Vyanzo Vya Mimba Ya Mapema: Jinsi Ya Kuweka Wasichana Wadogo Mbali Na Chumba Cha Kujifungua!

Vyanzo Vya Mimba Ya Mapema: Jinsi Ya Kuweka Wasichana Wadogo Mbali Na Chumba Cha Kujifungua!

Katika nyakati za hivi majuzi, viongozi kutoka nchi tofauti wamekuwa wakitafuta suluhu za vyanzo vya mimba ya mapema. Hizi ndizo baadhi ya suluhu bora.

Katika nyakati za hivi majuzi, watu wanao simamia haki za watu na viongozi wa dunia wamekuwa wakifanya kazi kukumbana na vyanzo vya mimba ya mapema. Jambo kuu la kuzingatia limekuwa kuepuka mimba isiyo tarajiwa wakati mabinti wangali wachanga. Mimba ya mapema sio kuhusu msichana mmoja tu ama familia yao; ila ina athiri jamii yote.

causes of teenage pregnancy

Mama wachanga nafasi kubwa ni kuwa wata wachana na shule. Huenda pia waka lazimishwa kuoleka mapema. Huku kuna maanisha kuwa jamii hizo zina poteza nafasi ya kupata madaktari, wakili, waandishi na waanzilishaji wa vitu vikubwa.

Utafiti mwingi umefanyika kwa mada hii. Umbali huu, wataalum wamefanikiwa kutambua vyanzo vikuu vya mimba ya mapema.

Vyanzo vya mimba ya mapema

• Kukosa masomo yaliyo sawa kimatibabu kuhusu ngono

• Kukosa maarifa kuhusu afya ya ngono na uzalishaji na haki za wanawake

• Kukosa mwongozo tosha unao wafaa watu wachanga na kuwashauri

• Shinikizo la kuingia katika ndoa ya mapema kudhihirisha uwezo wao wa uzalishaji

• Kudhalilishwa kingono

• Umasikini

• Kukosa masomo: watoto wasio enda shule wana nafasi zaidi za kupata mimba

Sababu sekondari zinazo sababisha mimba ya mapema katika nchi zinazo kua

1) Tamaduni

Katika nchi zinazo kua kama vile Kenya, mama wengi wachanga (miaka 15-19) wako katika ndoa za mapema ama za kulazimishwa. Watoto hawa hukosa maarifa kuhusu mbinu za kuthibiti uzalishaji na huwa na shinikizo kubwa kupata watoto na mabwana zao.

2) Umasikini

Kipato cha chini kwa wazazi na kukosa fedha tosha kunaweza fanya watoto wa kike kuwa katika hatari ya kupata mimba ya mapema. Wasichana wanapo kosa pesa za mahitaji yao ya kimsingi kama vile pedi za hedhi, nguo, chakula na vitabu, watu wenye nia mbaya wanaweza watumia vibaya.

Pia, familia masikini zina nafasi ya juu zaidi kulazimisha mabinti wao katika ndoa za mapema na wanaume wazee walio matajiri.

3) Kukosa masomo

Kiwango cha masomo cha msichana pia kina athiri. Mabinti walio na kiwango cha chini cha masomo ama masomo ya ubora wa chini wako katika hatari zaidi za kupata mimba ya mapema. Wasichana walio na kiwango cha chini cha masomo huenda wakawa mama wangali wachanga.

Athari za mimba isiyo kusudiwa katika wasichana wachanga

• Mwisho wa masomo yao

• Maisha ya kukosa na umasikini

• Nafasi ndogo za kuajiriwa

• Kutengwa

Cha kuhuzunisha, watu wasio na maarifa inayo faa hutazama ndoa kama nafasi ya kutoka kwenye familia mbaya ama shule zenye masomo duni. Hii ni sababu kuu ya mimba ya mapema.

4) Ukatili wa kingono

Ukatili wa kingono ni tatizo kubwa duniani kote leo. Visa vingi vya mimba ya mapema hutukia kufuatia kubakwa na kudhalilishwa kingono.

