Wakati bora wa kutunga mimba ni mwanamke anapokuwa katika kipindi chenye rutuba, kwa kimombo fertile window. Kupevuka hutendeka yai linapo achiliwa kutoka kwa ovari na kusafiri kwenye mirija ya ovari. Yai halina uwezo wa kudumu kwa muda mrefu, lina uhai wa kati ya masaa 12 hadi 24. Mwanamke anapofanya ngono bila kujikinga, manii yana achiliwa kwenye uke wake. Kisha kusafiri hadi kwenye mirija ya ovari. Manii yakipatana na yai, yana lirutubisha. Manii yana uwezo wa kubaki hai kwa muda wa hadi siku tano.
Mwanamke huwa na nafasi zaidi za kutunga mimba anapo fanya mapenzi siku ya kupevuka kwa yai ama siku tano kabla ya siku hii.
-
Kufahamu siku ya kupevuka kwa yai

Njia rahisi zaidi ya kufahamu siku ya kupevuka kwa yai la mwanamke ni kuhesabu siku 14 kutoka siku ya kwanza ya kipindi chako cha hedhi. Ila, kulingana na daktari wa afya ya uke ya wanawake, vipindi vya hedhi hutofautiana na siku ya kupevuka kubadilika.
Kuna baadhi ya wanawake wanao amini kuwa wanaweza kufahamu siku ya kupevuka kwa yai inapokaribia. Kwa kuona mabadiliko yanayo fanyika mwilini. Dalili iliyo kawaida zaidi ni uchafu wa ukeni kuongezeka, siku chache kabla ya siku ya kupevuka kwa yai. Kwa wanawake wasio makini kuona tofauti hii, wanaweza kutumia kit ya kupima temprecha ya mwili na kufahamu siku hii inapofika. Temprecha ya mwili huongezeka.
-
Mara na wakati bora wa kufanya ngono ili kupata mimba

Wanandoa wanapo jaribu kutunga mimba, ni vyema kufanya tendo hili mara kwa mara ili kuongeza nafasi zao za kutunga mimba. Hakuna wakati hasa ulio bora kuliko mwingine wa kufanya ngono ili kupata mimba. Lakini kuna mbinu zinazo ongeza uwezo wa mwanamke kutunga mimba kwa urahisi.
Kufanya mapenzi kila mara kwa siku huenda kukafanya wanandoa wachoke. Ni vyema kutafuta kinacho fanya kazi kwenu. Kupumzika mara kwa mara ama kuchagua mara mtakazo kuwa mkifanya mapenzi kwa siku.
-
Muda unaochukua kupata mimba baada ya kufanya ngono
Kutunga mimba hufanyika baada ya manii kurutubisha yai kwenye mfumo wa uzalishaji. Hufanyika siku sita baada ya kufanya tendo la ndoa. Kisha yai lililo rutubishwa lita safiri hadi kwenye mji wa mtoto na kujipandikiza kwenye kuta zake. Na ujauzito kuanza.
Kwa wanandoa wanao tia juhudi kuwa wazazi, wakati bora wa kutunga mimba ni mwanamke anapokuwa katika siku zake za rutuba. Fuata vidokezo tulivyo angazia ili kuongeza nafasi zenu za kupata ujauzito.
Chanzo: healthline
Soma Pia: Mama Anaweza Tunga Mimba Anapo Fanya Mapenzi Anapo Nyonyesha?