Wakati Sawa Kumpa Mtoto Mdogo Maji

Wakati Sawa Kumpa Mtoto Mdogo Maji

Hapa kuna sharti muhimu la kukumbuka: Wakati sawa wa kumpa mtoto maji wakati unapo anza kumlisha vyakula vigumu, anapokuwa miezi sita.

Swali la wakati wa kumpa mtoto maji huwa kawaida kwa wamama hasa walio jifungua mtoto wao wa kwanza. Na hawana maarifa kuhusu kulea watoto na wakati wanapo paswa kuwaanzishia maji na vitu vingine. Kwa ujumla, mtoto wako hapaswi kunywa maji hadi anapo timiza miezi sita. Hadi wakati huo, anapata maji yote anayo hitaji kutoka kwa maziwa ya mama ama formula, hata kunapo kuwa na joto jingi. Hapa kuna wakati wa kumpa mtoto maji ya kunywa. Mtoto wako anapo fikisha miezi sita, ni sawa kumpa vijiko vichache vya maji anapokuwa na kiu. Usimpe vingi zaidi, ama utasababisha aumwe na tumbo ama kumfanya ahisi amejaa sana na kushindwa kula. Baada ya siku ya kuzaliwa kwake ya kwanza, anapokula vyakula vigumu ama kunywa maziwa, unaweza mkubalisha kunywa maji mengi anavyo taka.

Ikiwa unamnyonyesha mtoto wako peke yake, hakuna haja ya kumpa maji. Maziwa ya mama ni asilimia 88 maji na humpa mtoto vyote anavyo hitaji. Hata katika siku chache za kwanza baada ya kuzaliwa kwake, kabla ya maziwa ya mama "kuingia", colustrum inamfaa na kumtosha mtoto na kuhakikisha kuwa ana maji tosha mwilini (kama mtoto ana nyonya inavyo faa). Watoto wanao kunywa formula hawa hitaji maji zaidi. Baadhi ya vyanzo hushauri kumpa mtoto anaye kunywa formula maji kunapokuwa na joto jingi nje (hata kama mtoto anaweza pata maji zaidi kwa kula mara kwa mara), ama anapokuwa mgonjwa na joto jingi. Wasiliana na daktari wa mtoto wako aku shauri.

Mwongozo Na Hatua Za Kumpa Mtoto Maji

Wakati Sawa Kumpa Mtoto Mdogo Maji

Kuwanyonyesha watoto peke yake hakuhitaji maji ya nyongeza hata kukiwa na joto sana nje. Bora mtoto ana nyonya inavyo faa. Hata kunapokuwa na joto ama kumekauka, mtoto wako anaweza pata vinywaji vyote vinavyo hitajika kwenye maziwa ya mama. Utafiti tofauti unao chunguza faida za maji mtoto anapo lishwa maziwa ya mama peke yake ulifanyika katika sehemu tofauti (zilizo na baridi na zilizo kauka) katika joto kati ya 22-41°C (71.6-105.8°F) na 9-96% baridi ya wastani (angalia mfano hapa chini); masomo haya yali hitimisha kuwa kumnyonyesha mtoto peke yake kunampa vyote anavyo hitaji.

Wataalum wana shauri nyongeza katika siku za mwanzo kuna weza ingilia kati na kunyonyesha kwa kawaida. Nyongeza na maji ama maji ya glucose kuna ongeza hatari za jaundice, kupoteza uzito mwingi na kukaa muda mrefu hospitalini." Katika miezi ya kwanza sita ya maisha yake hata kama kuna joto jingi, maji na sharubati hazihitajiki kwa watoto wachanga wanao nyonya na huenda kuka fanya apate allergens za vizio ama uchafu mwilini.