Nchi za Afrika zinaonekana kuwa na tatizo na watoto kudhalilishwa kingono. Nambari zina tia wosia. Utamaduni wa kunyamaza na kutenga walio athiriwa. Kiwango cha mimba ya mapema huenda kikaongezeka iwapo serikali haitafanya chochote kuhusu ukatili wa kingono.

5) Kukosa kupata masomo yanayo faa kuhusu ngono na mbinu za kujilinda kutokana na mimba

Kwa watoto wengi wachanga, ngono ni jambo lisilo julikana vyema, ucheshi, ama kitu ambacho mtu mwingine ana tarajia wafanye. Wengi hawana maarifa ya kimatibabu kuhusu mfumo wa kingono na afya. Hali ya kutaka kufahamu zaidi ni mojawapo ya vyanzo vya mimba ya mapema duniani kote.

Katika nchi ya Finland, watoto hupata masomo ya ngono mapema. Masomo ya utafiti yamedhihirisha kuwa watu wachanga kutoka nchi hii walianza kufanya ngono baadaye maishani kwa sababu wana maarifa tosha. Cha zaidi, visa vya kudhalilishwa kingono viko chini.

Katika nchi kama Nigeria, maarifa kuhusu ngono yana pitishwa kwa sauti za chini, na kufuatia jambo hili, watoto wengi hawapati masomo ya ngono kamwe.

vyanzo vya mimba ya mapema

Jinsi ya kupunguza mimba ya mapema

1) Wapatie maarifa yaliyo sawa kimatibabu kuhusu ngono

Serikali inapaswa kupatia shule jukumu la kuwafunza watoto kuhusu ngono katika shule ya msingi, sekondari na mashirika ya masomo zaidi.

Watu wachanga wanapokuwa na masomo yanayo faa ya kimatibabu ya ngono, nafasi kubwa ni kuwa:

• Kuepuka visa ambavyo huenda vikawa na matukio ya kingono

• Kuripoti watu wanao kudhalilisha kingono

• Kuelewa maagizo ya kukubali na kukataa jambo

• Kugeuza msimamo wao kuhusu kufanya mapenzi na nguvu

• Kuji dhamini na miili yao

Faida za masomo ya mapema ya ngono ni nyingi. Inapokuwa jambo la kawaida, chanzo kimoja cha mimba ya kawaida kitakuwa kimetatuliwa.

2) Kupata maarifa ya kuwaongoza na kuwashauri watu wachanga

Shirika za kiserikali na zisizo za serikali zinaweza anzisha masomo yanayo wafaa watu wachanga na kuwashauri kwenye jamii zao.

Utafiti umedhihirisha kuwa watu wachanga walio na hamu ya kujua mengi inaweza wafanya waingie katika tabia zilizo hatari. Kifaa cha kuwashauri kinaweza saidia kuelimisha watu wachanga wasio na maarifa. Ikikubalishwa, darasa hizi za kuwaongoza zinaweza wapatia ushauri kuhusu matibabu kwa mama wachanga na familia zao.

3) Kupanga kampeni za kungoja ngono hadi waolewe

Watu wachanga wanapaswa kufahamu kuwa kuto jihusisha katika ngono ndiyo njia pekee ya kuepuka mimba na maambukizi yanayo sababishwa na ngono na ukimwi.

Kampeni hizi hazi paswi kuorodhesha vyanzo vya mimba ya mapema tu. Zinapaswa kuwapa vidokezo na mbinu za kujiepusha na ngono. Waelimishaji wanapaswa kuongea kuhusu shinikizo la wana rika na kuongea kuhusu vidokezo vya kungoja hadi unapo olewa.

Chanzo: theBmj

Researchgate.net

Sexuality Education International 

Soma pia: Wamama Waongea Kuhusu Ngono: Hadithi Hizi Zitakuwacha Ukiumwa Na Mbavu!

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio