Mara kwa mara, wanawake hushuhudia uchungu kwenye matiti. Ambao huja kisha kuisha bila matibabu yoyote yale, na mara nyingi sio chanzo cha kiwewe. Ni chanzo cha maumivu kwenye matiti?
Kuna uwezekano wa mwanamke kupata kiwewe anapo anza kuhisi uchungu kwenye matiti na kuhofia kuwa hii ni ishara ya saratani. Maumivu haya sio dalili ya saratani yasipo andamana na ishara zingine. Katika wakati mmoja ama mwingine maishani mwa mwanamke, lazima atashuhudia uchungu wa aina hii. Asilimia 70 ya wanawake hushuhudia maumivu haya maishani mwao.
Je, maumivu haya ni jambo sugu?

Maumivu machache mara kwa mara ni kawaida sana na sio jambo la kumtia mwanamke shaka. Walakini, kuna wakati ambapo mwanamke anapaswa kwenda kwenye kituo cha afya kufanyiwa vipimo. Ishara kama:
- Maumivu makali kwenye kifua
- Kuhisi kufura ama kuvimba kwenye kifua
- Shinikizo kwenye kifua
- Matatizo ya kupumua
- Kutatizika kupumua
- Kuhisi kizungu zungu ama kuzirai
- Kuhisi kichefu chefu
Maumivu makali ni ishara ya saratani?
Maumivu makali kwenye matiti sio dalili ya mwanamke kuwa na saratani. Walakini ni vyema kuwa makini na mwangalifu kujua iwapo maumivu haya yana ambatana na dalili zingine. Mwanamke anapo shuhudia ishara hizi anapaswa kuwasiliana na daktari wake.
- Uvimbe kwenye chuchu
- Mabadiliko kwenye maumbile ya chuchu zake
- Kufura kwa matiti
- Mabadiliko kwa umbo la titi
Vyanzo vya maumivu makali kwenye chuchu
Hiki ndicho chanzo kikuu cha mabadiliko kwenye chuchu. Mwanamke anapokuwa ana shuhudia kipindi chake cha hedhi, ata shuhudia maumivu na chuchu kuwa laini. Kufuatia mabadiliko ya viwango vya homoni mwilini katika kipindi hiki.
Aina hii ya maumivu huja kisha kupungua baada ya wiki moja, hata bila kutumia matibabu yoyote.

Ujauzito huambatana na mabadiliko ya viwango vya homoni mwilini. Na kusababisha chuchu kuwa kubwa, chungu na laini.

Siku za kwanza za kunyonyesha huwa ngumu sana kwa mama. Kwa sababu ya uchungu anao hisi kwenye chuchu kufuatia mishipa ya maziwa kufungana.
Ili kutatua haya, anaweza jaribu kupiga masi chuchu zake, kuvalia sindiria bora na saizi inayomfaa ama kupaka mafuta kwenye chuchu zake.
Chanzo:
Soma Pia: Sababu Zinazosababisha Maumivu ya Kichwa Baada ya Kuvaa Miwani Mpya