Kwa watoto wachanga (hasa wiki 4-5), virutubisho/ nyongeza ya maji vinaweza kuwa hatari

Wakati Sawa Kumpa Mtoto Mdogo Maji

  • Watoto chini ya miezi miwili hawapaswi kupata maji ya kuongezea.
  • Maji ya kuongeza huenda yaka sababisha viwango vilivyo ongezeka vya bilirubin (jaundice), kupoteza uzito mwingi wa mwili na kukaa hospitalini kwa muda mrefu kwa watoto walio zaliwa tu.
  • Maji mengi sana yanaweza sababisha hali sugu ya oral water intoxication.
  • Mtoto anapokunywa maji ana hisi kushiba bila kupata kalori, kwa hivyo maji yata sababisha kupoteza kwa uzito (ama kuto ongeza uzito inavyofaa) kwa mtoto.
  • Watoto wanao kunywa maji wakiwa wachanga hawana hamu ya kunyonya. Na ikiwa mtoto hapati maziwa ya mama mara kwa mara inavyofaa, itachukua muda kwa maziwa ya mama kuweko. Huenda pia ika kawia ama kumzuia mama kuto pata maziwa mengi inavyo wezekana.

Kwa watoto waliopitisha hatua ya kuzaliwa hivi punde

wakati wa kumpa mtoto maji

  • Maji mengi sana huenda yaka ingiliana na kunyonyesha kwa sababu yana fanya mtoto ajae tumbo na anyonye kidogo. Watoto wanahitaji virutubisho na kalori zilizoko kwenye maziwa ya mama ili wakue -  maji hayana vitu hivi.
  • Maziwa ya mama yana maji yote ambayo mtoto anahitaji, hata kunapo kuwa na joto jingi.
  • Mtoto wako wa miezi 4-6 anapo soma jinsi ya kutumia kikombe, kumpa vijiko vichache vya maji mara chache kwa siku (sio zaidi ya ounsi 2 kila masaa 24) ni vizuri.
  • Mtoto wako anapo anza vyakula vigumu, huenda ukataka kumpa vijiko vichache vya maziwa yaliyo kamuliwa ama maji na vyakula vigumu. Baadhi ya watoto wanahitaji hivi ili kuepuka kukosa maji tosha mwilini.
  • Kwa watoto wa miezi zaidi, endelea kuwa nyonyesha na kuwapa maji kwa viwango vinavyo faa (ounsi 4-6 kwa siku). Maziwa ya mama huwa na maji tosha, kwa hivyo watoto wenye umri zaidi wanao nyonya bila kuthibitiwa wanaweza pata vinywaji wanavyo hitaji kwa kunyonya. Huenda wengine wakahitaji maji kidogo na vyakula vigumu kuepuka kukosa maji mwilini. Hakuna haja ya chupa - wape kikombe tu. Watoto wengi wakubwa wanapenda kunywa maji kwa kutumia kikombe cha wazazi wao.

Mtoto na Kukosa maji mwilini

wakati wa kumpa mtoto maji

Bora mtoto anakula vizuri na kuongeza uzito inavyofaa, sio rahisi kwake kukosa maji tosha mwilini. Ila pale ambapo ana homa, kukohoa ama matatizo mengine ya kiafya. Kukosa maji tosha mwilini kunaweza tendeka pale ambapo mtoto ni mgonjwa. Ama iwapo hawakunywi vinywaji toshi ama wanatoa vinywaji mwilini kupitia kwa kuharisha ama kutapika.

Unawezaje jua iwapo mtoto ana ukosefu wa maji mwilini na wakati wa kumpa mtoto maji ni upi? Mpigie daktari wako wa watoto bila kukawia iwapo unam badilisha mtoto wako diaper chache na chafu kuliko ilivyo kawaida, anakaa kulegea, kuchoka ama halii, ama ikiwa sehemu ya utosi wa kichwa chake kime bondeka. Huenda ukahitajika kumnyonyesha mara kwa mara, mpe mtoto wako electrolytes kama vile Pedialyte ama kwa kesi za dharura, huenda mtoto akalazwa hospitalini ili apatiwe IV fluids.

Kumbukumbu: Kelly

Soma pia: Je, Ni Maziwa Gani Bora Kwa Mtoto Mchanga?

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio