Insomnia ni nini? Kukosa usingizi usiku ni hali ambapo mtu hutatizika kulala anavyopaswa usiku, kulala kwa masaa machache ama kugutuka akiwa usingizini kisha kushindwa kulala tena.
Hali hii inaweza kuwa tatizo la muda mfupi (acute) ama muda mrefu (chronic). Kushindwa kulala kwa muda mfupi hudumu kwa kipindi cha usiku mmoja ama wiki chache. Huku kutatizika kulala kwa muda mrefu kukiwa kwa zaidi ya wiki tatu.
Aina za insomnia ama kukosa usingizi

Kukosa usingizi kwa kimsingi. Matatizo ya kulala hayahusishwi na matatizo mengine ya kiafya.
Kukosa usingizi kwa sekondari. Matatizo ya kiafya husababisha kukosa usingizi. Matatizo kama kusombwa na mawazo, saratani, kiungulia, uchungu, dawa, dawa za kulevya na vileo.
Vyanzo vya kutopata usingizi
Vyanzo vya kimsingi:
Mawazo mengi ya kimaisha. Kama vile kuwa na tukio kubwa siku chache zijazo, kufiwa na mwanafamilia ama rafiki, kusafiri ama kuwachwa na mchumba
Mazingara. Kuwa katika mazingira yenye kelele nyingi, temprecha ya juu ama mwangaza mwingi usiku
Kubadilisha ratiba ya kulala. Kuanza kufanya kazi usiku ama kutazama runinga usiku kunaweza athiri usingizi na kusababisha kukosa kulala usiku
Vyanzo vya kisekondari
- Dawa za hali za kiafya kama homa, mzio, shinikizo la damu
- Uchungu mwingi usiku
- Kutumia vitu kama kaffeini, pombe na dawa za kulevya
- Ujauzito husababisha kutopata usingizi usiku
- Uchungu na mabadiliko ya mwili kabla ya kipindi cha hedhi
- Kufika umri wa kutojifungua
Hatari za kukosa usingizi

Wanawake wengi hutatizika na hali ya kutopata usingizi ikilinganishwa na wanaume. Pia, watu wenye umri zaidi hutatizika na hali hii ikilinganishwa na watu wachanga. Kutopata usingizi usiku kwa muda mrefu kunaweza sababisha matatizo ya kiakili, kwani hupati wakati tosha wa kupumzika.
Ishara za kukosa usingizi usiku
- Kuhisi kulala mchanga
- Uchovu wa kupindukia
- Kukasirika ovyo ama kuwa na mhemko wa kihisia
- Kutatizika kuzingatia kazi unayofanya
Matibabu ya kutopata usingizi usiku
Hali ya kukosa kulala usiku kwa muda mfupi huenda isihitaji matibabu kwani huisha baada ya muda. Ikiwa ni vigumu kwako kufanya kazi zako za kila siku, daktari anaweza kushauri utumie tembe za kulala. Kumbuka kutotumia zaidi ya kiwango kilichoshauriwa.
Kwa kutopata usingizi kwa kipindi kirefu, matibabu yanahitajika kusuluhisha masuala ya kiafya yanayokusumbua. Baada ya kufanyiwa vipimo, daktari ataweza kufahamu chanzo cha kutopata usingizi na dawa bora kwako.
Kuepuka hali ya kutopata usingizi usiku
- Lala wakati sawa kila siku
- Epuka kutumia simu kitandani
- Epuka kula dakika chache kabla ya kulala
- Usitumie pombe na kaffeini dakika chache kabla ya kulala
- Fanya mazoezi kila siku ama mara kwa mara
- Unapokosa usingizi, usitumie simu, jaribu kusikiliza nyimbo za kupumzisha ama kusoma kitabu kigumu
Chanzo : Healthline
Soma Pia: Kipi Kinachomfanya Mtoto Wangu Kulia Usingizini?