuzunisha ni kuwa wazazi ambao hawakuwa na pesa za kutosha hawangeweza kuwanunulia watoto wao vyakula kutoka kwa kampuni hizi. Leo mambo yame badilika.

baby food in Nigeria

Ila kwa sasa unapo fikiria kuhusu vyakula vya watoto nchini Nigeria, unaweza kufikiria kuhusu nafaka zenye virutubisho vinavyo tengenezwa nchini. Na vyenye aina nyingi pia. Kufanya hivi kunawasaidia wakulima wa Nigeria sana. Na kupunguza nafasi kati ya watu masikini na matajiri. Kwa sababu bidhaa hizi zina vifurushi vilivyo na bei nafuu. Tuna angazia baadhi ya kampuni zinazo tengeneza vyakula vya watoto nchini Nigeria.

Aina 6 Ya Vyakula Vya Watoto Nchini Nigeria

1. Trebites Baby Meals

Vyakula Vya Watoto Vinavyo Tengenezwa Nchini Nigeria

Trebites wanatengeneza chakula cha mtoto anaye anzishiwa chakula mbali na maziwa ya mama. Vyakula vyao vina virutubisho vingi kutoka kwa watoto wa umri wa miezi 6, kampuni yao iko Ogba, Ikeja, Lagos, Nigeria. Watumie ujumbe mfupi kwenye Instagram ama WhatsApp 07064503070.

2. My First Meals

vyakula vya watoto Nigeria

Hiki ni chakula asili cha mtoto kinacho tengenezwa na kwa njia asili. Wanatengeza chakula cha watoto wa miaka tofauti. Bidhaa zao ni asili, zina wingi wa virutubisho ambavyo ni muhimu kwa lishe ya mtoto wako. Na kufanya iwe rahisi kwa mama kuelewa zaidi kuhusu chakula, kula bila vikwazo na ukuaji wa mtoto. Wanatengeneza nafaka za watoto na maandalizi ya watoto. Soma zaidi kuwahusu kwenye mitandao yao ya Instagram na WhatsApp.

3. August Secrets

baby food in Nigeria

Augustsecrets Nigeria ni kampuni ya bidhaa za chakula cha watoto inayo ibuka; kusaidia wamama wa Nigeria na nchi zingine kuwalisha watoto wao chakula kilicho na afya zaidi ikilinganishwa na vitamu tamu vilivyo na sukari nyingi. Chakula hiki kina tengenezwa kwa kutumia bidhaa 100% asili. Ili kuhakikisha kuwa chakula hiki kina virutubisho tosha kwa mtoto.

Vinafanya hivi kwa kuangazia ushauri wa mtaalum wa chakula. Kwa hivyo wana tengeneza chakula na mahitaji ya virutubisho kutoka miezi 6 hadi miaka 5. Pia wanaboresha maisha ya wakulima wa Nigeria. Kwa ujumbe zaidi, som hapa.

4. Baby Grubz

vyakula vya watoto Nigeria

Baby Grubz wanatengeneza chakula cha mtoto kisicho na kemikali na ni nzuri kwa afya, ukuaji na maendeleo ya watoto wachanga. Kutoka kwa watoto wachanga hadi kwa wanao karibia kuenda shuleni, watoto wanapenda Baby Grubz. Ina virutubisho vilivyo sawasishwa kama lengo, watu wengi wanapenda chakula hiki. Aliye anzisha chakula hiki ni mtaalum wa virutubisho na bidhaa zao zitamsaidia mtoto wako kuongeza uzito.

Anwani yao ni 1B, John Adeoti close, LASU Road, Ojo, Lagos. Pia unaweza wasiliana nao kwa kupitia kwa mitandao yao ya kijamii kama vile Instagram na tovuti yao.

5. Tomi's Treats

Vyakula Vya Watoto Vinavyo Tengenezwa Nchini Nigeria

Tomi's Treats ni asilimia 100% ya chakula cha mtoto cha kikaboni. Bidhaa hizi zina wekwa kwa kifurushi kilicho rahisi kutumia kwa mtoto na watoto wachanga. Soko yao kuu ni nchi za Magharibi za Afrika. Tomi's Treats wamehakikisha kuwa mawasiliano ni rahisi kwa kupitia ☎️simu ✉️barua pepe na tovuti. Iwapo ungependa kutembea ofisini mwao, anwani yao ni 6 Efunleye Street, Off Talabi, Off Adeniyi Jones, Ikeja, Lagos, Nigeria.

6. Nandy's Munchies

vyakula vya watoto Nigeria

Nandy's Munchies ni bidhaa yenye virutubisho vya asili vya mtoto. Vina husisha bidhaa za kemikali. Lishe hizi zinasaidia na kuchakata chakula tumboni. Wasiliana na Nandy's Munchies kwa kupitia simu ama mitandao ya kijamii.

 

August Secrets

Baby Grubz

Soma pia: Back To School Meals Your Kids Will Enjoy

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Ayeesha kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio