Sababu 3 Kwa Nini Wanawake Hutoka Nje Ya Ndoa Kulingana Na Wataalum

Sababu 3 Kwa Nini Wanawake Hutoka Nje Ya Ndoa Kulingana Na Wataalum

Je, unafahamu kuwa asilimia 50 ya visa vya kutoka nje ya ndoa huanza na wanawake? Naam, wanawake pia hutoka nje ya ndoa. Na nambari ya visa vya wanawake kutoka nje ya ndoa inazidi kuongezeka!

Miaka 10 iliyo pita, 3 kati ya wanandoa 10 walitoka nje ya ndoa walikuwa wanawake. Miaka ishirini iliyo pita, ilikuwa vigumu kumpata mwanamke akitoka nje ya ndoa. Ila sasa, siku hizo zimepitwa na wakati. Wanawake wa kisasa wanafahamu wanacho taka, na kamwe hawaoni uwoga kukipata.

Lakini je, kipi kinacho sababisha wanawake kutoka nje ya ndoa?

 

wanawake kutoka nje ya ndoa

Wataalum kwenye nyanja ya ushauri wa kindoa na wenye uzoefu wa miaka mingi wana haya ya kusema!

  1. Simu- kitunguu cha nyumba

"Aliipenda simu yake kuniliko. Na pia alikoma kunikumbatia, kunipapasa na kunipa kipau mbele." Umeyasikia maneno haya hapo awali? Simu ina changia pakubwa katika wanawake kutoka nje ya ndoa, alisema Leonardo Talpo mshauri wa ndoa.

Wanawake wengi huteta kuwa mabwana zao huzidi kutumia Whatsapp, muda baada ya kutoka ofisini. Hata wanapo fika nyumbani, wakati wote wana mawasiliano ya kiofisi hadi usiku wa maanani. "Katika hatua fulani, siku shughulika tena. Ila sikuwa na furaha, hadi nilipo patana na mwanamme huyu..."

2. Kazi wakati wote bila muda wa kucheza

Sawa na kufanya riziki yako, kuingia kazini kila siku ni kama kuwa na orodha ya mambo uliyo yafanya na yale ambayo haujatimiza. Mwishowe utaanza kuchoka na kazi yako. Siyo? Ndoa sio kazi inayo hitajika kufanyika. Mazungumzo hayapaswi kuwa kuhusu watoto wakati wote na unapo hitaji kununua chakula cha nyumba.

Hii ni sababu nyingine kwa nini wanawake huenda wakapata wachumba nje. "Alikoma kuzungumza kutuhusu. Hakuniambia kinacho tendeka maishani mwake tena. Tunacho fanya ni kuzungumza kuhusu watoto na mambo ya nyumba tu". Wateja wa Leonardo walimweleza. Baada ya wanawake kutia juhudi za kutatua hali hii na kukosa kufaulu. Huenda wengi waka amua kutafuta wachumba wengine nje.

3. Hutimizi jukumu la mwanamme kwenye nyumba

wanawake kutoka nje ya ndoa

Sio kila mwanamke anaye taka kuchukua usukani, na kufanya uamuzi wote wa kinyumbani. Wakati mwingine, mwanamke anacho taka ni kwa mume wake kuwa mume wa nyumba. Mume wako anapo kosa kufanya uamuzi wa kinyumbani, na mwanamke asipo amua, hakuna kitu kinacho fanyika. Kuwachilia familia lolote lile litendeke sio njia bora ya kuongoza familia yako.

"Baadhi ya wakati nilihisi kana kwamba nina mtoto kwa nyumba badala ya mume. Baada ya kutwikwa majukumu yote ya familia kwenye mabega, mwanamke hujipata na upweke, na hasira na kukosa amani. Anapo pata mwanamme mwenye uwezo wa kufanya uamuzi, kamwe hataangalia nyuma.

Baadhi ya mambo yanayo changia katika ongezeko la wanawake kutoka nje ya ndoa ni utumizi mbaya wa simu. Mwanamme anapo kosa wakati wa familia yake na kuto timiza majukumu yake kama mwanamme wa nyumba. Ni muhimu kwa kila mtu kuhakikisha kuwa anatimiza malengo yake katika ndoa.

Soma Pia: Ishara Za Uraibu Wa Tendo La Ndoa Za Kuangazia

Written by

Risper Nyakio