Je, Mwanamke Ana Uwezo Wa Kuamua Wakati Ambao Atapata Mimba?

Je, Mwanamke Ana Uwezo Wa Kuamua Wakati Ambao Atapata Mimba?

Ni kweli kuwa mwanamke ana aina ya nguvu za kuongeza nafasi zake za kupata mimba. Ni wakati upi bora kupata mimba? Soma zaidi!

Kutunga mimba hutendeka manii ya mwanamme yanapo patana na yai la mwanamke. Lakini wakati wote sio rahisi kama ilivyo kutaja. Wakati ambapo baadhi ya wanandoa wanapata ikiwa rahisi kutunga mimba, wengine huenda waka tatizika na kuchukua muda zaidi.

Kulingana na utafiti, wastani wa wanandoa 1000 kati ya 85 hutunga mimba katika mwaka wa kwanza wa kujaribu. Asilimia 15 inayo salia wata jaribu kwa muda zaidi kabla ya kufanikiwa. Baadhi yao wata hitaji msaada wa kimatibabu kutimiza lengo lao la kupata watoto.

Wakati bora kupata mimba- unapaswa kupata mimba lini

Ikiwa wana ndoa wote wana afya, nafasi za kutunga mimba ziko juu wakifanya ngono masaa 24 ama 48 katika kipindi ambacho mwanamke ana ovulate. Huwa siku 14 kabla ya kuanza kipindi chake kijacho cha hedhi.

Ishara za kifizikia zinazo dhihirisha kipindi hiki

mitindo ya kulala ukiwa mjamzito

  • Joto ya mwili wa mwanamke huongeza kiasi
  • Kuna uchafu wa rangi nyeupe unao toka kwa uke wa mwanamke
  • Baadhi ya wanawake hushuhudia kuumwa na upande wa chini wa tumbo

Yai la mwanamke huishi kwa kipindi cha masaa 12-24 baada ya ovulation na manii yanaweza ishi kwa siku 4-7 kwenye mwili wa mwanamke, wanandoa wanapaswa kuwa makini na wakati. Kumbuka kuwa, kutunga hutendeka baada ya manii kupatana na yai.

Mtaalum wa uzazi ana shauri wanandoa kufanya ngono siku 2-3 kabla ya kipindi hiki chenye rutuba zaidi kwa wanawake. Na kutasaidia kupatia manii wakati tosha kufika kwenye fallopian tubes kungoja kuachiliwa kwa yai.

Walakini, baadhi ya wanawake huwa na vipindi vya rutuba visivyo vya kawaida.

Wanandoa wanao kusudia kutunga mimba wana shauriwa kufanya mambo yafuatayo:

jinsi ya kulala ukiwa na homa

  • Kufanya ngono mara kwa mara

Ni sayansi rahisi. Ili kutunga, una stahili kufanya ngono mara zaidi. Wataalum wana shauri angalau mara moja baada ya kila siku mbili ama tatu ila pale unapo kuwa ukishuhudia kipindi chako cha hedhi.

Baadhi ya wanandoa pia hufanya kosa la kuwa na ratiba ya kufanya ngono na kungoja hadi pale ambapo kipindi chao cha rutuba kina wadia. Epuka kufanya hivyo na mfanye mapenzi mara kwa mara.

  • Kuwa na uzito wa mwili wenye afya

Utafiti umeonyesha kuwa wanawake wenye uzito mwingi wako katika hatari zaidi ya kuwa na matatizo ya kupata mimba.

"Ikiwa ungependa kutunga mimba mbio zaidi, fanya mazoezi na ukule lishe yenye afya. Kunywa asidi ya folic na vitamini C. Ni njia nzuri ya kutengeneza tumbo yako kuwa na mimba."

  • Punguza mawazo mengi

Kuwa na fikira nyingi ni mojawapo ya sababu zinazo dhibiti watu kutunga mimba. Kukwazwa kimawazo sio salama kwa afya ya mtoto. Punguza mawazo na usifikirie sana kuhusu kupata mtoto. Watu wengi wanao pata watoto hufanya hivyo waki furahikia.Kwa sababu mwili umetulia na umefunguka.

  • Pimwa kuwepo kwa maambukizi ya kingono

Baadhi ya wakati, maambukizi hudhibiti ujauzito kutendeka. Ili kuwa na uhakika ni vyema kufanyiwa vipimo kisha utibiwe na uchukue dawa ikiwa una magonjwa hayo.

Hitimisho kuhusu wakati bora kupata mimba

Inapofika kwa kutunga mimba, uchaguzi umo mikononi mwako. Unaweza soma mzunguko wa hedhi ya mwanamke, fanya ngono mara kwa mara, fanya mazoezi ya kifizikia na uchunge afya yako ya akili. Yote mengine yasipo fuzu, jaribu matibabu ya kukusaidia kutunga mimba.

Vyanzo: American Pregnancy

NHS

Soma Pia:Vyakula Ambavyo Unapaswa Kuepuka Katika Mwezi Wako Wa Kwanza Wa Ujauzito

 

Written by

Risper Nyakio