Wanawake wa umri zote kutoka kwa walio anza kushuhudia hedhi kwa walio fikisha umri wa kuto jifungua hushuhudia uchungu kwenye chuchu. Hata hivyo, uchungu kwenye matiti huwa maarufu sana kwa wanawake walio katika miaka yao ya kujifungua. Je, unafahamu vyanzo vya uchungu kwenye matiti?
Utafiti umedhihirisha kuwa asilimia 70 ya wanawake duniani kote hushuhudia aina hii ya maumivu maishani mwao. Kiwango cha uchungu na sehemu ambapo wana shuhudia maumivu haya hutofautiana na kuchangia pakubwa katika kufahamu chanzo na matibabu yake.
Huku ikiwa baadhi ya uchungu huu huisha bila matibabu yoyote, kwa visa sugu, baadhi ya uchungu huu huenda ukahitaji kutatuliwa kupitia kwa madawa.
Vyanzo vya uchungu kwenye matiti
- Dawa ama matibabu

Kuna aina ya dawa ambazo huenda zikamfanya mwanamke awe na maumivu kwenye chuchu. Baadhi ya matibabu yanayo husishwa na uchungu kwenye matiti ni kama vile:
- Matibabu ya hali za cardiovascular
- Dawa za kutibu baadhi ya hali za kiakili
- Dawa zilizo na homoni kama vile tembe za uzazi wa mpango
2. Upasuaji wa matiti

Kufanyiwa upasuaji wa matiti huacha kidonda ambacho huenda kika sababisha uchungu kwenye chuchu. Kiwango cha uchungu baada ya upasuaji wa aina hii kina tofautiana kati ya watu. Upasuaji huenda uka sababisha, uchungu unapo gusa sehemu iliyo fanyiwa upasuaji. Kuto hisi chochote ama kufa kwa neva za sehemu hiyo, ama uvimbe kwenye titi.
3. Saratani ya matiti
Huenda mwanamke akawa na saratani ya matiti bila kuhisi uchungu ama maumivu. Ila kuna baadhi ya saratani zinazo mfanya ahisi uvimbe na kiasi cha uchungu. Dalili za kuwa na saratani ya matiti ni kama vile, kutokwa na ute kwenye chuchu. Kuhisi uchungu sehemu moja ya titi. Uvimbe kwenye chuchu ama chuchu kuwa nyekundu.
4. Mastitis
Haya ni aina ya maambukizi ya chuchu. Wanawake wanao nyonyesha wako katika hatari ya kupata maambukizi haya. Dalili za maambukizi haya ni kama vile, kuhisi uchovu, uchungu, kufura na uchungu mwingi kwenye chuchu ama joto jingi.
Mbali na sababu hizi, ni muhimu kwa mwanamke kufahamu saizi ya sindiria zinazo mfaa. Kuvalia sindiria kubwa ama ndogo huenda kukamfanya ahisi uchungu kwenye matiti.
Njia za kudhibiti uchungu huu, ni kufanya mazoezi, kula vyakula bora, kupunguza unywaji wa kaffeini na kufanyiwa vipimo vya mara kwa mara na kupata matibabu yanayo faa.
Chanzo: WebMD
Soma Pia:Athari Chanya Za Kujichua Kwa Afya