Mama mjamzito huwa katika hatari kubwa ya kuugua anemia katika mimba. Ukosefu wa madini ya chuma mwilini husababisha anemia. Katika hali hii, mama hana seli nyekundu tosha mwilini za kusafirisha hewa kwenye tishu za mwili. Tunaangazia vyanzo, ishara, athari na kinga ya anemia in pregnancy. Je, nini vyanzo vya anemia katika mimba? Mama anaweza kujilinda dhidi ya kuugua anemia kivipi? Soma zaidi!
Vyanzo vya anemia katika mimba

- Hedhi nzito kabla ya kupata mimba
- Kuwa na mimba ya mtoto zaidi ya mmoja
- Historia ya kuwa na anaemia katika mimba
- Kutapika sana katika mimba ama hali ya ugonjwa wa asubuhi
- Kuwa na anaemia kabla ya kupata mimba
- Kupata mimba ungali mchanga
- Kutokula vyakula vyenye chuma tosha
- Kupata mimba iki fuatana
Ishara za anemia katika ujauzito
- Kuhisi uchovu wakati wote
- Kutatizika kupumua
- Kutatizika kumakinika kwa jambo moja
- Mpigo wa moyo wa kasi
- Maumivu makali ya kichwa
Athari ya anemia kwa fetusi
Kukosa chuma tosha mwilini katika mimba kunamweka mama katika hatari ya kujifungua mtoto ambaye hajakomaa ama kujifungua kabla ya wakati kufika. Kujifungua mtoto mwenye uzani wa chini ama mtoto kufa punde tu anapozaliwa. Mama aliyetatizika na anaemia katika ujauzito wake huwa katika hatari ya kupata postpartum depression.
Kulinda dhidi ya ukosefu wa damu tosha katika mimba

Ili kulinda dhidi ya ugonjwa huu, mama anastahili kula chakula chenye chuma tosha na chenye afya wakati wote. Lishe yake inapaswa kuwa na:
- Mayai
- Njugu
- Maharagwe
- Nafaka
- Mboga za kijani kama vile spinachi, sukuma wiki na broccoli
- Nyama nyekundu, nyama ya ndege wa nyumbani
- Samaki
Lishe inapaswa iwe na vyanzo vya vitamini C inayosaidia mwili kutumia madini ya chuma mwilini. Vyanzo hivi ni kama vile, nyanya, pili pili hoho, kiwi, matunda ya citrus kama machungwa na limau.
Kutibu anaemia kwa mama mjamzito
- Vitamini za prenatal huwa na chuma inayosaidia kutibu na kulinda dhidi ya ukosefu wa damu tosha mwilini.
- Lishe bora inalinda dhidi ya kupata anemia katika ujauzito.
- Kula vyanzo vya chuma kama nyama, sharubati ya machungwa, strawberries na nyanya.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Lishe Katika Mimba: Mambo Unayopaswa Kufanya na Usiyopaswa Kufanya