Jinsi Ya Kupunguza Uzito Wa Mwili Kwa Kutumia Lishe Ya Alkaline

Jinsi Ya Kupunguza Uzito Wa Mwili Kwa Kutumia Lishe Ya Alkaline

Lishe ya vyakula vyenye alkaline inasifiwa na kutumika sana na watu walio na lengo la kupunguza uzito na walio na mzio wa vyakula fulani.

Watu mashuhuri wana ifahamu na kuisufu lishe ya alkaline, kwa imani kuwa vyakula vyenye alkaline vinasaidia pakubwa katika kupunguza uzito wa mwili na matatizo yanayo ambatana na uzito mwingi wa mwili. Kama vile kisukari, matatizo ya mifupa na miguu ama hata saratani.

Utafiti una dhihirisha kuwa kuna baadhi ya vyakula vinavyo ufanya mwili wako kutoa asidi ambayo ni hasi kwa afya yako. Vyakula kama vile nyama, ngano, wanga ulio chakatwa, sukari zaidi na vyakula vyenye trans na unsaturated fats.

Unapaswa kula nini?

vyakula vyenye alkaline

Ina aminika kuwa kula vyakula vyenye alkaline hufanya mwili wako uwe na alkaline zaidi, kukulinda dhidi ya kuwa na asidi nyingi mwilini na kukusaidia katika kupunguza uzito.

Aina nyingi za matunda na mboga na pia njugu huwa vyakula vya alkaline.

Hata ingawa vyakula kama maziwa, mayai, nyama na nafaka nyingi na vyakula vilivyo chakatwa huwa kwenye kundi hili, havikubalishwi kwenye lishe hii ya alkaline. Epuka kutumia vileo na kaffeini.

Lishe hii ni sawa na ya vegeterian, ya watu wasio kula nyama. Usile ngano ama gluten ya aina yoyote ile. Inasaidia watu wanao punguza utumizi wa sukari na walio na mzio ya aina fulani ya chakula. Kama mayai, samaki na shellfish.

Kundi la chakula    Chakula cha kuepuka

vyakula vyenye alkaline

Mboga                                 Kitunguu mbichi, pilipili

Matunda                            maji ya machungwa, nyanya, limau, ndimu, sharubati ya cranberry

Nyama                                nyama zenye mafuta nyingi

Maziwa                               Ice krimu, krimu iliyo ganda, milkshake

Nafaka                               spaghetti kwa mchuzi

Vinywaji                            Mvinyo, vileo, kahawa

Kufuata lishe ya vyakula vya alkaline kuna maana kuwa unachagua kula matunda na mboga na kutupilia vyakula vyenye wanga na kalori nyingi. Kujitenga na vileo na kahawa nyingi. Manufaa ya aina hii ya lishe ni kuwa inakusaidia kupunguza uzito, kulinda afya yako ya moyo, kupunguza shinikizo la damu na matatizo yanayo ambatana na ugonjwa wa moyo.

Lishe hii ya vyakula vyenye afya inakusaidia kuwa na afya bora. Kumbuka kufuata kwa makini yote tuliyo angazia, na kujitenga na vyakula vyenye asidi. Ijaze sahani yako na matunda na mboga tulizo angazia.

Soma Pia: Vyakula 7 Bora Ambavyo Wanaume Wote Wanapaswa Kukula

Written by

Risper Nyakio