Ikiwa una mimba ama unapanga kupata mimba, huenda ukashangaa wakati wa kuacha kufanya mapenzi katika mimba. Umetafuta habari zote uwezavyo kuhusu kufanya tendo la ndoa katika mimba, na iwapo kuna athari hasi kwa mama na mtoto.
Ngono katika ujauzito ni mada isiyozungumziwa kwa sana. Watu wengi hudhania kuwa sio salama kwa mama mjamzito kujihusisha katika tendo la ndoa. Kutakuwa na mabadiliko katika maisha ya kingono ya mama mjamzito, hata hivyo, ni salama kufanya mapenzi.
Je, ni salama kufanya mapenzi katika ngono?

Tendo la ndoa ni salama katika hatua zote za ujauzito ulio salama. Ujauzito salama ni ule usio kuwa na changamoto kama kupoteza mimba ama kujifungua kabla ya wakati. Mabadiliko ya homoni mwilini mama anapokuwa na mimba huathiri hamu yake ya kufanya mapenzi. Hamu yake hupanda na kushuka ama akakosa starehe kufanya tendo la ndoa.
Mazungumzo ni muhimu kati ya wanandoa katika kipindi hiki, kwa njia hii, mama ataweza kumweleza mchumba wake anachotaka. Mitindo anayofurahia na inayomshinikiza na vitendo vingine vitakavyo mchechemua mbali na ngono.
Wakati wa kuacha kufanya mapenzi katika mimba
- Sio salama kwa mama mwenye historia ya kupoteza mimba
- Mama aliye na historia ya kujifungua mapema kabla ya wakati
- Mwanamke anapoanza kuvuja damu katika mimba
- Kuwa na ujauzito wa fetusi zaidi ya moja
- Mama anapotatizika kutokana na placenta previa
Je, tendo la ndoa katika mimba huathiri mtoto

La. Mtoto huwa amezingirwa na amniotic sac inayomlinda kutokana na hatari zozote.
Baadhi ya wanawake hushangaa iwapo tendo la ndoa linaweza kusababisha kuharibika kwa mimba. La. Ikiwa mimba ya mama ni salama, kufanya mapenzi katika ujauzito hakutaathiri safari yake ya mimba kwa vyovyote vile. Hata hivyo, wataalum wa afya hushauri wanawake kukoma kufanya mapenzi katika wiki za mwisho za ujauzito. Hii ni kwa sababu shahawa huwa na kemikali zinazoweza kuanzisha kubana katika wanawake.
Ikiwa una maswali zaidi kuhusu wakati wa kuacha kufanya mapenzi katika mimba, wasiliana na mtaalum wa afya. Unapokuwa na shaka kuhusu chochote katika safari yako ya ujauzito, ni muhimu kumweleza daktari kuhusu shaka zako. Ishara kama kuvuja damu, kutoa uchafu ukeni, maumivu wakati wa tendo la ndoa huwa hasi na wakati wote zinapaswa kuripotiwa kwa daktari kuhakikisha fetusi haijaathiriwa.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Vyanzo Na Jinsi Ya Kukomesha Kuvuja Damu Katika Mimba