Baada ya kufunga pingu za maisha, wanandoa huwa na shaka kuhusu wakati wa kupata mimba. Kama ilivyo kawaida, jamii na marafiki huwa wa kwanza kuwapa mawaidha kuhusu wakati bora wa kupata mimba. Jambo linalo washinikiza wanandoa. Je, mwanamke ana uwezo wa kudhibiti wakati wa kupata mimba?
Ni vyema kwa wanandoa kufanya kazi na mtaalum wa uzalishaji. Kuna mambo tofauti yanayo athiri uwezo wa mwanamke kushika mimba kwa kasi.
Kutunga ni nini na kunatendeka wakati upi?

Kutunga hufanyika manii ya mwanamme yanapo rutubisha yai la mwanamke. Lakini sio rahisi hivyo wakati wote. Wakati ambapo huwa rahisi kwa baadhi ya wanandoa kutunga mimba, wengine hutatizika na kuchukua muda mrefu.
Kulingana na utafiti uliofanyika, wanandoa 85 kati ya 100 hutunga mimba katika muda wa mwaka mmoja wa kujaribu. Asilimia 15 inayobaki huchukua muda mrefu zaidi. Baadhi yao watahitaji usaidizi wa kimatibabu kufikisha malengo yao ya kujifungua.
Ni muhimu kwao kusoma kuhusu viungo vya uzalishaji vya kike na kiume na majukumu yai. Ni muhimu kusoma misingi ya mzunguko wa hedhi wa kike na jinsi unavyo athiri uwezo wa kushika mimba.
Mzunguko wa hedhi huhesabiwa kutoka siku ya kwanza kipindi cha mwanamke kinapoanza. Siku chache baada ya kuisha, kati ya siku ya tatu na ya tano, ovari zake huachilia yai. Na uwezo wa uzalishaji wake kuwa juu katika kipindi hiki. Kwa hivyo ikiwa umekuwa ukishangaa wakati bora wa kupata mimba, una jibu lako.
Kipindi chake cha hedhi kitaanza kati ya siku 12 na 16 baada ya kupevuka kwa yai. Kwa kawaida, mzunguko wa hedhi huwa siku 28, lakini ni sawa kuna mzunguko wa hedhi mrefu ama mfupi zaidi.
Wakati bora wa kupata mimba

Ikiwa wazazi wote wana afya, nafasi zao za kutunga ziko juu wanapofanya mapenzi kati ya masaa 24 ama 48 baada ya kupevuka kwa yai. Wanawake walio na mzunguko wa hedhi wa siku 28 wana ovulate siku ya 14 ya mzunguko wa hedhi.
Ishara za kuovulate:
- Temprecha ya mwili wa mwanamke huongezeka
- Kutoa uchafu wa ukeni ama kamasi la uke
- Huenda mwanamke akahisi uchungu tumboni ovari zinapo achilia yai kwenye mirija ya ovari
Wanandoa wanao lenga kupata mimba wanashauriwa:
- Kufanya mapenzi mara zaidi
Ili kuongeza nafasi za kutunga mimba, wanandoa wanapaswa kufanya mapenzi mara zaidi. Angalu siku mbili ama tatu katika kipindi cha mzunguko wao wa hedhi.
Kufanya mazoezi, kula chakula chenye afya ni muhimu kwa wanawake wanaolenga kushika mimba. Wanawake walio na uzito zaidi huchukua muda zaidi kushika mimba.
Kuwa na maambukizi ya kingono huziba uwezo wa kushika mimba kwa kasi. Wanandoa wanastahili kuhakikisha wamefanyiwa vipimo hivi na kupata matibabu.
Inapofika kwa wakati bora wa kupata mimba, kufahamu na kuelewa vyema mzunguko wako wa hedhi ni muhimu. Fanya mapenzi bila kinga katika wakati wao wa ovulation ili kuongeza nafasi zako. Yote yanapofeli, jaribu kutumia matibabu ya rutuba.
Vyanzo: NHS
American Pregnancy
Soma Pia: Orodha Ya Vidhibiti Uzalishaji Vilivyo Salama Unapo Nyonyesha